Summarize kwa kusema "Wabunge rudini majimboni hakuna faida ya mnachoafanya hapo bungeni kwa sasa".Bajeti ni kwa kilometre 17,then hafla inabadilshwa angani inakuwa ya 70 kms.Nafuatilia mikutano ya Rais Magufuli Mbeya
Kitu nilicho observe ni kuwa Rais akifika mahali njiani akiona kuna wananchi wengi wanamsubiri, basi yeye hufurahi sana na kuwagawia hela mara kadhaa milioni 5 ndio naona anagawa mara nyingi
Kuna sehemu nyingine kapita tena kaona kina wananchi wanamsubiri kwenye mvua akawaahidi barabara sababu wamemfurahisha sana
Sasa ninachojiuliza ina maana Rais hana plan au bajeti ambazo zipo pre determined kutokana na umuhimu wake na kuzipa hela bali yeye anagawa tu hela kutokana na mzuka ambao wananchi watampandisha?
Tukiachana na hizo za milioni 5 nyingi, kuna milioni 400 kaahidi za zahati, kuna barabara ya nabilioni kaahidi tena baada ya kuona wananchi wamemsubiri kwenye mvua
Nashangaa hivi hakuna mipango ya kujenga barabara fulani kutoka na umuhimu wa hizo barabara bali Rais anagawa tu miradi ya barabara baafa ya wananchi kumfurahisha?
Magufuli ana uthubutu lakini anaivunja mihimili mingine na hii haina siha kwa Taifa.Akiondoka tunarudi kule kule.