Inakuaje miaka 60 ya uhuru DAWASA hawajalimaliza hata jiji la Dar es Salaam?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,767
2,000
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.

Leo ni miaka 60 ya uhuru lakini Dawasa hadi dakika hii hawajaweza kuyafikia maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Hii ni aibu sana na jambo la kusikitisha.

Hivi wanakwama wapi miaka 60 lakini hawajaweza, jee Tanzania nzima lini itakua na access ya maji kwa kila kijiji?

Naona itachukua miaka mingine 60 ndio tufikie Tanzania nzima ikiwa na maana ya jumla ya miaka 120.

Tuna safari ndefu!
 
Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,292
2,000
Kila mkoa una mamlaka yake ya maji mkuu.. Mwauwasa,Duwasa..n.k n.k

Mashirika haya changamoto kubwa ni
1. Ufinyu wa bajeti ya maji
2. Ufisadi miongoni mwa wakandarasi kwenye miradi ya maji
3. Vyanzo vya maji. Mfano Dar mnategemea maji toka mto Ruvu!
 
toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,767
2,000
Ufinyu wa bajeti mkuu wakat hawa jamaa wanatulipisha bill kubwa?
Kila mkoa una mamlaka yake ya maji mkuu.. Mwauwasa,Duwasa..n.k n.k

Mashirika haya changamoto kubwa ni
1. Ufinyu wa bajeti ya maji
2. Ufisadi miongoni mwa wakandarasi kwenye miradi ya maji
3. Vyanzo vya maji. Mfano Dar mnategemea maji toka mto Ruvu!
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,042
2,000
Yani maji ni shida kubwa sana!

Tangu Uhuru hadi leo maji ni shida kubwa sana!

Kila Mwaka bajeti zinasomwa na kupitishwa lakini maji hayapatikani wala nini.

Sijui tatizo ni nini
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,422
2,000
DAWASA na kampuni yao DAWASCO ni kituko kingine cha kuandikia historia, pengine vizazi vingi vijavyo viweze kusoma na kusema kweli wale zinjathropazi waliteseka kwa kukosa akili.

Maji yanayopotea ni zaidi ya maji wanayouza, hili wao hawajali, ni wakali kwa maji yanayopotea baada ya mita, kabla walaaa na hawana huo mpango wa kurekebisha na kuiboresha miundo mbinu yao ya usambazaji wa maji kukidhi ongezeko la watu Dar.

Kwa hii miaka Taifa lililoishi likiwa huru chini ys mkaburu mweusi, basi angalau stori za maji, barabara, hospitali, umeme, zisingekuwepo kwa mji huu na mingine kama 4 hivi.

Sasa miaka 60 ya matajiri na makaburu weusi wote kuishi Dar wakiwa huru, bado Dar haina tofauti na Namtumbo, wote wanalilia maji.

Kama wanahitaji na wana nia ya dhati, ongezeni bei ya maji ili muweze kupata pesa za kusambaza maji Dar yote, mbona tunachangia REA kwa lazima kwa kila unit moja ya umeme! Tzs 2000/1000ltrs ni ndogo ukilinganisha na sisi tuliokuwa tunanunua galoni moja la 20ltrs kwa tzs 500 mpaka 750. Na bado siku hizi tunalipishwa tzs 200 kwa ndoo ya lita 20 huku mtaani na wenye mabomba.
 
toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,767
2,000
Upo sahihi mkuu kumbe tunalipiaga rea eeh?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
24,349
2,000
Huku segerea kwa week wanaachia maji dk 10 ,wanatia aibu ,hii ni shirika la hovyo kabisa
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,770
2,000
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.

Leo ni miaka 60 ya uhuru lakini Dawasa hadi dakika hii hawajaweza kuyafikia maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Hii ni aibu sana na jambo la kusikitisha.

Hivi wanakwama wapi miaka 60 lakini hawajaweza, jee Tanzania nzima lini itakua na access ya maji kwa kila kijiji?

Naona itachukua miaka mingine 60 ndio tufikie Tanzania nzima ikiwa na maana ya jumla ya miaka 120.

Tuna safari ndefu!
Miaka 60 ya uhuru wa nini, DAWASA?
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,323
2,000
Maji ni moja ya hitaji la msingi la binadamu. Kama binadamu anamudu voucher ya simu kila siku hawezi kushindwa kulipia maji kila siku kama yanapatikana.

Serikali itangaze zabuni, apatikane mwekezaji mwenye uzoefu awe wa ndani au wa nje mradi alipe kodi kwa serikali. Mzabuni atatangaza kazi zake na watu watapatiwa maji.
 
Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
675
1,000
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.

Leo ni miaka 60 ya uhuru lakini Dawasa hadi dakika hii hawajaweza kuyafikia maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Hii ni aibu sana na jambo la kusikitisha.

