Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,225
- 113,561
Sabalkheri na msalkheri wana JF popote pale mlipo duniani.
Sasa leo nina swali. Swali ambalo nimekuwa nikilifikiria na kujiuliza kwa majuma kadhaa sasa.
Hivi kumbe kweli maisha chini ya utawala wa rais mstaafu Jakaya Kikwete yalikuwa bora eh?
Nauliza hivyo kwa sababu ukisikiliza vilio vya baadhi ya watu humu unaweza kupata picha kuwa wakati wa Kikwete maisha yalikuwa mazuri [mno] na sasa baada ya kuingia Rais Magufuli, ndani ya mwaka tu maisha yamekuwa magumu sana.
Bidhaa zimepanda bei, mabenki yanafilisika, wawekezaji wanaondoka, viwanda vinafungwa, ajira zinasitishwa, kampuni za ndege zinapunguza safari, na kadhalika na kadhalika. Kwa kifupi, hali ya uchumi ni tete.
Kauli mbiu ya rais mstaafu Kikwete wengi wetu humu tuliibeza sana kwa sababu ilikuwa haiendani kabisa na uhalisia wa maisha ya Watanzania wengi.
Ila sasa hivi vilio vya watu [kama si vya kinafiki na kipropaganda] ndo vinanifanya niwaze...kama maisha ya sasa ni magumu, ni magumu kulinganisha na ya lini?
Manake kwangu mimi maisha halisi ya Watanzania walio wengi ni magumu tu siku zote.
Kwa hiyo, kama maisha chini ya Kikwete yalikuwa mazuri au niseme yalikuwa na nafuu ukilinganisha na ya sasa chini ya Magufuli, ina maana Kikwete alifanikiwa kiuchumi?
Kama alifanikiwa kiuchumi, ina maana zile kelele na ukosoaji dhidi yake zilikuwa ni za kinafiki?