Inakuwaje mikopo ya TiGo na uhuru wa kupiga mitandao mingine?

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
125
Habari wana JF,

Leo asubuni nipo sehemu ambayo voucher za simu zinapatikani mbali kidogo. Alternative niliyonayo ni kukopa, hivyo nimepiga *149*05# nikapewa mkopo wa Tshs. 1300.
Lakini nilipojaribu kuipiga namba ya zain nilijibiwa kwamba sina salio la kutosha kuweza kupiga. Cha ajabu kingine ni kwamba baada ya muda mfupi jamaa alinipigia simu.
Sasa najiuliza je, TiGo wanafanya haki kweli kwa hili? Na je, kama una dharura ya hatari hawaoni kwamba inaweza kuleta madhara kwa sababu ya hii restriction yao?
Mwisho kabisa kwa nini wamtumie msg mtu niliyekuwa nampigia huku ningali na salio nililokopa? huku si kunidhalilisha kwamba naomba nipigiwe simu kwa sababu sina fedha za kutosha kwenye simu yangu?
Kwa mwendo huu nafikiria kuhamia Airtel kwani siwezi kurudi Vodacom tena.
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,914
1,115
Ni Kweli kabisa hatutendei haki, riba tunalipa halafu inakuwaje unashindwa kupiga mitandao mingine huo ni wizi.
 

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,436
1,579
Kazi yao kutujazia mamiziki ya ajabuajabu kwenye simu zetu, siku moja jamaa ananipigia anasikia bongo fleva kwenye simu yangu. Sipendi bongo fleva especially Mbagaraaaaa.
 

jameeyla

Senior Member
Aug 12, 2011
119
29
yaani tigo siipendi tabiya yenu kwanza nitawahama kama hamujirekebishi kwanini mnatuwekea nyimbo kwenye simu kwani tumewaomba kila mtu na uhuru wake sasa kutuwekea manyimbo wakati sijaomba wimbo manake nini,,cha pili mkopo na riba juu bado nikitaka kuutumia mkopo wangu kupiga simu nyingine hamutaki yaani nina salio la kutosha toka kwenye mkopo na kupiga simu pia unipe masharti acheni hizo huu sio UHURU WA KUONGEA sasa bali UTUMWA wa KUONGEA.
 

renfrid

Member
Sep 20, 2011
7
0
hapo kwenye mpango wa kuwekeana nyimbo bila kupenda co kabisa kwa m2 unawekewa wimbo eti cjui '' aliyeniacha mwanzo simtaki tena sijui nn na nn wanajua wenyewe'' hasa mnatuhalibia jaman, co mpango maana mtakuja kumwekea wimbo wa mapenzi padri hambaye hana mpenz na wimbo wa ni bebe ukamwekea shekh so mnatuvuruga....
 

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,022
1,766
Leo wameniboa,eti wamen2mia txt wanasema 2ma neno kaswida kwenda namba flani hvi kupata nyimbo za kaswida kila cku..sa cjui wanadhani kila m2 ni mwislamu au vp!
 

OTIS

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
2,237
799
Kazi yao kutujazia mamiziki ya ajabuajabu kwenye simu zetu, siku moja jamaa ananipigia anasikia bongo fleva kwenye simu yangu. Sipendi bongo fleva especially Mbagaraaaaa.

Waambie wakubadilishie wakuwekee dushelele.
OTIS.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom