Inakuwaje Filamu za ngono zinauzwa hadharani...?

.....Anyway,who is responsible?

Yeah, hilo ndilo la kujiuliza zaidi. Tumeona mamlaka inayosimamia vyombo vya habari jinsi inavyothubutu hata kutoa onyo kwa magazeti yanayotoa picha za nusu utupu zinazohamasisha ngono. Sasa sijui huku nani alaumiwe
 
Nilibahatika kutembelea nchi fulani za Magharibi. Maduka yanayouza vitu vya ngono ni sehemu wanayoingia watu wazima tu.

Nikashanga nilipokuta siku hizi, hata sigara zinafungiwa kwenye makabati na hazionekani na ukitaka sigara lazima wakinahi kuwa u mtu mzima ndio wakuuzie. Hata vinywaji vikali maduka yake tofauti hata supermarket hukuti vinywaji vikali vimeanikwa, mpaka uende maduka ya vinywaji na uwe umefikia umri wa kuingia humo.

Hapa kwetu hata bar utakuta watu wanaingia na watoto wadogo, utakuta mtu anampa mwanae beer, tana huku anajisifu "huyu anakunywa chupa nzima ya bia".

Usione tunavaa tai na makoti makubwa na tunaendesha magari ya mitumba ukafikiri Watanzania ni watu wa maana na wameendelea, hizo ni "cosmetics" na hazibadilishi mawazo na fikra za mtu. Hatuna maana hata kidogo, bado tuko nyuma sana kwa kila kitu chetu, na hii inatokana na kuwa elimu ya madarasani pekee haitoshi. Inabidi tubadilishwe "genetically" namna tunavyofikiri.

Kwa ufafanuzi zaidi nchi za magharibi pamoja na kuruhusu mambo hayo kuna sheria zinazothibiti uaendeshwaji wake, na kuna bodi maalumu zinazopitia maombi na kukagua mazingira kama hayana upenyo wa kuathiri wenye umri mdogo au wasiohusika. Mfano ni kama ifuatavyo:

Kibali cha kuuza aina ye yote ya kilevi (alcohol) hupitishwa na bodi maalum ya vinywaji ya serikali, na ukaguzi maalumu hufanywa na mtaalamu aliyebobea kama sehemu itakayouzwa bidhaa hiyo haiko karibu mno na nyumba za familia zenye watoto, shule na nyumba za kuabudia. Anayenunua kinywaji lazima awe na kitambulisho halali cha serikali au kama ni mgeni passport inayoonyesha kwamba amefikisha umri wa mika 21. Kama ni bar aliye chini ya umri wa miaka 21 haruhusiwi si kuingia tu bali hata kusimama eneo la bar. Mwuzaji lazima awe na kitambulisho cha serikali na awe na umri usiopungua miaka 21.

Kuna maduka ya majarida na vifaa vya kujamihiana ambavyo maduka yake hujulikana kama Adult Store XXX ambazo ni marufuku asiyefikisha miaka 18 kuingia humo na sehemu nyingine ni 21 years old. Kitambulisho lazima kionyehse umri wako kama kwa umbo waonekana mdogo. Maduka hayo yamedhibitiwa yasiwe maeneo ambayo ni shule, nyumba za kuabudia na makazi ya watu ambayo yana watoto.

Maduka yanayouza sigara yamefungia sigara sehemu maalumu na mwuzaji lazima awe na umri usiopungua miaka 18. Mnunuzi lazima awe na umri kuanzia miaka 18 vinginevyo hakuna huduma. Kitambulisho cha serikali ni utambulisho rasmi wa kupima kama amefikisha umri stahiki.

Na katika mauzo ya bidhaa hizo ipo sheria inayokataza two party sale, inaruhusu tu one party sale. Two part sale inamaanisha mmoja kumnunulia mwingine bidhaa ambazo hujulikana kama sensitive products to the minor ikiwa ni pamoja na tobacco, alcohol and adult sensitive material.

Sheria hizo ni kali na anayevunja kama ni mwuzaji ni kufungiwa biashara yake na kisha kutozwa faini, na pengine kupelekwa hata jela. Askari kanzu ndio wanawaliza sana hao kwani wanawatumia sana vijana wadogo kufanya mitego yao na wauzaji wasipokuwa makini hufikiwa kama ndege mjanja kunaswa katika tundu bovu.

