Tetesi: Inadaiwa Watumishi waliopambana dhidi ya UVIKO 19 hawajalipwa

NIFEDIPINE

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
206
250
Pamoja na Serikali kutoa TSH bilioni 3 kwa ajili ya kuwalipa watumishi waliopambana dhidi ya UVIKO 19 na kuahidiwa mwezi wa Tisa mwaka huu kuwa ndani ya wiki mbili watapata pesa zao Bado hakuna mtumishi yeyote aliyepata fedha hizo au kuwekewa kwenye akaunti yake kama NAIBU WAZIRI MOLLEL alivyosema.

Naona Bado Serikali imeamua kuendelea na SIASA hasa kwa kudanganya watumishi hawa maana inakaribia mwezi Sasa na si wiki mbili tena kama alivyosema waziri.

Huenda Waziri alikuwa na nia njema kabisa lakini watu walio chini yake waliopewa dhamana ya utekelezaji wanamuangusha kwa MAKUSUDI.

USHAURI.
Watumishi hawa walipwe stahiki zao kama serikali mlivyoahidi maana hatujui ya kesho.

Watumishi wengi wa Afya walikataa kuhudumia wahanga wa UVIKO 19. Sasa wale waliojitoa wapewe chao.

Ninyi mliopewa Dhamana ya kuhakikisha watumishi hawa wanapata stahiki zao fanyeni kazi yenu. Msikwamishe bila sababu ya msingi Kisa hiyo pesa hamuoni namna ya KUIPIGA
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,936
2,000
Wengine wapo wanaisaidia serikali "kubumba" takwimu za waliochanja j&j ionekane ni 100% na hakuna nanayewajali...wakubwa wanajilipa posho za usimamizi,nk.

Kuwa mtumishi wa afya Tanzania ni kujitafutia magonjwa ya Sonoma bure!

Watalipwa mbinguni tu, Mungu anayaona mateso yao.
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,336
2,000
Kumbe wataalamu wa afya walikimbilia kumushauri Rais alete chanjo,walijua watanufaika?
Hata mkizichukua zitawatokea puani,laana ya wanaolioathirika na chanjo haitawaacha salama.
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,326
2,000
Pamoja na Serikali kutoa TSH bilioni 3 kwa ajili ya kuwalipa watumishi waliopambana dhidi ya UVIKO 19 na kuahidiwa mwezi wa Tisa mwaka huu kuwa ndani ya wiki mbili watapata pesa zao Bado hakuna mtumishi yeyote aliyepata fedha hizo au kuwekewa kwenye akaunti yake kama NAIBU WAZIRI MOLLEL alivyosema.

Naona Bado Serikali imeamua kuendelea na SIASA hasa kwa kudanganya watumishi hawa maana inakaribia mwezi Sasa na si wiki mbili tena kama alivyosema waziri.

Huenda Waziri alikuwa na nia njema kabisa lakini watu walio chini yake waliopewa dhamana ya utekelezaji wanamuangusha kwa MAKUSUDI.

USHAURI.
Watumishi hawa walipwe stahiki zao kama serikali mlivyoahidi maana hatujui ya kesho.

Watumishi wengi wa Afya walikataa kuhudumia wahanga wa UVIKO 19. Sasa wale waliojitoa wapewe chao.

Ninyi mliopewa Dhamana ya kuhakikisha watumishi hawa wanapata stahiki zao fanyeni kazi yenu. Msikwamishe bila sababu ya msingi Kisa hiyo pesa hamuoni namna ya KUIPIGA
Hao watumishi walipambana kivipi dhidi ya UVIKO -19? Kama ni kuhudumia wagonjwa wa covid 19, hakuna malipo ya ziada kwani ugonjwa huo ni sawa na magonjwa mengine kama malaria, ukimwi, kifua kikuu, kichaa, saratani na kadhalika. Halafu wagonjwa hao na wengine huhudumiwa na watumishi wa kila kada kuanzia wahudumu, wafagizi na madreva kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Kwa hiyo hakuna posho ya kupambana na uviko-19 au gonjwa lingine lo lote kwa watumishi wa afya. Hapo kale kulikuwa na risk allowance (posho ya mazingira hatarishi) kwa watumishi wa afya lakini iliondolewa na awamu ya tatu ya rais Mkapa. Sasa ni posho gani unayoongelea? Ni overtime allowance au on call allowance? Hakuna kitu kinachoitwa corona allowance au TB allowance etc
 
Hii ni kanuni ya Tanzania pekee eti, mbona majirani zetu ambao walikopa IMF mapema walilipwa? risk ya kuhudumia mgonjwa wa uviko ni sawa na ile ya kuhudumia mgonjwa wa TB?
Watumishi wa afya na mawazo ya kimaskini na unafiki! Wenzenu TRA wanahamisha ofisi kutoka Dar kwenda Mbeya kwa mwezi mzima ili wajilipe per diem za kuwa nje ya kituo cha kazi kuanzia dereva, mfagizi hadi bosi, nyie mnaishia kumeza PEP, pumbavu zenu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom