Ina maana yale yalikuwa maisha bora?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,510
Sabalkheri na msalkheri wana JF popote pale mlipo duniani.

Sasa leo nina swali. Swali ambalo nimekuwa nikilifikiria na kujiuliza kwa majuma kadhaa sasa.

Hivi kumbe kweli maisha chini ya utawala wa rais mstaafu Jakaya Kikwete yalikuwa bora eh?

Nauliza hivyo kwa sababu ukisikiliza vilio vya baadhi ya watu humu unaweza kupata picha kuwa wakati wa Kikwete maisha yalikuwa mazuri [mno] na sasa baada ya kuingia Rais Magufuli, ndani ya mwaka tu maisha yamekuwa magumu sana.

Bidhaa zimepanda bei, mabenki yanafilisika, wawekezaji wanaondoka, viwanda vinafungwa, ajira zinasitishwa, kampuni za ndege zinapunguza safari, na kadhalika na kadhalika. Kwa kifupi, hali ya uchumi ni tete.

Kauli mbiu ya rais mstaafu Kikwete wengi wetu humu tuliibeza sana kwa sababu ilikuwa haiendani kabisa na uhalisia wa maisha ya Watanzania wengi.

Ila sasa hivi vilio vya watu [kama si vya kinafiki na kipropaganda] ndo vinanifanya niwaze...kama maisha ya sasa ni magumu, ni magumu kulinganisha na ya lini?

Manake kwangu mimi maisha halisi ya Watanzania walio wengi ni magumu tu siku zote.

Kwa hiyo, kama maisha chini ya Kikwete yalikuwa mazuri au niseme yalikuwa na nafuu ukilinganisha na ya sasa chini ya Magufuli, ina maana Kikwete alifanikiwa kiuchumi?

Kama alifanikiwa kiuchumi, ina maana zile kelele na ukosoaji dhidi yake zilikuwa ni za kinafiki?
 
Kikwete alitaka kutengeneza maisha bora ingawa hakufanikiwa 100% ........

Lakini alifanya mengi mazuri ambayo mwenzie anayazika kwa sasa ...........

Kama bunge live,Kiwanda cha dangote,Wanafunzi Wa udom,na mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu.....

Ukiwa unaishi na kufatilia mambo ya Tanzania utaelewa ilo ila ukiwa unaishi nje ya Tanzania na ufatilii habari za Tanzania uwezi elewa..........
 
Kuna maisha bora na kuna maisha afadhali...

Ya kikwete yalikuwa maisha 'afadhali' kulinganisha na ya Magufuli...

Mtu kama alikuwa na uhakika wa kula mlo mmoja wakati wa Kikwete
na sasa hana huo uhakika anashinda njaa hata siku mbili kabla ya kula
huwezi kumlaumu akisema 'hali imekuwa mbaya'
au akisema 'zamani ilikuwa nafuu'

hamaanishi zamani hiyo 'alipata maisha bora'
 
Wewe ni gamba tu unaweweseka!
Kama yeye ni gamba, wewe ni nani?

Nani anayeweweseka kati yake na wewe kwa sababu bandiko lake ameliweka tu na ndani ya dakika moja umejibu pumba.

Sina shaka umesoma heading tu na kutoa jibu lenye pumba.

Tumia nguvu za hoja kama una akili timamu zenye fikra pana na sio hoja za nguvu kama mtu mwenye fikra kiduchu.
 
Kuna maisha bora na kuna maisha afadhali...

Ya kikwete yalikuwa maisha 'afadhali' kulinganisha na ya Magufuli...

Wakati wa Kikwete maisha yalikuwa 'afadhali' kwa nani? Hata kwa wale watoto walokuwa wakikaa chini madarasani na wale wamama walokuwa wakilala sakafuni kwenye zile wodi za wazazi?

Mtu kama alikuwa na uhakika wa kula mlo mmoja wakati wa Kikwete
na sasa hana huo uhakika anashinda njaa hata siku mbili kabla ya kula
huwezi kumlaumu akisema 'hali imekuwa mbaya'
au akisema 'zamani ilikuwa nafuu'

Na walokuwa hawana hata uhakika wa huo mlo mmoja wakati wa Kikwete nao wanasemaje sasa hivi?

Au wakati wa Kikwete watu wote walikuwa na uhakika walau wa mlo mmoja kwa siku?
 
JK mwenyewe kaingia mitini dhidi ya JPM sembuse wachumia nanihii...kudadeki JK alisema tutamkumbuka nadhani hii ndo time mahususi na bado mtalipia hadi oxygen unayovuta ni ya serikali..
b46.JPG
 
Kama yeye ni gamba, wewe ni nani?

Nani anayeweweseka kati yake na wewe kwa sababu bandiko lake ameliweka tu na ndani ya dakika moja umejibu pumba.

Sina shaka umesoma heading tu na kutoa jibu lenye pumba.

Tumia nguvu za hoja kama una akili timamu zenye fikra pana na sio hoja za nguvu kama mtu mwenye fikra kiduchu.
Nyekundu haiwezi kuwa kijani.

Nyinyi ni wanafiki wakubwa.

Mifano iko mingi tu.Hivi sasa hata mkopo benkj mtu hupati alafu mnakuja kuongea upuuzi hapa!
 
Tutalia sana lakini ndo hivyo tena..Maisha kipindi hiki yamekua magumu zaidi kuliko kipindi kilichopita. Hii ni kwa wapiga dili na wasiokua wapiga dili wote hali mbaya. Magufuli nadhani ana nia nzuri lakini strategy anayoitumia sio nzuri. Washauri wa karibu wa Rais hasa wachumi hawafanyi kazi zao ipasavyo.Huwezi kufungia hela BOT kwa lengo la kuzuia wapiga dili,achia hela mtaani izunguke lakini uweke control mechanism. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ukali wa maisha.
 
Wakati wa Kikwete maisha yalikuwa 'afadhali' kwa nani? Hata kwa wale watoto walokuwa wakikaa chini madarasani na wale wamama walokuwa wakilala sakafuni kwenye zile wodi za wazazi?

Na walokuwa hawana hata uhakika wa huo mlo mmoja wakati wa Kikwete nao wanasemaje sasa hivi?

Au wakati wa Kikwete watu wote walikuwa na uhakika walau wa mlo mmoja kwa siku?

Sasa mbona majibu unayo tayari?
Wakati wa Kikwete humu kulikuwa na malalamiko kama haya?
je hizi habari za kampuni kufilisika zinazoripotiwa na Media za kutunga??
 
Sabalkheri na msalkheri wana JF popote pale mlipo duniani.

Sasa leo nina swali. Swali ambalo nimekuwa nikilifikiria na kujiuliza kwa majuma kadhaa sasa.

Hivi kumbe kweli maisha chini ya utawala wa rais mstaafu Jakaya Kikwete yalikuwa bora eh?

Nauliza hivyo kwa sababu ukisikiliza vilio vya baadhi ya watu humu unaweza kupata picha kuwa wakati wa Kikwete maisha yalikuwa mazuri [mno] na sasa baada ya kuingia huyu dikteta Magufuli, ndani ya mwaka tu maisha yamekuwa magumu sana.

Bidhaa zimepanda bei, mabenki yanafilisika, wawekezaji wanaondoka, viwanda vinafungwa, ajira zinasitishwa, kampuni za ndege zinapunguza safari, na kadhalika na kadhalika. Kwa kifupi, hali ya uchumi ni tete.

Kauli mbiu ya rais mstaafu Kikwete wengi wetu humu tuliibeza sana kwa sababu ilikuwa haiendani kabisa na uhalisia wa maisha ya Watanzania wengi.

Ila sasa hivi vilio vya watu [kama si vya kinafiki na kipropaganda] ndo vinanifanya niwaze...kama maisha ya sasa ni magumu, ni magumu kulinganisha na ya lini?

Manake kwangu mimi maisha halisi ya Watanzania walio wengi ni magumu tu siku zote.

Kwa hiyo, kama maisha chini ya Kikwete yalikuwa mazuri au niseme yalikuwa na nafuu ukilinganisha na ya sasa chini ya Magufuli, ina maana Kikwete alifanikiwa kiuchumi?

Kama alifanikiwa kiuchumi, ina maana zile kelele na ukosoaji dhidi yake zilikuwa ni za kinafiki?
Unapopewa vibovu viwili lazima uchague kibovu kimoja chenye unafuu
 
Sasa hivi mmekariri kuwa kila mtu anayelia ugumu wa maisha tofauti na ya awali, enzi za JK alikuwa anaishi kwa mbinu mbinu(kupiga dili)

Sasa sijui huyu mama ntilie anayelia biashara mbaya sijui alikuwa anaishi kwa mbinu ipu?..

Enzi za jK Kulikuwa na uafadhali lakini sasa uafadhali ule haupo, kama ni tajiri ndio unarudi kwenye umaskini na kama Maskini basi unakwenda kwenye Ufukara(dhariri).
 
Hii mada ni kama vile unarudia, ulishajibiwa kuwa,

kuna bad, worse na worst.

Wakati wa Kikwete maisha ya Watanzania wengi yalikuwa kati ya maneno mawili 'bad' and 'worse', leo yako level nyingine kutegemea na wapi ulikuwa.
 
Back
Top Bottom