Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,358
- 6,077
Tokea Rais Magufuli aingie madarakanai tumekuwa tukishuhudia kila aina ya "uozo na madudu" akiyaweka hadharani kiasi kwamba mtu unajiuliza hivi kwa kipindi chote cha miaka 10 iliyopita huyu Jakaya Kikwete alikuwa anafanya nini? Hii nchi haikuwa na Rais wala Serikali??
Uchafu wote ambao Rais Magufuli anahangaika nao leo hii, ulikuweko wakati Kikwete alipokuwa madarakani. Ina maana Kikwete alikuwa hana macho au na yeye alikuwa ni mpiga dili? Kila mahali nchi hii imeoza, hakuna sekta ambayo utasema iko salama; kila mahali wajanja wamepiga, hivi huyu Kikwete kazi yake ilikuwa nini? Hebu jaribuni kujionea wenyewe hii list ya uozo na madudu ya serikali ya Kikwete;
1-Serikalini kulikuwa na wafanyakazi hewa na Kikwete alichukua hatua gani?
2-Utoroshwaji wa madini nje ya nchi Kikwete alikuwa wapi?
3-Wizi wa mapato TRA, Kikwete alichukua hatua gani?
4-Bandarini palikuwa ni sawa na shamba la bibi, wajanja walikuwa wanajichumia pesa na Kikwete alikuwepo tu.
5-ESCROW wajanja walijichotea mapesa na kuyajaza kwenye mifuko ya sandarusi, Kikwete alifanya nini?
6-Utoroshwaji wa wanyama kwenda Ughaibuni, Kikwete alikuwepo tu kama picha
7-Mhasibu wa TAKUKURU kujilimbikizia majumba na magari, Kikwete yupo tu
8-TTCL kuuzwa kwa "buku" moja na Kikwete yupo tu
9-Akina Nyalandu kugawana vitalu vya uwindaji na ujangili kukithiri huku Tembo wakiuawa kila siku, Kikwete alikuwepo tu
10-Watu wanakwenda kufanya vikao vya Board Dubai na wengine kulipana posho za vikao hewa, na Kikwete yupo tu
11-Mashuleni kulikuwa hakuna madawati, yeye yupo tu
12-Mahospitalini wagonjwa walikuwa wanalala chini na yeye yupo tu
13-LUGUMI akizitafuna pesa za "polisi" na yeye yupo tu
14-Mikataba mibovu, na yeye alikuwepo tu
15-.....................
Hivi huyu Rais Kikwete kazi yake ilikuwa ni nini? Au kazi yake ilikuwa ni kwenda kucheza tu kwenye mabembea ya Ulaya?
Amemwachachia Magufuli kazi nzito sana na yeye hakuna alichokuwa anakifanya. Mbaya zaidi ni siku ile anaingia Bungeni kwenda kuhudhuria Mkewe kuapishwa, eti Wabunge wakainuka na kumshangilia na kusema eti wamem-miss; SERIOUSLY?? Hivi sisi Watanzania tuna akili kweli? Hivi sisi Watanzania tumelogwa na nani?
Yapo madudu mengi sana yamefanyika, mimi nimechoka kuendelea kuandika. Hebu na ninyi ongezeeni hapo nilipoishia.