Inaelekea hivi sasa kuna utata katika utendaji kazi serikalini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inaelekea hivi sasa kuna utata katika utendaji kazi serikalini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Dec 28, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mshauri; na kama mshauri yeyote yule, serikali ina uhuru wa kukubali ushauri wake au kuukataa. Katika hali hiyo, kitendo cha mh. Werema kutangaza hadharani ushauri wake kwa waziri wa nishati na madini kuhusu malipo ya Dowans, na kuuelezea kuwa huo ndiyo uamuzi wa serikali, kabla hata mhusika hajahufanyia kazi(kwani ikumbukwe waziri mhusika alikuwa ametangaza kuwa angeli tangaza uamuzi wa serikali juu ya suala hili wiki ijayo), siyo tu kinaashiria ukosefu wa nidhamu bali pia ni dalili kuwa sasa hivi kuna mkanganyiko katika utendaji kazi serikalini.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  :whoo::whoo::whoo::whoo:
   
 3. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Byendangwero,
  Inaelekea kuna matatizo Makubwa. Waziri Mkuu ametolea Tamko Katiba, na Mwanasheria Mkuu naye asema "ataweka viraka". Ni kama Serikali haina kauli mmoja (Collective Decision Making) na au haina Msemaji. Tusubiri tuone mparanganyiko zaidi......Lakini hatutegemei kutofautiana katika mambo mazito na makubwa kama hayo yanayogusa maslahi ya Taifa.
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  CHUKUAAAAAAAAAAAAAAAAAA CHAKOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO MAPEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!! kuna mwenye muda wa kushauriana nani aseme nini? vurugu mechi!! hiyo ni serikali au kikundi cha watu kinatufyonza damu!
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi MUNGU akupe maisha marefu Dr W Slaa.

  Zaidi Busara,Maarifa na Hekima akuzidishiwe.

  Hii nchi kwa kweli ilipofikia inasikitisha.
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usemacho ni sahihi kabisa. Lkn yote hutokana na weakness ya JK. Watendaji wake wanamjua kuwa he is very weak. Ndiyo maana hujiropokea watakavyo. Makamba sasa ndiye Mwenyekiti wa ccm. Asemalo ndiyo uamuzi wa mwenyekiti. Aliwakataza kuhudhuria midahalo ikawa hivyo. KUNA OMBWE KUBWA SANA LA UONGOZI CHINI YA JK!!!
   
 7. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Kwa hli ilivyo sasa, kila mtu amekuwa msemaji wa serikali. Na hii ni kwa sababu mkuu wa nchi mwenyewe amekuwa bubu kuhusu masuala ya msingi kabisa yanayogusa maslahi ya taifa. Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa kuna ombwe la ki-uongozi. Nchi imekuwa kama vile haina dereva. Kwa kweli tutaona na kusikia mengi msimu huu.
   
 8. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Nchi hii inatia uchungu! haina muelekeo wanaoitwa viongozi wamekosa sifa zinazostaili! hawana huruma na nchi! inatia uchungu sana. I am fed up!
   
 9. P

  Penguine JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180

  Brother Thank u very much kwa huu mtazamo wako.

  Pamoja na mkorogano huo (absense of consistency in the government statements) yapo mambo mengine ambayo hata kwa Watz ambao hawajaenda shule ya uchanganuzi wa mambo wameanza kuyatilia hofu. Juzi , Desemba 23, niliulizwa swali na bibi yangu kutoka kijijini kabisa kasulu. ananiuliza mbona eti haoni chochote kinachoendelea serikalini kwa sasa. Nikamuuliza angependa kuona kitu gani hasa? akanijibu haoni gari za mawaziri waliotangazwa wakizunguzunguka huku na huko kufuatilia utekelezwaji wa miradi.

  Jamani hati wabibi vijijini wametambua dullness hii. Amka Mr. Serikali, usingizi gani huo?

   
 10. l

  limited JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  yaani hiyo kwa serekali ya awamu ya nne ni kitu cha kawaidaaaaaa kila mtu anasema anachojua na anachotaka ni kama baa za komoni
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hilo nashukuru mkuu, kwani wengine tumekwishaanza kuwa na wasi wasi, hasa tunapoona baadhi ya wenzetu wanajichukulia jukumu la kuandaa rasimu za katiba bili ya kwanza kukubaliana ni utaratibu upi ufuatwe ili kushirikisha makundi mbali mbali ya jamii katika mchakato huo.
   