Bongo tambalare, kwani utakuta baba au mama anamtuma mtoto mdogo kwenda kununua bia, sigara nk. Vijijini wazee wamekaa uwanjani wanamtuma mtoto mdogo kwenyea kuwanda kipande cha sigareti kndani, na mtoto kwa utundu anajaribia kuvuta kama moto umekolea vizuri. Wachuuzi wadogo (machinga) wanatembeza majarida ya ngono mitaani kama wanauza karanga vile. Hadi watu waandamane kisha watupiwe mabomu na polisi na kisha waandamanaji wauawe kwa kupigwa na risasi ndipo serikali itazinduka na kufanya utaratibu wa kuthibiti bidhaa hizo nyeti na hatari kwa malezi bora ya watoto?
 
majina hayo yapo,ila ni vizuri umuulize mwenyewe.kuna mtu namfahamu anaitwa namtamu,na nampenda.hayo majina yaliwapa shida sana shule

Mkuu mhusika wa jina amejieleza vizuri kuwa anaitwa Sweetbath. Kumbuka jina baya lilimponza mwenye jina.
 
mh iyo username yako inatega?napita tu

Mkuu umeniwahi...Topic inafanana na yuza nem....
Mwenye mamlaka ya ku-enforce Human Trafficking Act(Sections 4 & 7) ambayo
ime-criminalize porn in public ni nani??
Sheria ya magazeti(The Newspapers Act, 1976) pia imekataza haya mambo...
Au ndiyo mambo ya BONGO kila mtu ni Mlalamikaji, hakuna anayethubutu kuchukua
hatua...hata yule anayepaswa kuchukua hatua utamsikia akilalama...Mtoa mada
alipaswa kuchukua hatua kabla hajaleta malalamiko hapa...
TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO BORA
 
Watanzania tumeishiwa maadili, hata wewe unayelalamikia picha za ngono barabarani unatumia jina lililokaa kingonongono bila kujali kuwa JF kuna watu wa rika mbalimbali!..kwa vile wabongo ni wabishi utaanza kusema haukumaanisha hivyo navyofikiria, na niache kukufuatilia!..MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!

Aaaaaaaaaah yaaaaaaaaaa! Mi napita tu!
 
Mbona hizi ndude zilianza kuuzwa miaka mingi sana kama huamini ukifika kwenye Trafic yoyote ile hasa Ubungo na ukabahatika kuletewa CD ununue wewe mwambie tu "Nataka Pilau" fasta ataichomoa na kukupatia kwa bei nzuri tu, meanwhile, magazeti ya udaku ambayo sasa yamegeuka toka kwenye udaku kwenda kwenye ngono si yanasomwa na kila katoto kashule kwenye vituo vya dala dala ambako ndio wamegeuza meza za kuuzia magazeti? Nilishawahi kuona katoto kama ka darasa la nne au la tano pengine, kamesoma heading ya gazeti ambayo haiukuwa hata na chembe ya maadili ila kakaisoma kwa sauti kisha kakaishia kucheka sana na kukimbia pale Magomeni Mikumi mwaka juzi.....

Mi naona hii kitu maadili pia muizungumze kwenye katiba mpya! Ha ha haaaa
 
kwani hata zisipouzwa mtaani watoto hawazipati?
mbona tangu zamani haziuzwi mtaani lakini ukizitakia mtaani zipo zimejaa tele
BTW,rekebisha heading yako
 
Nilibahatika kutembelea nchi fulani za Magharibi. Maduka yanayouza vitu vya ngono ni sehemu wanayoingia watu wazima tu.

Nikashanga nilipokuta siku hizi, hata sigara zinafungiwa kwenye makabati na hazionekani na ukitaka sigara lazima wakinahi kuwa u mtu mzima ndio wakuuzie. Hata vinywaji vikali maduka yake tofauti hata supermarket hukuti vinywaji vikali vimeanikwa, mpaka uende maduka ya vinywaji na uwe umefikia umri wa kuingia humo.

Hapa kwetu hata bar utakuta watu wanaingia na watoto wadogo, utakuta mtu anampa mwanae beer, tana huku anajisifu "huyu anakunywa chupa nzima ya bia".

Usione tunavaa tai na makoti makubwa na tunaendesha magari ya mitumba ukafikiri Watanzania ni watu wa maana na wameendelea, hizo ni "cosmetics" na hazibadilishi mawazo na fikra za mtu. Hatuna maana hata kidogo, bado tuko nyuma sana kwa kila kitu chetu, na hii inatokana na kuwa elimu ya madarasani pekee haitoshi. Inabidi tubadilishwe "genetically" namna tunavyofikiri.

EXACTLY MR.ZOMBA, hatuangalii mbali..hututaki kufikirisha ubongo hata 25%..kweli Africa ni bara la giza..walisema!
 
watanzania tumeishiwa maadili, hata wewe unayelalamikia picha za ngono barabarani unatumia jina lililokaa kingonongono bila kujali kuwa jf kuna watu wa rika mbalimbali!..kwa vile wabongo ni wabishi utaanza kusema haukumaanisha hivyo navyofikiria, na niache kukufuatilia!..miafrika ndivyo tulivyo!

endorsed
 
taja mtaa hata mmoja tukajionee na sisi..

Nenda kariakoo zunguka mitaa yote wanaouza DVD za kutandaza chini, nenda ubungo mataa ukianzia pale songas mpaka huku nbc pia barabara ya samnujoma nenda buguruni sokoni, nenda mwenge kituo kikuu...
 
Back
Top Bottom