Inafikirisha sana kuona viatu vinakupwaya lakini unajipa matumaini ya kuendelea na safari ya uongozi kwa Watanzania

Kwa hiyo,kwa kauli Yake kuwa Viatu vya Magufuli Ni vikubwa anamaanisha Magufuli alikuwa na uwezo Mdogo kulinganisha na yeye mama?
Hivi wewe unaweza kuvaa viatu vya mama yako au vya mke wako?embu jiongeze basi uelewe.Aliyepita ni alieyepita na huyu ni huyu ni watu wawili tofauti
 
Kila mtu hata yule anayetembea peku anaweza kuwa RAIS. Na ikitokea si lazima tulazimishe avae viatu!
Tunachohitaji ni Katiba nzuri, uongozi bora, weledi, matashi mema na wananchi waliochangamka kudai haki zao.
 
Ili nisionekane nahangaika ulitaka nifanye niandike kitu gani? Hivi uliisikiliza hotuba ya huyo mgombea pekee mtarajiwa? Yeye anakiri hana uwezo wa kumfikia Marehemu Maguguli halafu wewe unasema Ni kauli tu ya kisiasa? Kwa hiyo, ili tuweze kumuelewa mama tuwe tunakuuliza wewe kwa kauli hii au ile alimaanisha nini?
Mkuu tazama ulichokiandika kwanza... Jambo la msingi ni kudai katiba mpya haya mengine ni sawa na kujilisha upepo tu. Kama hakuna katiba ya maana hapawezi kuwa na tume huru za uchaguzi.
 
14. CCM, mgombea wenu huyu ikiwa atakuwa wa pekee, mumefanya utafiti mtaani ni kweli anachagulika? Ni mgombea ambaye akishindanishwa na vyama vingine makini mnaweza kusema kwa dhati kuwa kweli atatoboa kabla hata Jogoo hajawika?Ni kwa nini hamumuelezi ukweli kuwa hachaguliki? mkuu wewe kwa uelewa wako ni chama gani kingine makini kwa sasa ambacho kinaweza kupambana na ccm ikiwa wao wenyewe watampigia kura kwa sababu wao ndio walitwambia anaupiga mwingi dhalimu ameondoka.
 
Vyama makini mimi naamini vipo ila vinahujumiwa ili kuonekana sio makini. Vyama pinzani ni wale wananchi wasioafikiana na mambo ya Chama Tawala.
 
Vyama makini mimi naamini vipo ila vinahujumiwa ili kuonekana sio makini. Vyama pinzani ni wale wananchi wasioafikiana na mambo ya Chama Tawala.
Njia pekee ya kuiondosha CCM ni madarakani ni vyama vya upinzani kuunganisha nguvu,na kuja na agenda mujarabu jinsi ya kutatua changamoto za watanzania kuliko hivi Sasa wanavyo dandia hoja nyepesi nyepesi zisizokua na mashiko kwa wananchi.Pia wachague ile mikoa ambayo ni ngome za CCM(mwanza,tanga,shinyanga,katavi na rukwa,Tabora,n.k wapeleke agenda zenye nguvu zinazoeleweka na wamachinga,boda boda,mama lishe,wakulima,wafanyabiashara,wasomi na wapiga kura wote kwa ujumla.
 
Mleta mada umeandika mengi lakini kwa ufupi ni wale wale wanaomia mioyoni kumuona Mama akiongoza nchi.​

JPM keshaondoka juu ya ardhi, hawezi tena kusimama na kuja kutuongoza kama wengi wetu tunavyopenda iwe hivyo.​

Cha muhimu ni kuondoka jana na kuhamia leo kwa ajili ya kuitengeneza kesho yenye mwanga na maendeleo.​

Zinduka mleta mada, amka na simama kisha nawa uso usingizi uweze kukutoka.​

Back
Top Bottom