Hivi wanakwama wapi miaka 60 lakini hawajaweza, jee Tanzania nzima lini itakua na access ya maji kwa kila kijiji?

Naona itachukua miaka mingine 60 ndio tufikie Tanzania nzima ikiwa na maana ya jumla ya miaka 120.

Tuna safari ndefu!
Hivi DAWASA ni ya nchi nzima au kwa Dar peke yake? Kama ni kwa Dar tu, siyo sahihi kutegemea wafikishe huduma kila kona ya nchi.
 
Ba Martha

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
346
225
Hivi DAWASA ni ya nchi nzima au kwa Dar peke yake? Kama ni kwa Dar tu, siyo sahihi kutegemea wafikishe huduma kila kona ya nchi.
Sio sahihi kwanini? Wanaopewa madaraka wakiwa na maono kama yako hatuwezi fika popote! Lazima waone inawezekana kua na maji ya kutosheleza Dar nzima na ziada juu. Tuache kufikiria vitu vidogo vidogo na mawazo ya kushindwa.
 
toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,767
2,000
Kabisa kuliko hii monopoly ya ajabu
Maji ni moja ya hitaji la msingi la binadamu. Kama binadamu anamudu voucher ya simu kila siku hawezi kushindwa kulipia maji kila siku kama yanapatikana.

Serikali itangaze zabuni, apatikane mwekezaji mwenye uzoefu awe wa ndani au wa nje mradi alipe kodi kwa serikali. Mzabuni atatangaza kazi zake na watu watapatiwa maji.
 
Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,625
2,000
Hiyo miaka 60 sijui umeitolea wapi maana hata Historia huijui na hujishughulishi kuifahamu...

Kwa ufupi tu anza na hii..

Jiji la Dar es Salaam kwa nyakati tofauti limekuwa na usimamizi wa aina mbalimbali;Mwaka 1980 Jiji la Dar es Salaam lilikuwa linapata huduma za maji kwa kusimamiwa na Dar es Salaam Water Supply Cooperation Sole.Shirika lilikabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile, ukosefu wa vifaa; nyenzo za kufanyia kazi; fedha; na uchakavu wa mitambo na mabomba.Mwaka 1981 Serikali ikaunda Mamlaka ya Taifa ya Maji Mijini (National Urban Water Authority-NUWA) kwa lengo la kutoa huduma nchi nzima.Huduma ilikabiliwana changamoto mbalimbali, na hivyo ikashindwa kutoa huduma ilivyokusudiwa chombo hicho kilitoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Jiji tu. Wahandisi wa Maji wa Mikoa wakaendelea kutoa huduma kwenye Miji Mikuu ya Mikoa na Wilaya.

Mwaka 1997 Sheria ya NUWA ilifanyiwa marekebisho, na huduma ya maji kwa Jiji la Dar es Salaam ikawekwa chini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).

Chini ya Sheria ya DAWASA ya mwaka 2001, DAWASA ilipewa jukumu la kuhudumia Jiji la Dar es Salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo na eneo la kilomita mbili kila upande wa bomba kuu kutoka Ruvu Juu na Ruvu Chini. Katika kuboresha huduma ya maji Jijini Dar es Salaam, Serikali iliridhia DAWASA kuingia mkabata wa miaka 10 na kampuni ya City Water Services ili kuendesha huduma za majisafi na majitaka Jijini. DAWASA iliendelea kuwa mmiliki wa miundombinu. Mkataba huo ulisitishwa mwaka 2005 baada ya Kampuni ya City Water Services kushindwa kutoa huduma kwa viwango vilivyotarajiwa. Serikali ikaunda Shirika la Maji la Dar es Salaam (DAWASCO) chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992, ambapo lilianza kazi rasmi Juni, 2005 hadi leo.

#5Tena
 
Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
675
1,000
Sio sahihi kwanini? Wanaopewa madaraka wakiwa na maono kama yako hatuwezi fika popote! Lazima waone inawezekana kua na maji ya kutosheleza Dar nzima na ziada juu. Tuache kufikiria vitu vidogo vidogo na mawazo ya kushindwa.
Kama kampuni iliundwa kwa minajiri ya Dar, itakuwaje waende kutoa huduma Mwanza, au Tanga, n.k? Ni sawasawa na kuuliza kwa nini UDA hawatoi huduma Dodoma au Arusha. Jibu kwanza swali nililouliza: Jee DAWASA ni kwa Dar au kwa nchi nzima? Jibu la swali hilo linafuta dodoso zingine zote.
 
Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,676
2,000
Kama week au zaidi, huku maeneo ya Bunju tunapata maji ya chumvi kabisa kutoka DAWASA, kulikoni?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom