Inakuwaje viongozi watuambie nini tunahitaji badala ya kutusikiliza nini tunataka?

Jehanamu Hii

Member
Dec 16, 2016
41
125
Raia anatakiwa kuwa msingi wa mawazo. Yeye ndiyo wa kusikilizwa kwanza. Bila raia hao viongozi wangekuwa madarakani? Si sisi ndiyo tunaowalipa kwa kutumia kodi zetu na kuwapa uhalali wa kutawala mali asili za nchi kama zive machimbo ya madini, mbuga za wanyama, ardhi inayotoa gesi n.k ili zitutuletee faida sisi? Cha kushangaza naona viongozi ndiyo msingi wa mawazo--kwenye nchi yetu, na nchi nyingine za kimaskini nikimaanisha nchi nyingi za Kiafrika ukiachilia mbali Tanzania! Wao ndiyo wamegeuka kutoa amri ya nini tufanye badala ya kujaribu kutusikiliza tunahitaji nini. Mbaya zaidi, elimu yetu na maisha yetu kwa ujumla, hayamjengi mwananchi au mtu kudai haki yake. Inamjenga kufuata amri tu. Dhana ya kufuata amri tu bila kuulizia, inaanzia toka ngazi ya familia nikimaanisha mtoto na mzazi. Mtoto=fuata amri za mzazi bila kuuliza swali, mwanafunzi=fuata amri za mwalimu bila kuuliza swali, raia=fuata amri za viongozi bila kuuliza swali!!! Inasikitisha sana. Kwa mtindo huu tunakosa 'changamoto' ambayo ndiyo kichocheo cha mabadiliko. Hakuna mabadiliko pasipo changamoto! Nchi inayoogopa changamoto kama vile viongozi kukosolewa, haiwezi kuendelea.
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,595
2,000
huko ni kukosa mbinu za uongozi, ndio maana wanaona kipaumbele cha mtanzania ni kufanya mazoezi, mmhh... sijui ya nini wakati watu tunakula katikati ya mchana na usiku
 

Jehanamu Hii

Member
Dec 16, 2016
41
125
huko ni kukosa mbinu za uongozi, ndio maana wanaona kipaumbele cha mtanzania ni kufanya mazoezi, mmhh... sijui ya nini wakati watu tunakula katikati ya mchana na usiku
Mwamko unahitajika sana. Yaani, hii nchi bila watu kuamka na kuandamana kwelikweli hakuna maendeleo yatakayotokea. Viongozi wanafaidi upole wetu wa kukubaliana na hali. Hali hii siyo ya kuridhia. Lazima wananchi wafikie pahala pa kuona tunahitaji kusema kwa vitendo kama kwa lugha ya kawaida imeshindikana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom