Ina maana gani form 4 kujaza celform za kuchagua shule?

JambaziSugu

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
245
203
Kiukweli nowadays post za shule za A level ni vurugu. Ina maana gani mwanafunzi kujaza celform kuchagua shule then baada ya matokeo unapangiwa shule tofauti? Asilimia kubwa ya wanafunzi waliomaliza mtihani wa kidato cha 4 mwaka 2011 wanalalamika kupangiwa shule wasizozijua. Inaboa sana mtu unafaulu kwa ufaulu mzuri, unachagua shule alafu unapangwa shule isiyoeleweka. Shule za A-level zimekuwa nyingi to the extent zingine hazina hadhi ya kuitwa shule. Unapangiwa shule mpya ndo inaanza ninyi ndo mnakuwa form 5 wa kwanza inakuwaje?. Utakuta shule inaitwa cjui Nang'wanda, mwinyi, mahiwa. Aaaarg! Inaboa!!. Kingine Nisaidieni wadau process za kuhama shule. Nimechaguliwa shule mbovu, nataka nihame faster bila hata kuripoti. Nianzie wapi?
 
ulikuwa unataka upamgwe wapi?chagua shule unayoitaka mimi nina uwezo wa kukuhamisha au ni pm
 
ulikuwa unataka upamgwe wapi?chagua shule unayoitaka mimi nina uwezo wa kukuhamisha au ni pm

Nimescore div i ya 14. Kwenye combi nna A,A,A. Wamenipangia tambaza day. Process za kuhama inakuaje?
 
Nenda bordng za kulipia bac kama hutak kwenda shule uliopangiwa na government,bora hata mie nimechaguliwa TECHNICAL COLLEGE(D.I.T) mambo pouwa.
 
meonaee me nime2pwa xongea kudadadek.yan ntaka nihame fasta



shule za serikali zote zinafanana! Kapige shule tu, mwisho wa siku utaona matunda...nakumbuka wakati nipo Njombe kuna jamaa alihamia toka Minaki, tukamuuliza kulikon akadai minaki hakuna walimu, wakati huo tulikuwa na mtu darasan anang'ang'ana aamie Minaki...aliishiwa. Kaa ukijua shule zote za govt zinatofautiana katika matatizo.
 
we unataka shule gani? Tulia kijana, utapoteza muda wako. We endelea kuhangaika na mwisho wa siku lazima upate 4 au zero.
Sio kwa style hiyo. Umeona lini PCB anachomoka Tambaza au Benja! Pale magumash tu. Sanasana usubiri 4 yako tu. Uctegemee kufika Muhimbili.
 
Kuna case nyingine ambazo ni seriuos, mwanafunzi amefaulu PCB kwa kiwango cha CCC na alichagua comb za sayansi kuanzia 1-4 ya tano ndiyo akaweka HGL; sasa amechaguliwa kwenda HGL ambayo ana DDC.
Halafu tunalalamika TZ hatuna wanasayansi! - NIPENI MANTIKI KATIKA HILO NA JE MTOTO HUYU AFANYEJE? baba yake yuko kijijini hawezi kumlipia private. Hii si kulazimisha mjaze shule za arts kwa kuwa ni nyingi?
Mwaka jana niliweka topic humu ya mwanafunzi wa kike aliyefaulu PCM kwa kiwango cha DCC lakini hakuchaguliwa kwenda kidato cha tano wala ualimu eti tu kwa sababu ana div IV ya pts 26. Nadhani sasa ameshakata tamaa, sijui yuko wapi.
Tufike mahali tuangalie jinsi mtoto alivyofaulu combination husika; suala la points liwe ni kuwapanga (RANKING) tu.
Ikibidi tufikirie kuwapunguzia watoto masomo iliwa-specialize. Kuna haja gani ya kulazimisha masomo saba wakati masomo matano tu yangeweza kufanya mtoto aka-concentrate zaidi na kufaulu vizuri. Kwa mfano akisoma Physics, Chemistry, Biology, Mathematics, na Geography tayari anazo comb nyingi tu. Kwa nini tumlazimishe eti lazima na kiswahili, kiingereza, civics etc?. Halafu eti siku hizi mnawalazimisha comb tano!
 
Back
Top Bottom