Inakuaje Mzee uajiriwe na kijana Tena mwanamke,na akutume!!!

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,375
Sometime nakaa nawaza na kushangaa na kujiuliza

Huyu Mzee mtu mzima anakubalije kuajiriwa na kijana Tena kama mtoto wake tu Tena ni mwanamke

Wewe Mzee miaka yote ulishindwa kabisa kupambana ukawa na biashara zako ambazo baada ya kustaafu/kufukuzwa/kuacha kazi ungeziendeleza na ukaajiri watu sawa na watoto wako wakasimamia?

Ni Mambo ya ajabu sana kwenda ofisini na kukuta mzee mzima amekaa katika ajira ambayo mwenye nayo ni mwanamke Tena sawa na mwanae na anatumwa na mwanamke huyo

Huku ni kujifedhehesha Sana Yani Mzee ujana wako wote umeshindwa kujijenga Hadi ukubali kutumwa na mwanamke /kijana sawa na mwanae wa kumzaa huku ukubwani,unakurupuka asubuhi kwenda kwenye kibarua ulichopewa na binti ambaye sawa na mwanao

Halafu nawe Mzee unaona ufahari kabisa na kumsifia huyo mtu anaekupa ugali Yani kuna wazee wengine wapumbavu Sana

Wewe kijana wewe Mzee andaa maisha yako na wanao sasa usisubiri ukaajiriwe na watoto wadogo wakupangie kazi ni Mambo ya aibu sana na ya kutia kichefuchefu Mzee kuajiriwa na mtoto tena mwanamke

Jipange Mzee.
 
mwambie huyo mzee wako aache kazi halafu maisha yakiwachapa ndo mtaelewa
 
Una miaka mingapi vile? Unaweza ukazitafuta ujanani na ukawa nazo nyingi sana lakini ukifika uzeeni zikapukutika na ukaajiriwa na binti ambaye yuko kwenye umri wa kuzitafuta. Kutafuta mali na kudumu nazo ni vitu viwili tofauti. Hakuna mtaalamu wa kuendeleza mali zifike mpaka uzeeni. Zinaweza kupotea kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako.

Naamini huyo anayefanya kazi kwa binti ana akili sana na anajua wajibu wake kwa familia aliyonayo ndio maana yuko hapo. Azoge Ze Blind Baga,
 
ukija zeeka utataka kuhesabiwa mmoja wa wenye akili,hekima na busara kisa umekula chumvi.

wakati toka ukiwa kijana ni mpumbavu wa kiwango hiki.
 
Huyo mwanamke anamiliki kampuni au nae nni mwajiriwa wa kampuni ya mtu mwingine ikiwemo serikali (ya watu wote)? Kama ni mwajiliwa basi si mwajiri, na huyo mzee anatumwa na mwajiri kupitia huyo mwanamke.

Kwani haruhusiwi kuachia ngazi kama sheria ya kazi inavyoelekeza?
 
Mwanamke! mwanamke ! Mwanamke! Mwanamke ! , mbona mwanamke umemshusha sana, umemzarau mno kana kwamba yeye hawezi kuajiri, kinachoangaliwa hapo ni hela na wala sio swala la umri wala jinsia,

Waache wadada walijenge taifa
 
Maisha hayana formula kabisa, napesa inaweza kuja baadae ikaisha, kwaiyo usidharau kazi wanazofanya wenzako. Komaa na maisha yako mazuri ambayo hautumwi na mwanamke.

Kuna kitu kinaitwa mind your own business, ushawai kukisikia?
 
Makamu Wa Raisi wako Ni mwanamke ... Vipi unaweza kutuachia nchi yetu ukahama ?
Mwanaume wote wanaofanya kazi chini ya mama Samia waache kazi. Utatumwaje na mwanamke?.

Wewe Mleta mada Ni zwazwa na hauna exposure,maboss kibao Ni wanawake .. Ina maana watu Sasa wakitaka kazi, Kama boss Ni mwanamke Basi waacha coz hawataki kutumwa na mwanamke...

Yaaani umekaaa umewaza umeamua kuleta thread ya kipumbafu namna hii..
 
Back
Top Bottom