Inakuwaje wanafunzi wanafeli hesabu wanafaulu physics na chemistry

Sababu masomo mengi ni yanahusu social skills za kijamii tofauti na science, kwenye social Kuna Hadi masomo ya governance, leadership na mambo ya gender
 
Sababu kubwa ya kufeli ni waalimu wengi wa hesabu kudhani ukali ndio kuwaelewesha wanafunzi. Matokeo yakr wanafunzi huishia kuwaogopa na hivo kuondoa umakini wakati wa kufundishwa. Hata shule zenye waalimu wa hesabu bado ufaulu hauridhishi hivyo sababu ya uchache wa waalimu haiwezi kuwa na uzito kusudiwa.
Kwa iyo walimu wa hesabu tuu ndio wakali ??
 
Sababu masomo mengi ni yanahusu social skills za kijamii tofauti na science, kwenye social Kuna Hadi masomo ya governance, leadership na mambo ya gender
Kwamba Physics na Chemistry ni social studies??? Yereuwiiiiiii!!!
 
Inakuwaje mwanafunzi anafeli hesabu halafu anakuja kufaulu chemistry na physics ,kumbe Tanzania kuna wakemia wengi aisee sikulijua hili wanafunzi wamepiga kemia jaman halafu hesabu kama kawaida chaliiiView attachment 2083593
Kweny Hesabu ni Issue ya Numbers tu lakn physics na chemistry utapat hat definition ya what is physics
 
Masomo ya Sayansi yanabebwa sana na Practicals. Mitihani ya Practical ni myepesi sana na kwa walimu wazoefu, mtihani anaujua kabla wote. Hata actual practical huwa hazifanyiki, kuna vimbinumbinu flani hv.
 
Kwa hiyo wakijibu maugoro wapewe tu maksi? Nani kakuambia mitego ya pysics na ya hesabu zinafanana wee kilaza?

Swali la pysics huwa lina sehemu mbili sehemu ya kwanza ni maelezo ya theory kama archimedes principle, Newton laws ,faradays law etc na sehemu ya pili huwa ni calculation ambazo ni simple zinazoendana na principle uliyoitaja.

Hutokea na mara nyingi ndivyo ilivyo mtu akawa amemeza principles zote na akazipata akijumuisha na baadhi ya calculations ambazo ni simple akama ukutafuta upthrust , mechanical advantage , velocity au voltage mtu anatoboa

Lakini hesabu mfumo wake ni tofauti huwa ni viswali ambavyo ni application ya formular fulani ambavyo wanategea vimitego fulani hivyo kama huijui ku derive formula husika au ubongo wako ni one way traffic na sio MULT SECTORAL unaingia chaka na kulikosa swali zima


Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Mimi tangu nipo shule na tena nilishawahi kuwaambia hata wanafunzi wenzangu kwamba ni rahisi sana kufaulu Physics au Chemistry kwa fact moja ya kwamba swali la physics la calculation linakuja direct na linajionyesha kuwa linataka nini kwa mfano swali la kutafuta density utatolewa maelezo mengi lakini mwisho wa siku data utapewa pale kwahiyo mwenyewe unamaliza kwamba Density=mass/volume na data zinakuwa given lakini sasa uje Maths weee utakuta umbo limekaa bila maelezo halafu unaambiwa utafute thamani ya X ujue hata uanzie wapi au tu swali linakuja simple tu simplify 2x2 − 6x + 2x − 3 sasa mzee wa kazi hapa hukuo hata utumie kanuni gani au uanzie wapi kudeal na hili swali,ugumu ndio unaanzia hapo kanuni sio constant maana kunanjoa nying ya kusimplfy swali hilo tofaut na physics ambayo inakuja na given data wewe kazi yako ni kupachika tu kwenye kanuni ya inayotumika lwa swali husika
 
watu wote waliosoma arts wanaamini mathematics ni ngumu kuliko physics na kwa bahati mbaya ndio wengi,sasa sijui tuwaambie ukweli au tuwaache tu
 
Hesabu za kwenye physcis ni za kujumlisha na kutoa na kugawanya tofauti na hesabu za kwenye hesabu, kuna kitu linear programming, circle, Matrix, earth as a sphere, trigonometry, statistcs hayo madubwasha huwezi kuyakuta kwenye physcs wala chemistry kwa hiyo mleta maada siku nyingine usilinganishe ufaulu wa somo lolote na hesabu, vitu viwili tofauti kabisa na havitegemeani
 
Back
Top Bottom