Inakuwaje ATM ya Stanbic benk Ubungo, siku ya nne leo haina pesa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje ATM ya Stanbic benk Ubungo, siku ya nne leo haina pesa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Matope, Jul 3, 2011.

 1. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Naomba niwakilisha malalamiko yangu juu ya ATM ya Stanbic benk leo tarehe 3 mwezi wa saba ni siku ya nne haitoi pesa wanasababisha usumbufu mkubwa kwa sisi wateja wao hii inapelekea tutumie visa na kukatwa pesa nyingi!jambo la pili ikitokea bahati mbaya card yako ikanaswa kwenye Atm tofauti ya yao kuipata ni mpaka uombe mpya!binafsi ningeomba wabadilike usumbufu wa namna hii utapelekea mpoteze wateja wenu wa kwanza nikiwa mimi!!!!!!!!!
   
 2. g

  geophysics JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole nitawasiliana na wakubwa na kupeleka malalamiko yako maana nami ni mdau wao....
   
 3. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Waambie kaka kiukweli wanaudhi sana
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  pole sana.......siku nyingine nadhani utaamua kuwa na accounts bank tofauti tofauti kuepuka huo usumbufu
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Halafu hawa jamaa wana ATM chache sana, yaani inabidi nitolee pesa barclays au KCB au NBC pale Mlimani city coz ni Visa card. Ongezeni ATM jamani
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  mimi nilikuaga na account stanbic lakini walichonifanyia ilibidi nihame haraka sana,nakumbuka kuna wakati fulani nilikuwa na shida kubwa ya hela nikaenda kwenye ATM ya stanbic pale myfair nikachukua fedha ikatoka slip ikawa imenikata mara mbili ya ile pesa niliyochukua wakati hali halisi sijapokea hela mara 2,nikachoka sana kwa sababu hela iliyokatwa ilikua imebaki huko,fasta nikaenda kwenye office yao iliyoko palepale,nilichoambiwa nilichoka,wakaniambia kwanza nisubiri wiki mbili kama hazitarudi niandike barua ya kutoa taarifa baada ya hapo nisubir tena kama wiki mbili ya investigation jumla ni mwezi,nakuambia walinizungusha miezi miwili ndio hela yangu ikarudishwa,toka siku hiyo nilihama stanbic haraka sana,nikaamia TIB benk ndogo yenye ATM za umoja kibao sijapata tatizo hilo tena huu ni mwaka wa tatu.We cha kufanya hamia kwenye benk zenye ATM nyingi.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nashukuru umenikumbusha CRDB,ina wiki ya pili pale makutano ya SHAURIMOYO+LINDI,JAMANI!!!!!!PESA KAMA TUNAOMBA?????
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Huduma ya ATM Tanzania iko chini mno sijuhi tatizo liko wapi?
   
 9. g

  geophysics JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watanzania tunaharibiwa na majina makubwa tu eti ndo huduma safi..... Kama wengi wetu tungejua....bank nzuri bongo zipo na si NBC, NMB, CRDB...etc.... Huwezi kuamini TIB ni moja ya Benki ambayo wengi hawaitumii au kuijua vizuri lakini wana huduma nzuri sana.... Hawa Stanbic ovyo kabisa....sitaki niseme yote lakini TIB na Bank ya Posta sasa hivi wapo juu kweli kwa huduma ingawa Banki ya Posta bado wana ule userikali kidogo.
   
 10. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hawa jamaa wasumbufu sana me nahama benki fastaaaaa!!!!
   
 11. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimechukua kadi ya VIZA ya Stanbic najuta kuzaliwa mwanawane....nimekuja nayo nje ya nchi inagoma kila kukicha yaani bure kabisa hawa watu....Na nilitumia miezi miwili kupata hii kadi ya Viza yaani wanafanya mambo ya kingese ngese inaboa sana. Leo hii ni miezi takribani 6 niko huku ughaibuni kadi haifanyi kazi wakati ya CRDB inachanja mbuga....Mi nadhani wangefunga bank tu sio kutuwekea majengo huku huduma zikiwa mbovu kupindukia. Siongei haya maneno kiushabiki ila nina ushahidi 100% hawa jamaa kazi imewashinda hawabadiliki kwa kweli.
   
 12. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni bora wafunge kbs kwa mahesabu ya haraka haraka ni kama wana Atm nne Dar es salaam nzima duh nawapa pole!
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Stanbic inazingua sana atm zao chache sana...hapa dar!!na hiyo visa yao inaboa sana sijui tatizo nini nami najuta kuwafahamu!!!
   
 14. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Poleni sana kwa matatizo makubwa yanayowapata huko,karibuni Barclays jamani,huku wadau full starehe,customer care ya hali ya juu.Kwa kweli sijawahi kujutia kujiunga nao.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huduma za kibenki tanzania imekua kama mtu umeenda kuomba pesa......walioweka castama senta ukiwapigia hawapokei.....yannniiiiii
   
 16. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Barclays mhhhhh sidhani hata kama nina hamu ya kufufua akaunti yangu tuyaache hvy hvy humu lkn hatupo kibiashara zaidi wakuu!
   
 17. l

  ligera JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2014
  Joined: May 17, 2014
  Messages: 2,564
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  kuna siku nilienda benki moja kutoa ela kwenye account yangu ilikuwa asubuhi , kufika pale wahudumu wananishauri asubuhi sana nisubiri mpaka saa nne watu waweke kwanza fedha . nilichukia mno lakini nikawashauri kwa nini wasifanye biashara nyingine na waachane na biashara hiyo ya kibenki , bank teller wale walicheka sana.
   
Loading...