Inakuaje Tabora ambayo si tegemezi kwa kila kitu inakuwa na barabara nzuri kuliko Mbeya tegemeo la chakula?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
755
1,000
Nianze kwa kuipongeza serikali kwa kujenga barabara nyingi na nzuri sana hapa Tabora manispaa. Kwa wale waliofika tabora miaka ya karibuni watakubaliana na mimi kwamba serikali imewekea pesa nyingi kuijenga hii manispaa.

Naomba nieleweke kwamba sina tatizo kabisa na ujenzi wa miundombinu maadamu panapojengwa ni Tanzania na kwa fedha za watanzania. Jambo linalonisumbua ni kwamba shughuli za uzalishaji katika mkoa wa Tabora athari yake ina iko chini kutokana na hali yake kiuchumi na kijiografia.

Ninadhani serikali ingewekeza nguvu nyingi sana kujenga miundombinu kwenye mikoa ambayo athari zake kiuchumi ni kubwa na zinaathiri maisha ya watu wote mojakwa moja.

Mfano: ukiruhusu barabara ziwe mbovu kwenye mikoa kama mbeya, ambayo huzalisha mazao mengi sana ya chakula tegemeo karibu kwa nchi nzima na nchi jirani, unafanya haya mazao yasafiri kwa gharama kubwa sana na hivyo kuyafanya hayo mazao yasafiri kwa gharama kubwa sana. Na kwa jinsi hiyo unawasababishia hata hawa uliodhani kuwasaidia maisha magumu.
 

Galileo_Gaucho

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,236
2,000
Mkuu,hata tumbaku uzalishaji wake hauna positive impacts zozote?Huwa inanifikirisha jinsi sigara zinavyosindikizwa na bunduki tena kwenye ka-gari/pick-up tu.Halafu mahindi semi truck zima hakuna anayehangaika nalo.Jiunge nami kutafakari.🤔🤔🤔🤔🤔
Economic strengths za mkoa linganishi amezipuuza angejikita kuainisha umuhimu wa mbeya kiuchumi na uharaka na umahususi wa kuboresha mazingira wezeshi kwa mbeya wilaya za ileje,mbalali, mbeya rural, rungwe etc. Hata Mbeya Mjini barabara hovyo Mbeya ina wabunge matopopolo kabisa.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
7,248
2,000
Wakati namyetea Chalamila kwamba angalau kajitahidi kupambana na wapigaji hapo Mbeya mlikuwa mnabisha Sana.

Sasa kwa taarifa yako Mkoa wa Mbeya na Songwe imejaa wezi kupita kawaida,hakuna mradi kwenye mikoa hiyo umefanyoka vizuri.

Sio tuu Tabora hata Sumbawanga kuna barabara nzuri kuliko Mbeya.na watumishi wa huku na wananchi wao wanajali na ni waaminifu kuliko hiyo mikoa hapo juu.

Hapo Mbeya walipewa mradi wa TSCP(WB) km za kutosha lakini barabara zote walizojenga zimechimbika baada ya mwaka , saizi zimebakia mitaro.

Hiyo Tabora na miji mingine kama Sumbawanga walitekeleza mradi wa ULGSP chini ya WB na wasimamizi wakawa waaminifu ndio matokeo hayo unayaona.
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,775
2,000
Mbeya hakuna barabara,tatizo ni kwa viongozi na wananchi wanaowachagua!!!
Tabora ikikaza,Mbeya itaifukuzia mbali Sana!
 

venine

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
1,439
2,000
Hizo barabara zilifadhiliwa na World Bank kujenga barabara za kwenye miji/ majiji yaliyopo makao makuu ya mikoa. Je Mbeya hamkupata hizi pesa?

Au mkandarasi aliwaangusha? MKandarasi wa Tabora yupo vizuri sana. Kwa Morogoro pia nimeona barabara inayotoka Mafiga kupitia Mji mpya then to KIchangani hadi Nanenane, na nyingine kwenda Kilakala, Mkandarasi kaijenga vizuri sana.
 

Kimbuge

Senior Member
Dec 28, 2019
126
225
Mtoa mada mimi sijakusoma vizuri, hivi unazungumzia barabara za ndani ya jiji la Mbeya au kwenye mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake? Maana katika mkoa wa Mbeya, wenye wilaya za Kyela, Rungwe, Chunya, Mbarali na Mbeya yenyewe, zote zimeunganishwa na lami, hebu fafanua kidogo
 

wilmar

JF-Expert Member
Nov 27, 2018
200
500
Mtoa mada mimi sijakusoma vizuri, hivi unazungumzia barabara za ndani ya jiji la Mbeya au kwenye mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake? Maana katika mkoa wa Mbeya, wenye wilaya za Kyela, Rungwe, Chunya, Mbarali na Mbeya yenyewe, zote zimeunganishwa na lami, hebu fafanua kidogo
Mkuu mbeya barabara ni mbovu mfano anzia kabwe mpaka mbalizi potholes kibao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom