KERO Inakera sinki za kukojolea za vyoo vya wanaume kukaribiana sana bila vitenganishi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
42,500
56,995
Vyoo vya matumizi ya umma hasa kwa ajili ya kukojoa katika bar nyingi na migahawa ya bus za abiria Tanzania vina changamoto nyingi sana upande wa sinki za kukojolea.

Kuna mahali bar kubwa au mgahawa mkubwa sana na wateja wengi lakini kuna sinki mbili tu za kukojolea kwa hiyo wateja chooni mnapanga mstari kusubiriana, kuna mahali sinki ziko karibu sana yani hata ukijikung'uta baada ya kumaliza kukojoa unamrushia mwenzako mkojo, kuna vyoo unaingia nafasi ndogo sana huko ndani ya vyoo inabidi kutembea kiubavu kupishana lakini pia unakojoa wengine wanakusubiria mgongoni umalize!

Mazingira kama haya ni kudhalilishana na kuambukizana UTI tu. Wamiliki wa bar na migahawa hasa ya bus zingatieni maslahi ya afya za wateja wenu na boreshini mazingira ya vyoo. Pia idara ya afya ya jamii ya serikali timizeni wajibu wenu wa usimamizi na udhibiti.

20240914_083625.jpg
 
Back
Top Bottom