Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 52
- 138
...Maisha ya Makocha wa Football kwenye Timu huwa hayategemei mafanikio uliyowapa huko nyuma bali mwenendo wa timu kwa wakati huo.
Maisha ya Makocha wa Klabu za Simba na Yanga huwa hayategemei rekodi uliyoiweka kwenye klabu bali kelele za Mashabiki na maamuzi ya viongozi kwa wakati huo.
Na hii ni kwasababu viongozi wa timu wanajua huwa wanashindaje hizo mechi...
Ndio maana Simba waliachana na Didier Gomes Da Rosa na Patrick Aussems walioweka alama kubwa kwenye mafanikio ya Simba Kimataifa hivi karibuni.
Ndivyo ilivyo hata kwa Master Miguel Gamondi wa Yanga
Licha ya vikao kuisha na Gamondi kupewa mechi 3 bado Viongozi wa Yanga wanatafuta mbadala wa Gamondi.
Taarifa zinaeleza mmoja wa viongozi wa Yanga hivi karibuni amesafiri nje ya Nchi kumfuatilia mbadala wa Gamondi.
Hata Gamondi mwenyewe anafahamu...
Najiuliza,
Gamondi amewapa mataji mengi Yanga kwa muda aliokaa
Gamondi yuko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi akiwa nyuma kwa alama moja tu.
Gamondi ameipeleka timu hatua ya Makundi CAFCL
Kama huyu hafai...Yanga inapaswa kuwa na Kocha wa namna gani? Maana hata Pep anafungwa!
Hii inafikirisha sana...
✍️Sospeter Ilagila