Upo umuhimu wakuwepo sheria maalumu ya maadili ya umma, mfano mtu akidanganya anaweza shitakiwa kwa kosa lipi? watumishi wa umma wamekuwa waongo wanamdanganya hadi waziri mkuu. Nenda kwenye ofisi za umma watu waongo unaambiwa tuko kwenye mchakato kumbe uongo mtupu. wanasiasa waongo wanajinadi nitaleta maji nitawagawieni bodaboda uongo mtupu. Maafisa mikopo wanakwambia fungua account upate mkopo wakati wanajua hauna vigezo uongo tu. Tuweke sheria za kuwashughulikia waongo.
Lipo tatizo la machukizo ya jamii kama udada poa ukaka poa ukahaba na kufanya ngono hadharani. Kuongea matusi hadharani liwe kosa la jinai, ona mateja pale stand ya ubungo yanaporomosha matusi hovyo mgambo wa jiji wapo wanatizama tu. Nchi za kiarabu kama oman haya makosa yanasheria zake na unaadhibiwa bila huruma. Kule Katavi kabinti kadogo kamezalishwa hadi RC kaamuru hilo njema lisakwe, ni mabinti wangapi wamechochewa mimba kwa style ile? Kila mwanaume awajibike kwa kila mimba anayotundika.
Lipo tatizo la mavazi, tunasema hili ni vazi la heshima na hili sio vazi la heshima je niwakati gani vazi la heshima linatakiwa, zipo ofisi utakuta mabango kuwa panatakiwa nguo za heshima lakini hata ukiingia na kaptula hakuna anayekuuliza. Yapo makanisa siku hizi wanaweka walinzi kuzuia waumini waliovaa hovyo, ijulikane ni kosa la jinai kuvaa nguo za aibu.
Natizama miziki ya kisomali wadada wazuri wamevaa nguo ndefu na wanaimba muziki kwa heshima yake hata kama yuko kwenye tamasha ufaransa bado atavaa vazi la kisomali jukwaani, hivyohivyo kwa miziki ya Rwanda, sasa sisi hizi ndombolo ya solo zimetokea wapi? mbaya zaidi hata TBC1 machukizo haya yanaonyeswa tena bila kututahatharisha watizamaji tukaondoa watoto wetu wasijeona uchafu ule.
Tembelea familia zenye watoto wadogo TV zinaonyesha katuni tu, kisa ndombolo ya solo, nani kawaambieni video yako bila madada poa haiuzi? Tunahitaji sheria itakayolinda maadili yetu.