Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by juma sal, Jun 24, 2012.

 1. juma sal

  juma sal Senior Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.
  "Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

  Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?' Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!' Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!

  Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

  Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.


  Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

  Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

  Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.


  Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Jane alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima', alisema Jane tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake'. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

  Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

  Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

  Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa'. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini'. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

  Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Jane alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu'. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?' Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.'

  Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika "Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha". Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.
  Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
  Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema…

  Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao
  Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa   
 2. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ujumbe mzuri
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hii ni ka love story unaweza toa chozi
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duuuh.....umeniharibia jumapili yangu kwakweli!


  Imeniuma sana!
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba nilishaisoma habari hii b4, lkn again machozi yamenitoka!

  Inauma sana yaani.
   
 6. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duuh.. Inasikitisha lakini kuna somo nimepata hapo. Shukrani ndugu
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Si jukwaa langu lakini inafundisha sana jamani!

  Tunashukuru Jum sal.
   
 8. M

  Malolella JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Du ngoja nimsomee na mkewangu.
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dah mdau pole kama ni true story but i learned something today, you made my day
   
 10. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana....sob.... sob
   
 11. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  asante kwa kuitafsiri,me nliƮsoma ikiwa kwenye lugha ya malkia!
   
 12. G

  GTesha JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  umetransilate ile ya kingereza eeh? hakuna jipya
   
 13. A

  Anne deo JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Duh inasikitisha sana.
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Sijawai kulizwa na story lakini hii imenitoa machozi.

  So sad
   
 15. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  DU moyo unauma sana hii .machoz yanatoka
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  mmh! nimeumizwa sana lol !
   
 17. L

  Lukwa Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Somo tosha kaka!
   
 18. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shukran ni story nzuri na yenye mafundisho ndani yake
   
 19. Rodcones

  Rodcones JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 16, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  This is constructive story
  Inaonyesha Jambo forum ilivyokuwa miaka ya 2007
  ilikuwa saaafi kabisa na sio sasa
   
 20. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Its good to look back and do things that made you and your partner be together and happy.
   
Loading...