Impossible is richness. Lisilo wezekana ndio utajiri. The problems is that the rich man is not yet a rich, and a poor man is not yet a poor

Ghost boss

Member
May 3, 2019
29
75
IMPOSSIBLE IS RICHNESS. LISILO WEZEKANA NDIO UTAJIRI

The problems is that the rich man is not yet a rich and a poor man is not yet a poor. Hayo ni maneno kutoka kwenye kitabu cha rich dad and poor dad cha Robert kiyosaki. Jambo ambalo linaonekana haliwezekani ndilo lenye siri ya unapotaka kuwa. Mwenyezi Mungu ali wahi sema anaonyesha njia ya hazina na mahali pa siri pa utajiri. Utajiri umejificha kwa Yale yasiyoonekana, sio rahisi kuuona nandio maana matajiri ni asilimia chache tu duniani, Mara nyingi watu wanao penda kuwa sawa kuendana na dunia kamwe hawafiki popote, watu Mara nyingi upenda kufanya Yale ambayo kila MTU hutarajia kufanya. Usawa utakuzamisha kwenye jambo lolote lile unalofanya,

Ukiwa unafanana na watu wengi kwa asilimia 90 Basi ujue sio rahisi kutoka hapo ulipo. Kwenye biblia inawataja wanawake watano wenye hekima na wanawake watano wapumbavu, wale wenye hekima walikuwa na hekima sio kwasababu nyingine yoyote ila ni kwasababu walibeba mafuta kwenye taa zao na wapumbavu hawakuwa na mafuta kwenye taa zao. Kitendo cha wale kuwa na mafuta kwenye taa zao wakawa na busara na wale waliokosa mafuta wakawa wapumbavu, upumbavu na hekima ni vile au uwezo wakufanya mambo tofauti na wengine.

Asilimia kubwa ya jamii hufanya mambo ya kufanana na kuwafanya wote wawe sawa na yeyote anayefikiria nje ya box huonekana waajabu sana na jambo lake haliwezekani, utasikia wewe ushaona wapi iyo kitu ikafanya Kazi bongo? Au ushaona jambo ilo afrika? Hata ulaya hawajawahi Fanya hivyo kwaiyo jambo lako haliwezekani. Misemo hiyo ndio huwaangusha wengi na kuwafanya wengi wawe kwenye maeneo ambayo hawakupaswa kuwa.

Jambo huwezi au haliwezekani ni siri ya kukutoa kwenye hatua moja hadi nyingine, huwezi ukaanzisha biashara ya nyanya kwenye sehemu yenye nyanya nyingi zinapouzwa na ukategemea ufanikiwe hapo, ila pale nyanya ambapo hazipo na sio rahisi kupatikana ilo ndio eneo sahihi la kuuzia nyanya, sio kwa vile George kafanya vile Basi jamii nzima mnataka mfanye kama George na kisha mfanane na George mshindwe mumuite mchawi. Kila MTU Mungu amempa upekee nisawa tu watu wakisema jambo hilo haliwezekani kwa vile ni kwasababu karama yako sio sawa na yao ukisoma soma biblia utaona Hadithi ya Bwana mmoja aliwapa watumishi wake pesa mwengine tano, mbili na moja,

Kila Mtu alipewa pesa kulingana na uwezo wake Wa kuzalisha sasa kama wewe ulipewe tano na unamsikiliza aliyepewa moja hilo sasa nitatizo lazima akuambie kuwa huwezi kuanzisha Microsoft, kwakuwa yeye kitu Microsoft haipo kwenye mawazo yake, nisawa tu watu wakiona jambo kwako lisilo wezekana, kujiingiza kwenye umoja na kisha kufanana na kila MTU iposiku utaadhibiwa, nisawa kuambiwa mawazo yako niyakipuuzi haya wezekani na unaota ndoto za mchana, ila ni hatari sana ukaambiwa upo sawa hata Juma alifanya hivyo na Alex alipita hapo.

Jambo la muhimu ni lile linalofanywa na wachache na sio jamii nzima, ukiona jambo linafanywa na jamii nzima ujue ni useless halina maana kabisa. Ukiona wazo lako halifanani na MTU yeyote ujue upo sawa kabisa, ukiona wazo lako linakosolewa kuwa haliwezekani ujue ndio wazo bora, hakuna aliyeijua Microsoft ila bill gate, angetaka tuwe sawa wote tungekuwa tu na Leo sijui angekuwa nani, jackma alisema alikuwa akiwaambia watu juu ya wazo lake la alibaba watu wakawa wanapuuza na kuona ni wazo lisilo weza kufanya Kazi,

Impossible ndio siri ya kufanikiwa, pale panapo onekana pana utulivu ujue hakuna utulivu ila pale penye vurugu ndio penye utulivu, eneo linaloonekana lina amani ndilo linaloongoza kuuwa watu wengi zaidi duniani, mfano mbu hakuna anaye muogopa wala kuhofu ila ndio anaongoza kuua watu wengi zaidi kuliko ukimwi na cancer. Ile comfort zone ndio eneo baya sana duniani. Kimbilia kwenye lisilo wezekana achana na mkumbo Fanya kwaakili yako inavyokutuma maana wewe ni MTU sahihi na kama kila MTU angekuwa sawa na wewe Mungu asingekuwa na haja ya kuumba kundi kubwa la watu wanao fanana,

Wewe ni wewe na hakuna kama wewe jambo lisilo wezekana kwa Pascal linawezekana kwa Juma ila Juma akilegeza akili akiona pascal yupo sahihi Basi Juma mwisho wake ni mbaya. Hakuna kiongozi Wa maisha yako zaidi ya Mungu na wewe lolote utakalo taka kufanya Fanya maana hakuna kama wewe ilojambo lako ndio Yale maisha tunayo yasubili imagine bila Thomas Edson tunangekuwa na taa kweli tungeweza kurekodi kweli, bila mark Leo tungekuwa na Facebook. Bila Jeff bezo tungekuwa na amazon Leo, angalia bila bill gate tungekuwa na Microsoft kweli hata sema mambo yangekuwaje kwa uchache wake, yule aliyetengeneza simu kabla haja tengeneza simu aliwashirikisha wazo lake ndugu na rafiki.

Baada ya ndugu na marafiki kumsikiliza walimfunga kamba na kumpeleka hospitali wakampime akili maana walihisi amesha changanyikiwa, how come MTU uwasiliane na MTU Wa mwanza kwa sekunde tu wewe ukiwa mbeya,? Ndugu waka mtia kamba wakamuwaisha hospitali asije akaleta tabu zaidi.

Fanya kile unachokipenda na kutaka sio kwasababu tumesema hatujawahi sikia ilo Basi ukate tamaa huo ni Mwanzo wakutafuta kukaa jehanam kama hutatumia kile ulichopewa kwa kuogopa macho ya watu kama pilato.

Aaamen
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom