Inakuwaje mpaka leo Mishahara UDSM bado?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Wakuu nashangaa sana mpaka jana ka account kangu bado katupu hapa UDSM kulikoni?????
 
Billioni tatu Igunga unadhani zimetoka wapi? Wakuu wote wa UDSM ni makada wa magamba unategemea nini?
 
Wanasubiri wakusanye tution fee maana serikali haitoe hela vyuoni ndio maana wanafunzi wote inabidi walipie kabla ya kufika chuoni.
 
Naanza kwa kuwapa pole ndugu zangu mnaofanya kazi serikalini,nimekuwa nikipata taarifa za hapa na pale kuwa mwezi uliopita (September) serikali imewakopa kwani mpaka leo hii tar 5/10/2011 bado watu hawajapata mishahara yao. Kwa cc tunaofanya kazi ktk makampuni binafsi hili ni jambo la kawaida.
Hofu yangu ni kwamba kwa hali hii serikali inataka kutuonesha nn? Kuna kipindi cha nyuma Mh. Zitto aliwahi kutoa kauli kuwa serikali imeishiwa,naanza kushawishika kuunga mkono hoja ya Mh.Zitto. Au hali ile ya kupita na bakuli kwenye maduka ya wahindi kuomba fedha za kulipa mishahara ndiyo inarudi tena? Kazi unayo mzee wa Magogoni .
 
Serikali ya ajab sana! Mi mwenyewe mshahara uliingia jana jioni! Mshahara wenyewe Mdogo afu wanashindwa ku2lipa watumishi!
 
UDSM walimu wengi wanaipinga serikali ya JK, kwa hiyo hii ni kama adhabu kwao. Kingine, serikali yetu inatumia pesa nyingi sana kwenye mambo yasiyo kuwa na tija n kuruhusu mambo yaende ende bila mpangilio. Ile nidhamu aliyoiacha mzee wa utandawazi kwa wafanyakazi saizi inapotea taratibu. Watu wanaanza kuona private sector zinalipa kuliko serikalini which is very dangerous for our country economy.
 
Poleni,serikali ni sikivu,itawasikiliza tu,si umeona mpaka leo tarehe 35 bado mshahara aujapata::
 
Nasikia hazina imekauka ile mbaya. Hii miaka 5 ni ya laana kwa watanzania. Hii inasababishwa na
1. Matumizi mabaya ya serikali
2. Ukusanyaji wa kodi ni mdogo kwa sababu biashara nyingi zimefungwa/hazifanyi kazi vizuri kwa sababu ya umeme
3. Uchaguzi wa Igunga (Refer 3+ billions zilizotumika kwa serikali kuhihujumu chadema)
4. Safari zisizoisha za JK
5. Ufisadi wa kutisha unaofanywa na viongozi wa serikali
6. Ukwepaji wa kulipa kodi
7. nk
 
UDSM walimu wengi wanaipinga serikali ya JK, kwa hiyo hii ni kama adhabu kwao. Kingine, serikali yetu inatumia pesa nyingi sana kwenye mambo yasiyo kuwa na tija n kuruhusu mambo yaende ende bila mpangilio. Ile nidhamu aliyoiacha mzee wa utandawazi kwa wafanyakazi saizi inapotea taratibu. Watu wanaanza kuona private sector zinalipa kuliko serikalini which is very dangerous for our country economy.

hata SUA hawajapata nafikiri ni kwenye public universities
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom