Inakuwaje Demu wa rafiki yako anapokumezea mate na kutoa visingizio/sababu lukuki?

malamia

Member
Aug 18, 2011
50
14
Ndugu wana JF,
Asaalam. mwenzenu nimepata mtihani, tena mtihani mzito. Dem wa mshkaj anadai jamaa hampendi na wala hana mpango nae kwani ni miaka 4 sasa hataki kusikia habari ya ndoa wala mapenzi ya karibu, staili ni kukutana kila baada ya mwezi angali wote wako hapa hapa DAR. Sasa huyu dem anadai bora hata mimi shem wake ambae sina mapepe na wanawake kama mshkaji. Mimi nimemwambia huyu dada mmmh!hilo tifu anatafuta alafu tayari ni shem wangu!, mwenyewe haelewi anadai atanifukuzia hadi kieleweke. Sasa sijui anataka aniendee Tanga, nikiingia line je na mshkaji si ataniona mimi ndo mchawi... jamani nisaidieni.....
 
Mkuu ungebadilisha hiyo heading kidogo neno demu sijui kama linasound vyema
Ila inategemea wewe na huyo rafikio mmeshibana vipi maana kama ni best friend wako na kuna uwezekano mkakosana kwa sababu ya huyo mwanamke ni bora ukae pembeni. Tena ikiwezekana mwambie kabisa kuwa huyo mwanamke wake hajatulia au ana madai ya ndoa na yeye kama mtu wake hajaonyesha dalili hizo
 
  • Thanks
Reactions: LD
achana naye huyo, jamaa yako atakutata koromeo ati
jamaa amesubiri matunda ya 'urafiki' yaive sasa yameiva wewe unamwambia asile! kama jamaa hana taimu na huyo manzi, kwanini msela asimsaidie? hapo anakuwa amemsaidia rafiki yake jukumu na huyo manzi at the same time kwa kukata kiu yake na pia kukidhi shauku yake wenyewe ya kujua kinachofichwa na shemeji yake huko kwa kufuli. ndo kuuwa ndege 3 kwa jiwe moja. mie sioni kosa hapo.eeh?
 
Mimi naona kama wewe pia unamtaka tatizo ni huyo mshikaji wako maana ukiwa humtaki its so easy kumtema. Waogopa Tanga atakufanya nini ukiwa unaamini mungu.
 
Sasa mshauri rafiki yako amuoe huyo mpenzi wake kuliko wewe umchukue labda wewe uamue kumuoa huyo binti sio amuache boy wake alf na wewe umchape alf usimuoe,
 
Usiombe akakuendee Tanga, yasije yakakupata yaliyonipata mimi. Mwenzio niliendewa Tanga kilichofuata ni jogoo kugoma kabisa kabisa kuwika maeneo mengine bali kwa mhusika tu. Sina jinsi imebidi niwe mpole na kuachana na tabia ya kuonja onja kabisaaa.
 
Sisi wanaume wote tunafanana bana..huwa tunatamani vitu vya ukweli ila tukishavipata ndo vile tena tunaanza kuvichkulia poa..kwa ivo mpotezee huyo..tafuta mwingine kaka..mtenda hutendwa
 
Ndugu wana JF,
Asaalam. mwenzenu nimepata mtihani, tena mtihani mzito. Dem wa mshkaj anadai jamaa hampendi na wala hana mpango nae kwani ni miaka 4 sasa hataki kusikia habari ya ndoa wala mapenzi ya karibu, staili ni kukutana kila baada ya mwezi angali wote wako hapa hapa DAR. Sasa huyu dem anadai bora hata mimi shem wake ambae sina mapepe na wanawake kama mshkaji. Mimi nimemwambia huyu dada mmmh!hilo tifu anatafuta alafu tayari ni shem wangu!, mwenyewe haelewi anadai atanifukuzia hadi kieleweke. Sasa sijui anataka aniendee Tanga, nikiingia line je na mshkaji si ataniona mimi ndo mchawi... jamani nisaidieni.....[/QUOTES

Sharing is caring...
 
Achana nae huyo shem wako kicheche atakuja kukupa headache baadae. Wewe umejuana nae kwa kupitia huyo mshikaji wako halafu ss hv anajifanya kudai jamaa yake si lolote hivi unadhani wewe ukiwa nae hatokuona kama anavyomuona huyo jamaa yake kwa sasa?
Huu ni ushauri tu ila maamuzi halisi yatakuwa kichwani mwako.
 
Kuwa makini wewe k=ndugu, hapo umetegwa tu....
hiyo ni technique ambayo wanawake huitumia kuwatongoza wanaume. unaweza ukakuta wanakutana na jamaa mara kwa mara ila ameona akuambie hivo ili umhurumie umpe anachotaka.
Usiharibu urafiki wenu kwa ajili ya ajili ya huyo mwanamke utajuta milele
Thanks
 
duuuhhh, jamaa akijua mazee itakua noma mbona, na kama alikuwa msela wako wa muda mrefu..ndo usela hamna tena..jama kama si muelewa utakuwa adui yake kwa muda mrefu sana..ina madhara kwa namna flani kama utaona poa tu..ila mazee mbona kuna mademu wengi tu wakali na hawana wanaume..ni bora ukawa na demu wako..hata kama si mkali sana..lakini hakuna kiwingu..unakula vitu vyako fresh tu..
 
It seems hata wewe mwenyewe unammezea mate cause ungekua unajiheshimu na kumuheshimu yeye kama shemeji yako wala huo muda wa kudiscuss hayo msingeupata..umejirahisisha sana kwa shem wako!
 
Ndugu wana JF,
Asaalam. mwenzenu nimepata mtihani, tena mtihani mzito. Dem wa mshkaj anadai jamaa hampendi na wala hana mpango nae kwani ni miaka 4 sasa hataki kusikia habari ya ndoa wala mapenzi ya karibu, staili ni kukutana kila baada ya mwezi angali wote wako hapa hapa DAR. Sasa huyu dem anadai bora hata mimi shem wake ambae sina mapepe na wanawake kama mshkaji. Mimi nimemwambia huyu dada mmmh!hilo tifu anatafuta alafu tayari ni shem wangu!, mwenyewe haelewi anadai atanifukuzia hadi kieleweke. Sasa sijui anataka aniendee Tanga, nikiingia line je na mshkaji si ataniona mimi ndo mchawi... jamani nisaidieni.....

Inaelekea unammezea mate huyo shemejio. Hii siyo issue nzito ya kuomba ushauri hapa JF! Akili za mbayu wayu, changanya na zako.
 
Hahaha Hiyo engene lazima umepiga sasa imekolea mavi2zi........... Hiyo dhambi umeshaifanya ndugu huhuhu......
 
Jombiiii naona ushapenda unatafuta tu go ahead humu jamvini....haya basi mkubalie yaishe!
 
Back
Top Bottom