 12. D

  DENYO JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  byendangwero-tumefika pabaya sasa ndio ule usemi usemao chenye mwanzo kina mwisho -sasa wanaumana kila mwnye sauti anajitokeza kivyake kila mwenye ubavu anajituma kivyake kuna mambo mawili ambayo werema kayaongelea kirahisirahis bila au huku akijua yanagusa maisha ya watanzania -ndio maana mtoto wa mkulima alijibu kwa umakini saana pamoja na kuwa tunashaka na political will yake

  1. malipo ya dowans -sitta, mwanasheria mkuu before werema na mwakyembe wote ni wanasheria -wasingeweza kuvunja mkataba kijinga mpaka iwe hivi kuna kamchezo-au ndio kurudisha gharama za kulipia mabango yaliyotandazwa nchi nzima? manake 2005 epa ilitumika sasa tuna hofu hii isiwe janja -lakini pia sitta na mwkyembe na mwanasheria wa zamani wanayo mengi walificha sasa werema kuropoka hadharani akimponda sitta anataka sitta na mwakyembe wamjibu???? dowans kwani ya nani???? hukumu ina jina la roastam -lakini roastam amekana mara nyingi umiliki sasa analipwa nani??? mwansheria wa costa rica ameikana dowans -sasa werema anasema nini huyu??????????

  2. katiba mpya -sisi watanzania tunataka katiba mpya yeye anataka viraka il;i iendelee kumlinda anataka nguvu ya umma????? hwa ndio watu waliowekwa madarakani kulinda kwa vyovyote vile sirikali za wakubwa na jinsi wanavyoinyonya nchi -werema chukua chaklo mapema ila kitarudi piga ua -umma umebadilika saana slaa amefanya kazi.

  kwa kumalizia serikali hii sijui ngoja tusubiri mziki ------

  angalau nina kiongozi wangu slaa wasimguse ila atawalipua katika haya yote mawili
   
 13. Bless the 12

  Bless the 12 Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  -----------
  JK ni very very weak leader sijapata kuona yani mpk ni aibu ya nchi, haiwezekani viongozi wako waongee lugha zinazotofautiana katika mambo nyeti na ya msingi kama katiba na yeye hata haongei chochote nao na hata labda ukute anawaogopa pia.

  Ni aibu sana, ukifatilia kauli za pinda, kombani na werema utagundua serikali haina rais.
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Evidence nyingine ni jinsi magufuli alivyovamia mambo ya TRA pale Namanga.yaani ni mparanganyiko the goverment is not a single unit/system as it used to be.
   
 15. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Denyo unachosema ni kweli lakini ukumbuke Sita na Dr.Mwakyembe hivi sasa wako serikalini hivyo wanabanwa na dhana ya collective responsibility,hivyo hawawezi kuzungumzia suala hili serikali ikishatangaza uamuzi wake. Pili, kadri mambo yanavyozidi kuwekwa bayana, inaonekana kuna uwezakano wa kuwepo njama; maana haingii akilini ilikuwaje TANESCO wakazuia mitambo ya Dowans kama walikuwa hawadaiani.
   
 16. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dr., pamoja kwamba sina wasi wasi na dhamila yako katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa nchi yetu, lakini kwa suala hili la katiba wewe mwenyewe pamoja na chama chako mtapashwa mjifunge kibwebwe; ukiona mwanasheria mkuu, anaungana na waziri mwenye dhamana ya sheria na katiba kutamka wazi kuwa hakuna uwezekano wa kufanyika kwa katiba mpya, ujue kuna mahali waliposimama. Mh. Pinde anaweza akawa waziri mkuu lakini hasiwe kwenye "inner cabinet," ambamo masuala nyeti yana amuriwa.
   
 17. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  MI nina wasi wasi maana kama kamati ya bunge ya ukaguzi wa hesabu za serikali haitakua makini mpaka 2015 tutakua tumefika pabaya maana waliopo wote serikalini now ni WACHAKACHUAJI WA RASILIMALI ZA WATANZANIA wakijua kwamba baada ya hii awamu ya JK awamu ijayo watakua na Rais mwingine so inawezekana akaja na watu wake na wao wasipate tena uongozi.
  WAPINZANI TUNAOMBA MUWE MAKINI MAANA HAWA JAMAA WATATUFILISI.
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu Salaam,
  PM ametolea Tamko katiba ambayo si katika mambo yakutekelezwa katika ilani ya ccm..in fact anadanganya tu kwakuwa aliulizwa na mwandishi akasema atamshauri ..si unajua mtoto wa mkulima kwa maneno ya kistaarabu..mpole sana huyu ndugu yetu

  AG statement basically ni operational statement siyo political unlike PM

  Mpaka sasa CCM hawana makosa yoyote kwa wananchi kwasababu hawakuchaguliwa ili kuleta katiba mpya? hayo ni CUF na CDM au siyo?
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio mnara wa babeli ulivyoanza kuporomoka


  pwani tunasema... angenda juu kipungu, hafikilii mbinguni... sasa hivi tutaanza kusikia JK hana kauli ya mwisho tena, na ameamua kunyamaza haswaa...
   
Loading...