Inahitaji zaidi ya mapenzi kufunga ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inahitaji zaidi ya mapenzi kufunga ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by eRRy, Nov 9, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mapenzi ni mamlaka huru ya hisia, mtu kwa ridhaa yake kudondosha moyo kwa yule aliyemhusudu. Ni vema kugundua mapema kwamba uliyenaye si wa maisha yako kuliko kuanza safari itakayokutia jakamoyo siku za usoni.

  Tafsiri ya mapenzi ni moyo huru kila siku kwa ajili ya kupenda. Wengi wanakosea kwa sababu wana tabia ya kujenga mazoea badala ya kupenda na kupendwa. Ndoa nyingi wanandoa wanaishi si kwa sababu wanapendana, bali wamezoeana.

  Hii ndiyo sababu ya wengi kusaliti, tamu ya ndoa anaipeleka nje. Huko anakopeleka anasema ndiyo anapenda, eti mwenzi wake wa ndoa yupo naye kwa mazoea tu, si mapenzi. Kama mshauri wa saikolojia na uhusiano, nimekutana na kesi nyingi kama hizi.

  Usikubali kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya mazoea, kwani utateseka maisha. Upe maswali moyo wako mara mbilimbili na ukujibu, kisha tathmini penzi la mwenzako kwako, ukiona linatosha basi heri kuanza safari ya ndoa, lakini kama una shaka ni bora kuangalia ustaarabu mwingine.

  Unadhani ndoa inahitaji mapenzi peke yake? La hasha! Yapo mambo ya msingi zaidi ya kupendana ambayo kama yatajionesha kati yenu basi ni ruhusa kuingia kwenye safari ya maisha ya pamoja. Ikiwa viashiria hivyo havipo, ni bora ukaacha kuthubutu.

  Umejiridhisha kuwa mnapendana lakini vipi kuhusu maelewano yenu, vipi hisia zenu mnapokuwa pamoja. Mnafanana katika mambo yapi? Mnasaidiana? Kama hamuendani, hata kama mnajitangaza mnapendana huo ni utani. Mapenzi hayapo hivyo!
  Dunia ya leo, safari ya maisha ya ndoa inaanzia kwenye urafiki. Vipi mnavyoelewana? Kutofautiana ni kawaida lakini ndiyo kila siku? Epuka uhusiano ambao utakulazimu kutatua migogoro kila inapofika mawio ili uweze kulala usingizi mnono.

  Unachowaza, kwake hakipo. Haumii kwa kutowasiliana na wewe, unapomuonesha kwamba unaumia, yeye badala ya kujiona ana wajibu wa kukupa faraja, anacheka na kuwaambia marafiki zake kwamba amekuteka na hujiwezi kwa sababu presha inakupanda na kushuka kwa ajili yake.

  Hapa chini kuna maeneo ambayo ukiyazingatia ni muongozo sahihi katika kumteua mwenzi wa maisha yako.

  HISIA​

  Mapenzi ni mguso wa hisia, kwa maana hiyo kigezo kikuu cha kuzingatia kwa mtu anayestahili kuwa mwenzi wako wa ndoa ni vile ambavyo hisia zake umeziteka. Hali kadhalika na wewe mwenyewe ulivyotekwa naye.

  Amani ikitawala kati yenu unajiona upo huru kwa kila kitu na mnapokuwa hamuelewani kila kitu kwenye ubongo wako unaona hakiendi. Vivyo hivyo na yeye kwamba amani ipo pale mnaelewana na inatoweka mnapokosana. Huyo ni wazi mnaendana.
  MAWASILIANO

  Anapenda kuwasiliana na wewe, ukimtumia SMS anaijibu ‘fasta’. Hatengenezi sababu ya kutowasiliana na wewe, daima anaona njia pekee ya kuwaweka karibu hata kama mpo mbali ni kuwasiliana. Nawe unampigia simu kwa wakati, unasikia raha kupokea ujumbe wake naye anaona fahari kupigiwa simu na wewe.

  Kama hali hiyo ipo, basi upendo wa kweli upo na hiyo inatosha kuthibitisha kwamba mnaendana. Ukituma SMS naye akachelewa kujibu ni wazi haoni umuhimu wako.

  Katika mapenzi, mpenzi nafasi yake ni VIP, anastahili thamani ya juu kabisa.

  KUTOSHEKA
  Ukiwa naye unajisikiaje? Umetosheka eeh? Akiwa mbali inakuaje, unahisi kuna upungufu mkubwa? Vipi na yeye anajiona hivyo hivyo? Kama jibu ni ndiyo maana yake mnaendana kwa sababu ukamili wako unamtegemea yeye, hali kadhalika na yeye.
  Anakata kiu yako yote? Na upande wake inakuaje? Unamkuna vilivyo? Ikiwa ni hivyo, basi anatosha kuwa mwenzi wako wa maisha. Katika kutosheka ni hata kwenye mapenzi. Mnapokutana faragha anakusafirisha kule unapotaka, pia naye anaridhika na wewe.

  Spidi ya nyonga au vilio vingi na kusifiana kitandani ni chachandu tu lakini si kila kitu kwenye eneo la mapenzi. Pointi kuu ni vile moyo wako anavyoukonga. Unahisi kuna raha ambayo huwezi kuipata kwa mwingine, naye anakupigia saluti kwamba wewe ni namba wani wake. Hapo sawa.

