Inakuwaje Filamu za ngono zinauzwa hadharani...?

Mimtamu

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
368
105
Jamani wadau imekaa vp hii, maana kila kona jamaa wamezitandaza tena kweupeee! Sipendi hii kitu, ni aibu hasa kwa watoto zetu waliopo huko mitaani.
 
Nilibahatika kutembelea nchi fulani za Magharibi. Maduka yanayouza vitu vya ngono ni sehemu wanayoingia watu wazima tu.

Nikashanga nilipokuta siku hizi, hata sigara zinafungiwa kwenye makabati na hazionekani na ukitaka sigara lazima wakinahi kuwa u mtu mzima ndio wakuuzie. Hata vinywaji vikali maduka yake tofauti hata supermarket hukuti vinywaji vikali vimeanikwa, mpaka uende maduka ya vinywaji na uwe umefikia umri wa kuingia humo.

Hapa kwetu hata bar utakuta watu wanaingia na watoto wadogo, utakuta mtu anampa mwanae beer, tana huku anajisifu "huyu anakunywa chupa nzima ya bia".

Usione tunavaa tai na makoti makubwa na tunaendesha magari ya mitumba ukafikiri Watanzania ni watu wa maana na wameendelea, hizo ni "cosmetics" na hazibadilishi mawazo na fikra za mtu. Hatuna maana hata kidogo, bado tuko nyuma sana kwa kila kitu chetu, na hii inatokana na kuwa elimu ya madarasani pekee haitoshi. Inabidi tubadilishwe "genetically" namna tunavyofikiri.
 
Jamani wadau imekaa vp hii, maana kila kona jamaa wamezitandaza tena kweupeee! Sipendi hii kitu, ni aibu hasa kwa watoto zetu waliopo huko mitaani.

Watanzania tumeishiwa maadili, hata wewe unayelalamikia picha za ngono barabarani unatumia jina lililokaa kingonongono bila kujali kuwa JF kuna watu wa rika mbalimbali!..kwa vile wabongo ni wabishi utaanza kusema haukumaanisha hivyo navyofikiria, na niache kukufuatilia!..MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
 
Watanzania tumeishiwa maadili, hata wewe unayelalamikia picha za ngono barabarani unatumia jina lililokaa kingonongono bila kujali kuwa JF kuna watu wa rika mbalimbali!..kwa vile wabongo ni wabishi utaanza kusema haukumaanisha hivyo navyofikiria, na niache kukufuatilia!..MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
Ha ha haaaa!!Sina comment aisee duh!!
 
Mbona hizi ndude zilianza kuuzwa miaka mingi sana kama huamini ukifika kwenye Trafic yoyote ile hasa Ubungo na ukabahatika kuletewa CD ununue wewe mwambie tu "Nataka Pilau" fasta ataichomoa na kukupatia kwa bei nzuri tu, meanwhile, magazeti ya udaku ambayo sasa yamegeuka toka kwenye udaku kwenda kwenye ngono si yanasomwa na kila katoto kashule kwenye vituo vya dala dala ambako ndio wamegeuza meza za kuuzia magazeti? Nilishawahi kuona katoto kama ka darasa la nne au la tano pengine, kamesoma heading ya gazeti ambayo haiukuwa hata na chembe ya maadili ila kakaisoma kwa sauti kisha kakaishia kucheka sana na kukimbia pale Magomeni Mikumi mwaka juzi.....
 
heading zenu ziendane na mnayoandika, mnavuta attention yetu bila sababu

Mkuu, ninachoongelea hapa ni kitu kilicho wazi. najua kama hizi picha za ngono zinauzwa but systm ya sasa inayotumika ndio tatizo. jaribu kupitia hawa wauzaji wa DVD za kutandaza chini utajionea mwenyewe. wanazianika peupee tena mstari wa mbele. zamani ilikuwa mpaka umuulize ndipo akutolee tena kwa kujificha.
 
Back
Top Bottom