In kilolo; nape awapa somo viongozi wilaya ya kilolo

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
KATIBU wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Nape Nauye amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo kuzuia madandarasi wanaofanya kazi katika wilaya hiyo ambao wanashindwa kutoa ajira kwa vijana kutoka ndani ya wilaya hiyo.



Nauye ametoa agizo hilo Leo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Ilula katika wilaya hiyo ya Kilolo.


Alisema kuwa lengo la serikali kuanzisha miradi ya maendeleo vijiji na wilaya ni kuona Kuwa wananchi wananufaika na miradi hiyo hivyo lazima ushiriki wa wananchi katika miradi hiyo uwepo na wanaopaswa kunufaika na miradi hiyo ni wananchi wanaozunguka miradi hiyo hivyo lazima hata wanaopewa kazi ya kujenga miradi hiyo lazima wananchi hasa vijana kupewa ajira katika miradi hiyo.


Kwani alisema kuwa miradi hiyo haitakuwa na faida kwa wananchi iwapo makandarasi wa miradi hiyo wakatumia Wafanyakazi kutoka nje ya wilaya hiyo ya Kilolo.


Hivyo aliuangiza uongozi wa wilaya ya Kilolo kusimamia suala la ajira kwa wananchi wa wilaya hiyo ya Kilolo ambao wanasifa ya kufanya kazi .


Aidha Nauye alipiga marufuku tabia ya watendaji hasa mabwana shamba ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango ikiwa ni pamoja na Kwenda ofisini wamevaa suti wakati wao wanatakiwa kuwatembelea wakulima mashambani .


Alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya mabwana shamba kushinda maofisini huku wakiwa wamevaa suti wakati serikali imekuwa ikiwalipa mishahara kwa kazi hiyo ya kusimamia kilimo.


Kuhusu Suala la pembejeo za Ruzuku ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali alitaka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mkuu wa wilaya hiyo ya Kilolo iwapo watabaini kuwepo kwa wakala ama kiongozi anayechakachua vocha hizo za ruzuku Pindi zitakapotolewa na serikali.


Alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2012/2013 iliyosomwa mapema wiki hii na waziri wa fedha na uchumi DKT Wiliam Mgimwa ni bajeti ambavyo imewajali zaidi wakulima na kuwa kazi nzuri imefanywa na wabunge wa CCM katika kupigania suala zima la kilimo.


wakati huo huo Nauye alipinga hatua ya vyama vya upinzani kuendelea kubeza jitihada za serikali ya CCM chini ya Rais DKT Jakaya Kikwete kwa Madai hakuna kitu kinachofanyika kuwa huo ni upotoshaji mkubwa na wananchi wanapaswa kuwa makini na upotoshaji huo.


Kwani alisema kuwa CCM ndicho Chama pekee ambacho kitaendelea kuongoza nchi na kuwa wao vyama vya upinzani wamekuwa wakizunguka kupandikiza chuki kwa wananchi ili waichukie serikali ya CCM jambo ambalo wananchi wanapaswa kuwa makini na upotoshaji huo.


Nauye alisema kuwa vyama vya upinzani vimekuwa vikipotosha umma kuwa wao Ndio waasisi wa vita dhidi ya ufisadi lakini ukweli vita hivyo vilianzishwa na CCM kwa kipindi hicho kikiwa Chama cha TANU kupitia azimio la Arusha ambapo kwa wakati huo mafisadi waliitwa ni wahujumu uchumi .


Hata hivyo alisema kuwa vita dhidi ya ufisadi bado inafanyika ndani ya CCM kwa kuwawajibisha wahusika na kutaka watumishi wa umma kuendelea kuonyesha uzalendo na Taifa.



Alisema kuwa kwa mwaka huu CCM umepiga marufuku wanachama wala Rushwa ama watoa Rushwa kuchaguliwa na kuwa ikibainika kuna mtoa Rushwa amechaguliwa ushindi wake utapokonywa ili kulinda heshima ya Chama.


Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu ndani ya Chama watoa Rushwa hawstakuwa na nafasi na iwapo itabainika mwanachama wa CCM kashinda uchaguzi kwa kutoa Rushwa atakuwa amepoteza sifa ya kuwa kiongozi ndani ya CCM.


My TAKE; Sidhani kama huyu jamaa kwa cheo chake ana mamlaka ya kuamrisha viongozi wa halmashauri, kwani nchi yetu ilishatoka katika enzi za Chama kushika hatamu.

Ndg. Nnauye I think you need to move away from that old-fashioned paranoid confrontational Chama-dola mentality and find a better way of doing your job, kwani hata hao watumishi wauma unazidi kuwaongezea hasira tu kwa kuwafata na kuwakoromea kama Mwanri au Pinda!
 
Back
Top Bottom