Inakuwaje Kenya, Uganda wanachimba Mafuta Bonde la Ufa sisi hatupati?

Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,449
717
Mimi si Mjiolojia, lkn ufahamu wangu unanitaka nijue kuhusu upatikanaji wa Mafuta. Uganda wamepata mafuta kwenye Ziwa Albert Bonde la Ufa Magh ambalo linapitia Ziwa Tanganyika na Kenya watachimba mafuta eneo la Turkana ambalo Bonde la Ufa Mash linatokea kwetu. Kampuni iliyopata mafuta nchi hizo ni Tulow Oil.
Mbona sisi Tz hatusikii hata dalili za mafuta ktk Bonde hilo ambalo sehemu kubwa liko kwetu? Au Tulow Oil hawatafuti mafuta Tz?
Najiuliza huku kwetu kuna nini kinaendelea.
Wataalamu mtujuvishe.
 
Kwa sababu hata pakichimbwa hakusaidii Taifa hili ,ngoja ule mradi wa kuzika bomba la mafuta toka Dar hadi kigoma utakapomaliza ! Na sijui umeishia wapi ?
 
Wacha kwanza shetani apite, muharibifu wa hazina zetu. Kwani watatumaliza Watanzania
wote, kwa tamaa ya utajiri. Baada ya mwaka 2015 mwangalizo wa uchimbaji ndio uanze.
Geological activity, zinajisemea wenyewe wazi wazi, kwamba kuna mkoa kaskazini, naficha
maelekezo, kuna mafuta mengi sana. Kuna ukanda mikoa ya magharibi kuna mafuta mengi sana.
Kuna mkoa kusini ya Tanzania, sisemi kama Magharibi au mashariki kuna mafuta mengi sana.
sasa basi tuache kama ilivyo na tungojee Serikali yenye maendeleo na usalama zaidi.
 
Mkuu chonde chonde usiseme kwa sauti..hawa viongozi wetu hawana fikra zaidi ya urefu wa pua zao watafilisi Mali asili zetu wakijua. angalizo Kigoda aliyepiga "Dili" za exploration karudi kwenye cabinet.
 
Kumbe hisia zangu huenda zina ukweli! Chini ya Ziwa Albert yanapochimbwa mafuta Uganda kuna Ziwa Tanganyika ktk Bonde hilo hilo la Ufa.
Tena tuna mabonde mawili ya ufa, wenzetu wana moja moja lkn mafuta bwerere, sisi vipi?
 
Tz hadi leo hatujapata mafuta, tuache longolongo, ila gesi tunayo. cha muhimu ni kuendeleza exploration tu ziwa Rukwa, Tanganyika na pwani yetu kule ambako gesi imepatikana. kama mozambique kule walikopata gesi nyingi kama yetu wamepata pia mafuta mengi sana, basi na sisi pengine kule kwenye gesi nyingi tutapata mafuta huko...vilevile, sijui huwa inakuwaje, manake gesi inapatikana tu kule ambako tumepakana na mozambique, sasa sijui kama wale wa mozambique wakichimba hawatachota na ya kwetu au isijemwagikia kwao kama sisi tutakuwa legelega kusubiri kuchimba haraka....la sivyo ndo ngumi huwa zinawaka hapo kati ya nchi na nchi....

kuhusu kenya na Uganda, ungeuliza kwanza why south sudan, manake mafuta waliyopata kenya ni maeneo yale karibia na south sudan, so is for Uganda wamepata maeneo yale karibu na south sudan, sidhani kama ni bonde la ufa pekee ndo kigezo. nafikir wenzetu wako kwenye mwamba ule wa south sudan.
 
Mkuu chonde chonde usiseme kwa sauti..hawa viongozi wetu hawana fikra zaidi ya urefu wa pua zao watafilisi Mali asili zetu wakijua. angalizo Kigoda aliyepiga "Dili" za exploration karudi kwenye cabinet.
Kama kuna mtu jambazi wa rushwa kubwa ktk nchi yetu ni huyu jamaa na mwenzie Daniel Yona. Sijui karudishwa kumalizia alichosahau ama vipi! Hawa jamaa walisimama kidete kuliua Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) ili wapige dili zao kilaini. Walishindwa,na hii angalau ndiyo ahueni tuliyonayo sasa. Sitashangaa ktk hizo account 6 za Uswizi majina yao yapo!
 
Mimi si Mjiolojia, lkn ufahamu wangu unanitaka nijue kuhusu upatikanaji wa Mafuta. Uganda wamepata mafuta kwenye Ziwa Albert Bonde la Ufa Magh ambalo linapitia Ziwa Tanganyika na Kenya watachimba mafuta eneo la Turkana ambalo Bonde la Ufa Mash linatokea kwetu. Kampuni iliyopata mafuta nchi hizo ni Tulow Oil.
Mbona sisi Tz hatusikii hata dalili za mafuta ktk Bonde hilo ambalo sehemu kubwa liko kwetu? Au Tulow Oil hawatafuti mafuta Tz?
Najiuliza huku kwetu kuna nini kinaendelea.
Wataalamu mtujuvishe.

Hayo Mafuta hata hayatoshi kwa biashara; labda kumwagilia mboga ndio Maana Kenya wamenyamaza Kimya; Midomo

Imeziba!!! Ungeshasikia something kama ni Mengi wow; EAC wangetaka wao ndio Marais wa kudumu na kila kitu!!!
 
Back
Top Bottom