Inakuwaje makosa ya kutakatisha fedha hayana dhamana wakati faini yake ni ndogo?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,743
141,604
Najaribu tu kuutafakari huu uwiano wa makosa ya utakatishaji fedha na adhabu zinazoendana na makosa hayo.

Ni juzi tu tumeshuhudia Jamal Malinzi na mwenzie Mwesiga wakilipishwa faini ya Sh. 500,000 baada ya kusota mahabusu kwa miaka.

Wako wakina Kitilya na Sioi nao wamesota sana rumande.

Naendelea kutafakari kama wanasheria wetu wanaijua sheria kama wale wa enzi za Pontio Pilato waliomjaribu Yesu kila wakati.

Maendeleo hayana vyama!
 
Sheria hii ni moja ya sheria mbovu sana kutungwa na watu wenye akili timamu, imetungwa kuwakomoa watu badala ya kutenda haki. Mtu sasa hivi akitaka kukuficha tu anakufungulia kesi ya utakatishaji pesa na uhujumu uchumi, can you imagine eti mtu anahujumu uchumi kwa shillingi milioni 17 !! Ujinga ulioje?
 
Back
Top Bottom