  MATARAJIO
  Kila mtu anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo lake huwa ni kudumu. Achana na hulka za viruka njia. Pointi hii inakujenga kujua matarajio ya mwenzako kuhusu wewe. Anakuhitaji kwa maisha yake yote au yupo na wewe kwa sababu hana pa kwenda?

  Wengi wapo kwenye majuto kwa sababu waliingia kwenye ndoa na watu ambao hawakuwa na nia ya dhati nao, bali walijichanganya baada ya kukosa uelekeo. Siku alipotokea anayehisi kumpenda, akaanza vitimbi ndani ya nyumba. Usiingie kwenye mkumbo huo.

  Familia nyingi zinasambaratika, wengine wanadaiana talaka mahakamani. Ni aibu! Je, mna matarajio ya kuishi pamoja? Unampenda kweli au unabembeleza ndoa? Moyo unakutuma kuwa naye au unao huruma kumuacha? Huruma yako leo, kesho itamgharimu kwa sababu utakuwa umemkinai, hivyo kushindwa kumpa upendo wa dhati.

  MNAUMIA NA KUFURAHI PAMOJA​

  Hapa ni hisia tu, ikiwa mnapendana kwa dhati basi akiumia nawe yatakuwa ni maumivu yako. Ikiwa hauna raha halafu yeye ni mwenye furaha basi huyo anakupenda kinafiki. Hatofautiani na yule anayebembeleza ndoa ili kuondoa mkosi. Kuwa makini.
  Tatizo lako analivaa vipi? Mtu wa kweli ni yule anayetambua hali yako na kushirikiana na wewe. Hangoji umkumbushe, anaposikia tu umefikwa na lolote anavaa uhusika mara moja, pia kwenye sherehe mpo wote na nyoyo zenu zinakuwa na bashasha katika kusherehekea pamoja.

  ANAJUTIA KOSA NA KUOMBA MSAMAHA​

  Mpenzi bora ni yule anayejutia kosa pale anapokukosea, pia anaomba msamaha. Hapa ieleweke kuwa kuomba msamaha peke yake haitoshi, isipokuwa anapaswa kuonesha wazi kwamba ametambua makosa yake na amejuta.
  Kimsingi mtu mwenye sifa hiyo huwa hasumbui mnapokuwa ndani. Epuka mtu mbishi, anakosea na hatambui kosa leke na badala yake anajenga hoja. Kwa maana hiyo unapaswa kuwa makini na kugundua mwenzako yupo kwenye kundi lipi kati ya hayo kabla hujafanya uamuzi.

  HAYUPO RADHI KUKUPOTEZA
  Mnagombana anaumia lakini bado yupo na wewe. Anakuonesha waziwazi kuwa hayupo tayari kuachana nawe. Yupo radhi kutumia muda mwingi kutafuta suluhu ili muendelee kuwa pamoja. Hiyo inaonesha kuwa anakupenda kwa moyo mmoja.
  Mtu mwenye moyo mgumu, mnagombana wala hashtuki na hatengenezi mazingira ya kurudiana, maana yake hana hisia za kweli, na anavyokuchukulia ni kwamba hata mkiachana yeye anaona sawa. Ni vema kumshtukia mtu huyu mapema kabla hajakutia donda kubwa la moyoni baadaye.

  VIPI KUHUSU WEWE?
  Umeangalia yote hayo, sasa jiangalie na wewe mwenyewe. Moyo wako unakusukuma kuwa na yeye?


  [​IMG]
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nimeipenda!
  naomba link yake basi:D
   
 3. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mada imetulia kweli,nimeipenda sana.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  asante sana erry84 kwa mada nzuri
   
 6. k

  kisoti Member

  #6
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imetulia sana. Unaonaje ukaendesha semina kwa vijana kuhusu suala hili la mahusiano,maana kwa mtazamo wangu suala hili linawakanganya wengi
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Ndoa ni kuchagua mwenza ambaye huwezi kuishi bila yeye na sio kuchagua unaye weza ishi naye. Choosin' a partner that you cant live without and not otherwise na mengineyo
   
 8. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tatizo wengi wanaamua kuoa ilimradi anamfahamu mwenzi wake huyo!
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu,swala la mahusiano linasumbua wengi sana,tukiwa mara kwa mara tunapata mada kama hizi zilizotulia nadhani tutajifunza mengi sana,hii mada imeeleza mambo ambayo ni ya kweli kabisa.
   
 10. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yeah ni kweli!
   
 11. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umeorodhesha yoote! sidhani kama unaweza kuwa perfect au kumridhisha mwenzio. Ni kuomba Mungu tu aingilie kati mahusiano ya watu. Kuna Proffesors wengi wameainisha, wengine wanafanyiwa kitchen party on the same day, mmoja kati ya wanandoa anaenda kufata wale aliowaacha uraiani.

  Mapenzi ni kitendawili!
   
 12. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  That is just literature my friend!
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Inawezekana lakini kama mkiamua.nothing is imposible under the sun(labda kurudisha uhai)
   
Loading...