Inakuwaje 'CT Scan' ya Muhimbili haifanyi kazi...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje 'CT Scan' ya Muhimbili haifanyi kazi...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 24, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo hospitali ya taifa. Inazo ct scans ngapi na hii imekuwa out of service kwa muda gani? Wanataka madaktari wafanye vip kazi? Vipimo gani vingine havifanyi kazi?

  [​IMG]

  Mashine ya aina hii inaweza kugharimu kati ya dola laki 2 hadi karibu dola laki tano na more sophiscated ones zinaenda hadi karibu ya dola milioni moja. Ninachojiuliza ni kwanini hizi zinaonekana kama ni luxury? Kwanini kila hospitali zisiwe nazo kwani hata tukisema tunatenga dola milioni 20 (Nusu ya fedha zilizochotwa na Kagoda) tunaweza kuhakikisha hospitali zote za mikoa zinamashine hizi! Lakini unajiuliza kama tunashindwa hata kutunza hako kamoja tena kwenye hospitali ya taifa itakuwaje kama tukipeleka Hospitali za mikoani? Kama mashine iliyoko Dar inachukua milele kuweza kutengenezwa itakuwaje kama mashine ingekuwa Kigoma au Katavi?
   
 2. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii ndio nchi yetu, hii ni miaka hamsini ya uhuru sijui tunasonga mbele au tunarudi nyuma.
   
 3. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii ndo nchi yetu,i ni miaka hamsini ya uhuru; sijui tunasonga mbele au tunarudi nyuma.
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  muhimbili ni kituo cha afya cha india,kazi yake kurefer wagonjwa india.
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hivi haiwezekani kubinafsisha baadhi ya vitengo hospitali hii ?
  Idara za maabara na vipimo, x-rays na CT scan, laundry, usafiri, sewage systems and sanitations zinaweza kubinafsishwa ili kuongeza ufanisi. CT scan inapoharibika itatengenezwa haraka ili wanaoimiliki wapate faida, pia watapigwa faini isipofanya kazi kutegemeana na makubaliano ya yaliyofikiwa.
  Hospitali yenyewe ibaki na core functions za Hospitali, kutibu.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwame, kwanza tungehoji hiyo cat scan ilinunuliwa mpya? Na pili ni kwa interests za nani kuwa na scanner MBOVU? ninaamini kuna mtu ananufaika somehow.
   
 7. g

  gogomoka Senior Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari yako Mwanakijiji,

  Hili suala la CT scanners, MRI na mazingira ya kazi kwa ujumla etc ni jukumu la Medical Association of Tanzania (MAT) kulipigania kwa nguvu zote. Sie wengine wote tutapiga kelele mpaka tuchoke lakini kama madaktari wenyewe kupitia MAT huwasikii anywhere wakiwa vocal kupigania hivyo vyombo na mazingira yao kwa ujumla basi ujue ndio tatizo. Sie wengine tukisema tutaambiwa tunafanya siasa kwa kuwa ni CDM/CUF/NCCR-Mageuzi.
  MAT inabidi walichukulie hili suala kuwa kwenye top 3 important objectives zao, ukiachia uboreshwaji Mishahara na Mazingira.

  Mwanakijiji unajua vizuri jinsi nilivyo bitter na hizi issue za madaktari toka kwenye thread uliyoweka iliyoandikwa na LULA MWANANZILA kuhusu kudharauliwa kwa madaktari. Honestly MAT is supposed to be more effective kuliko HAKIELIMU. Beneficiary mkubwa wa MAT ni huduma bora za afya kwa kila mtanzania. Hoja ya Kwame Nkurumah inaweza kutekelezwa effectively kama MAT watakuwa policy drivers na kiranja kwenye utekelezaji.
  Kazi njema!
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  saa zingine unanishangaza sana wewe

  sijui ndio kukaa sana nje ya nchi au ndio uko delusional...only God knows

  Mara ya mwisho umeenda Muhimbili lini?

  na kitu gani cha ajabu hapo kilichokushangaza?

  Hayo ni mambo ya kawaida sana na mengine ukija kuyajua utasema nini?

  btw tumetumia BILIONI 100 kwa ajili ya sherehe za uhuru and no one cares

  Hii ndio bongo
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Labda ungemwambia Pasco akupe CAG report ya Muhimbili

  then ungeona level of corruption kwenye Procurement ya Muhimbili nadhani utajiuliza whats the point?

  ever asked your self kwa nini JF sikuhizi hapa kwenye siasa hakuna anyeleta issues ambazo ni sensitive na expose za corruption?

  the answer is simple: JF is part of the problem kwenye hii cover up

  the most popular subforum ya JF ni siasa lakini imejaa nini?

