Inabidi sasa tubadilishe title ya Tendwa, badala ya kuitwa mlezi wa vyama, aitwe mlezi wa CCM!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inabidi sasa tubadilishe title ya Tendwa, badala ya kuitwa mlezi wa vyama, aitwe mlezi wa CCM!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mystery, Sep 9, 2012.

 1. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,947
  Likes Received: 6,705
  Trophy Points: 280
  Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, msajili wa vyama John Tendwa akitoa vitisho, eti kuanzia sasa hatasita kukifutia usajili chama chochote, ambacho kwenye mikutano yake kunatokea vifo, ingawa hakukitaja chama anachonuia kukifuta, lakini ni dhahiri kutokana na matukio ya hivi karibuni, mikutano ya Chadema ndiyo imesababisha vifo.

  Sasa hapa ndipo ninapomshangaa Tendwa, yeye anatambulika kama mlezi wa vyama, na kila mtu hivi sasa anafahamu, vurugu zote zinazotokea kwenye mikutano ya Chadema, hazitokani na fujo ya viongozi na wanachama wa Chadema, bali inatokana na polisi kuzuia shughuli halali za chama hicho chenye usajili wa kudumu na kinachoendesha shughuli zake kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Sasa kwa nini hatoi karipio kali kwa polisi kuzuia shughuli halali za Chadema, badala yake aitishe Chadema?

  Sasa hapa ndipo ninapotaka kumuuliza Tendwa iweje yeye kama mlezi wa vyama, na anaona wazi wazi namna polisi wanavyozuia kwa makusudi shughuli za Chadema, wakati shughuli kama hizo zikifanywa na CCM bila kubughuziwa na polisi,huo si upendeleo wa wazi? sasa hapa ndipo ninauliza, hivi kweli Tendwa anastahili kuendelea kuitwa mlezi wa vyama?

  mimi kwa maoni yangu kuanzia sasa atambulike kwa title ya mlezi wa chama cha magamba, badala ya kuitwa mlezi wa vyama vyote vya siasa, wadau wenzangu, mnalionaje pendekezo hilo?
   
 2. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Duh hii nmeipenda sana mkuu
   
 3. K

  KALEBE JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  nilikuwa najiuliza ya kuwa msajili wa vyama vya siasa anachaguliwa au anateuliwa na kama jibu ni kuwa anateuliwa ni nani anyemteua ni waziri mkuu, jaji mkuu, au raisi na kama ni rais je unategemea angesema nini kuhusu suala la mwangosi huko iringa ya even me i do concur with u that better we say he is the registrar for ccm and not otherwise
   
 4. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aliwahi kusema washiri wa Arumeru mashariki wamemwambia LEMA akienda huko watamua, Lema akaenda hakufa. Vijana wa Ccm waliua Igunga sikumsikia akitoa tamko. Sasa nashiwishika kuamini Tendwa ni pro Ccm. Na hata Dr. Släa aliwahi kumwambie yeye ni kada wa Ccm mpaka leo sijawahi kumsikia anakanusha. Hii title inamhusu.
   
 5. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Njaa zinawadhalisha sana wazee wetu wanao watumikia hao waliowateua!Yaani ukiwaona wanavyoongea hata utawahurumia,wameporwa uwezo wa kufikili,kuamua kukemea pamoja na elimu walyonayo kilichobaki kuelekezwa cha kuongea!
   
 6. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  binafsi sioni tofauti kati ya Tendwa Nape na Mukama
   
 7. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,618
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli hii Tendwa anaamini CDM ndio imeua mwandishi wa habari maana kwanini kauli hii imekuja punde tu baada ya kutokea mauaji ya mwandishi wa habari japokuwa ukimuuliza atajifanya yupo neutral
   
 8. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana nawewe mkuu ila niongeze kidogo kwa ruksa yako,minaomba aitwe kibaraka wa CCM,Mimi nimeshawahi kusema baada ya kumsikia akitishia kukifuta CHADEMA,nitoe mfano "unababa mlezi anawatoto anaowalea nyumbani kwake na kawatengea chumba cha kujisomea halafu akaingia mlinzi wa nyumbani akambakaau kumlawiti mmoja wa watoto tena mbele ya macho ya watoto wenzie kamfanyia hivyo mpaka kafa!!!!!Ajabu baba mlezi alipokuja asimpeleke polisi na badala yake akawaita wanae na kuwakaripia pia nakuwaonya vikalikuwa kuanzia sasa mtoto atakaye rawitiwa na kubakwa nitamfukuza hapa kwangu!!!!!!"Huyu mlezi ni bazazi si mlezi na hana sifa tena za baba mlezi.Tendwa hana tofauti na mlezi niliyemtolea mfano wa baba mlezi niliyemtaja hapo juu.Asanteni.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Mukama ni Mjanja sana. Usimjumuishe na kina nape, angalia alivyo kimyaaa, manake hakuna cha kukisemea chama chake. Kawaachia kina nape na mwigulu kubwabwaja miutumbo ya kuwapotezea utu wao mbele ya jamii.
  Tendwa ni kaliba ya kina tambwe hiza, lusinde, na mwigulu + nape.
   
Loading...