  Nothing of public interest....kila kukicha ni CHADEMA vs CCM and nothing on issues kama ulizoraise

  eti ukileta malalamiko yanapelekwa Intelligence....a subforum no one even reads

  think!
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,120
  Trophy Points: 280
  Sasa unausifia huu upupu unaoendeshwa na serikali yetu au unamkosoa Mwanakijiji kwa kuliweka wazi? Eti hii ndio bongo..so??? tuendekeza upuuzi wa namna hii? wangapi wanao uwezo wa kwenda kutibiwa India wangapi wanakufa kwa kukosa huduma ya kawaida mahospitalini??? Kwa kweli umenishangaza sana tena sana.
  Viongozi wetu wanatumia pesa kiasi gani kukidhi mahitaji yao ya anasa kwa kutumia pesa yetu walipa kodi ambayo ingesaidia kununua CT scan mpya!
  Mkuu ni hivi tumechoshwa na huu uzembe wa kupindukia...leo madaktari wakigoma mnawalaumu ni haki yao kudai haki zao za msingi.....wabunge wanalipwa mamilioni ya pesa hakuna wanalolifanya zaidi ya kusinzia bungeni na kula raha kila siku hizo pesa si bpra zingenunua hiyo mashine!! ni hilo tu.
   
 11. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kuna mwaka mmoja.Nikiwa ofisini kwa Profesa mmoja (DR) Hapo Muhimbili akaingia mfanyakazi amefuata check ya kwenda lipa Lugalo Hospital garama za kusterilazi mashuka ya Theater zote za Muhimbili kwani Sterelizer yake ilikuwa imekufa so wakawa wanatumia ya Lugalo na wanalipia kila siku.nikaomba nikaione,nilipoiona nikawambia kuna nnaweza itengeneza,(ilikuwa na tatizo kwenye PLC programmable logic controler ) wanipe go ahead ntairipea,watanilipa after 3 mths wakishaitumia na kuridhika nayo.Head wa ufundi akakataa na kunitamkia KIJANA UNA HATARISHA AJIRA YANGU ikipona watajua mimi cjui kazi.mbali na kauli hii pia wanapata 10%.kuna madudu mengi sana muhimbili.Nna rafiki angu anafix Hizo CT Scan na X rays za hospital nyingi tu hapo Dar but sio kama huongozi aujui hilo ila ni ufisadi tu ndo umetawala pale
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwakijiji ilinunuliwa mpya from the manufactural, na oparators wakasomeshwa nje, imefanya kazi kama ilivyofanya ile military radar, ika malfunction due to electrical flactuation ya umeme usio wa uhakika. Sasa huu ni mwaka wa 3 unakwenda wa 4!.

  Wagonjwa wanakuwa reffered Regency, bili ni laki 600,000 kwa gari la muhimbili na laki 800,000 kwa gari la Regency. Hizo ni rate za mimi nilipoenda miaka 3 yuma!.

  Madaktari wanaokurecomend, wanapatiwa chochote kama wanavyokimbilia kurecomend India!.
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  halafu watu wakigoma kurudi bongo wanaambiwa sio wazalendo

  wakikosoa wanaambiwa rudini mrekebishe hali

  for what?

  TRA hali ndio hiyo hiyo

  MUHIMBILI uozo ndio middle name

  ukiwa na mawazo mapya unaambiwa unagatarisha ajira za watu

  uki criticise unaambiwa unatishia watu

  kila sehem imeoza

  ukitoa maoni yanaonekana yako too radical
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  tatizo sio sccanner tuu tatizo procurement process nzima ya Muhimbili ni OVYO

  Jiulize HEAD OF IT pale ni nani na ni mjukuu wa nani na alipata kazi kwenye mazingira yepi?
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Unakubali au unakataa kama JF is part of the problem?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ngoja nielezee hivi hili:

  Kwamba, kuna tatizo katika kusimamia mali za umma hilo halina shaka. Nimebahatika kusoma karibu ripoti zote za CAG kuanzia 2006 na ninazo nakala zake. Hakuna ambacho kinanishtua au kunishangaza tena. Tumeona ufisadi ulivyotamalaki kwa miongo sasa kwa hiyo hilo halihitaji mtu kumshawishi mtu mwingine. Ndio maana sioni sababu ya kufichua ufisadi zaidi kwani hakuna Mtanzania ambaye hajui aina ya ufisadi ambao upo nchini. Bahati mbaya sana hauihitaji kuwemo ndani ya Tanzania kuweza kuuona na labda wakati mwingine inaweza kuwa ni disadvantage kwako kuwa nchini kwani pressure to conform is tremendous.

  Lakini ukweli huo hauwezi kutufanya tukubali ufisadi au kuukumbatia na kuufumbia macho. Tutafanya makosa makubwa sana kama tutaanza kuonesha kuwa tumezoea ufisadi; hatutajitendea haki sisi wenyewe na wala hatutawatendea haki wale wanaokuja baada yetu. Ni lazima tuwe na moyo wa kukataa na kukataa kwa kwanza kabisa lazima kuwe ni kule kwa kifikra. Bahati mbaya sana watu wetu wengi na baadhi yao ni watu waliowahi kupita kwenye majengo ya shule au kupokea gamba la kuhitimu wamefika mahali wanakubali ufisadi kama ni kawaida.

  Watu wanachukulia yanayoendelea katika huduma za afya nchini kuwa ni kawaida; yanayotokea polisi kuwa ni kawaida, yanayotokea polisi kuwa ni kawaida na wengine hata wanajaribu kutushawishi kuwa ni sehemu ya mila na utamaduni wetu. Nani atakayekataa kati yetu? Kazi kubwa tuliyonayo ni kuzifungua fikra za Watanzania kukataa na ndio maana mgomo huu wa madaktari ni wakuunga mkono kwa sababu kama madaktari hawajafunguka kifikra nani mwingine kwenye jamii anaweza kufunguka?

  Walimu wamefungwa, wafanyakazi wamefungwa, waandishi wamefungwa na sasa tunagombea kuzifungua fikra hizo na hili si rahisi kihivyo. Ushahidi ni haya mapambano ya kifikra ambayo niliyaasisi na kuyapigania nikiamini kuwa kabla watu hawajaweza kubadili kura zao ni lazima kwanza wabadili fikra kwanza. Mapambano haya kwa kweli yanaendelea na sasa hivi nimegundua yamekuwa na ugumu wa aina yake; walio upande wa ufisadi nao wanajitokeza wazi kutetea ufisadi na kuuutafutia udhuru!

  Lakini tutashinda tu! Kwani gharama ya kushindwa watailipia watoto wetu!
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Swali la kujiuliza, hizo machine za regency na agha khan wanaziatamia kama mayai ndo maana hazifi? Hao waliosoma nje jinsi ya ku-operate machine hiyo hawakuambiwa jinsi ya kuhandle issues za umeme? Kupata huduma hiyo sio bure, kuna mchakato wa kuhakikisha mapato yake yana-ensure phasing out ya hiyo machine?
  Niliwahi kuwaza pengine mambo yangeenda kama watumishi wote wa serikali especially technical support wangekuwa wanapewa kazi kwa mikataba na kuongezewa baada ya review, lakini baada ya kuona mikataba ya miaka 5 ya urais na ubunge haijasaidia sana nikajikatia tamaa.
  Pasco umeongea kuhusu kutoa referral na kupata commission. Ufisadi tu kila mahali! Ni kweli, na cha ajabu ukipewa 'referal' hata ya maabara unapata majibu chap chap kuliko ukienda hapo kama individual!
   
 18. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hii nchi naamini wagonjwa wanakufa kwa umasikini wao.
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania haishindwi kununua CT Scan kwa kila hospitali ya Mkoa. Tuanzie hapo. Uwezo upo kabisa ila priorities ziko kushoto. Pili,hoja ya umeme vs. flactuations ni cheap excuse. Hospitali ya Regency iko Kenya? Wanafanyaje kukabiliana na flactuation ya umeme wa Tanzania hadi machine yao inafanya kazi? Huo utaalamu wanaotumia kuhakikisha machine yao inafanya kazi uko kwao (Regency) peke yao?

  Kama uongozi tulionao unashindwa kusimamia vizuri hii machine moja ya Muhimbili watawezaje kusimamia machine kama zingekuwa kila hospitali kubwa hapa nchini?

  Tatizo ninaloona sasa hivi hapa Tanzania liko kwenye 'implementation level'. Tuna sera nzuri lakini ukija kwenye utandaji kazi mambo ni hovyo kabisa. Pengine hii inatokana na kasumba mbaya ya kutowajibika. Kama mtu hana hofu ya kufukuzwa kazi hata kama amekuwata akiiiba kwa nini ajirekebishe? Na kama mkuu wa Muhimbili hana pressure ya kuhakikisha machine zinafanya kazi kwa nini ajisumbue?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kwa kweli ukiangalia sana unatakiwa kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Hivi kama Muhimbili hali iko hivi hayo mahospitali mengine mikoani yakoje? Je, vifaa vyao vinafanya kazi?
   
Loading...