Impeachment of Kikwete only solution out of official graft.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Impeachment of Kikwete only solution out of official graft....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Jamani tuache blablaa..................Kikwete ndiyo chimbuko la ufisadi hapa nchini na ushahidi upo wa wazi kabisa..........Hivyo haiwezekani kila siku ni wadogo zake tu ndiyo wanawajibika na yeye anabaki akila kuku kwa mrija..... Sasai wakati umefika wa kuanzisha msukumo wa kumfukuza kazi kupitia Bunge letu.....................

  Chadema wanao wabunge wa kutosha wa kuanzisha muswada wa kumchunguza JK na ni jukumu letu kuanzisha vuguvugu la kuwashinikiza wabunge wa CCM kutuunga mkono kwenye hilo kwa maandamano nchi nzima.........................

  Bila ya kufanya hivyo itafika mahali watakapomaliza vya kupora......hii serikali ya kifisadi wataanza kututafutia soko la kutuuza sisi wazima wazima na huku tunaona.........................


  IMPEACHMENT OF KIKWETE ONLY PATH OUT OF OFFICIAL GRAFT.  The election of Kikwete in 2005 was greeted by plenty of goodwill and jubilation. The main reason why the nation had contemplated too much on Kikwete shoulders was flowing from an ennobling promise Kikwete and his CCM henchmen had deceptively injected upon us: The promise of change and new ways of conducting public affairs.

  Five years down the road, the nation was shocked to learn actually Kikwete was worse than his predecessor Mr. Benjamin Mkapa whose name had, in 2005, become synonymous with official graft. The nation was forced to hurtle from one scandal to another whereof some of those disgraceful scams led to ignominious departures of Kikwete's closest allies not excluding Edward Lowassa who earned an unenviable titular of having served the premier docket in the shortest stint in our short Independence history!

  Following the parliamentary diktats, that require the Takukuru Chief Mr. Hosea being shown the door for misleading the nation on Richmond scandal, only Kikwete was reading a different script when he decided to defy parliamentary authority and protect Mr. Hosea there at Takukuru. The only reason that can explain this Kikwete's u-turn on the fight against official graft was: He was a beneficiary of it. There is no any apt narrative that can explicate Kikwete from his refusal to obey parliamentary directives but the lures to his self-gratifications.

  Then we thought the decision to severe ourselves from the Richmond/ Dowans scams had extended a huge relief upon us but then came a telling blow from an arbitrator's award that smacks of official graft engineered from State House. How can we exculpate Kikwete from personally interfering in Tanesco's Board of Directors' mandate to fill the vacant post of Executive Director? It is the Kikwete personal pick of Dr. Idrissa Rashid to head Tanesco contrary to laid down procedures which had triggered off events leading to Tanesco being forced to depart with an excruciating sum of over Tshs 185 billions.

  From Tanesco Board of Directors' advertisement that was head-hunting her Chief Executive Officer, it was very lucid that only registered engineers with post graduate qualifications in Business Administration stood a chance of being considered. Surprisingly, when Tanesco announced that they had settled upon Dr. Rashid - the nation stood gaping at these despicable acts of flouting parastatal procedures. Equally puzzling, Dr. Rashid was a sexagenarian something our laws disdain in full: Mandatory retirement age stands at 60 years while Dr. Rashid was already 62 and counting at a time he joined Tanesco!

  Matters were not made easier when Dr. Rashid being a swashbuckler in chief bragged in public that after all he did not even applied for the job confirming our worst fears that his appointment at Tanesco was an upshot of State House engineered cronyism. And Kikwete was the chief mastermind………Why should he not take the rap?

  Under Dr. Rashid auspice, Tanesco surreptitiously conspired with both Richmond and Dowans to siphon off billions of shillings from the parastatal leaving this nation in a precipice of being conned in daylight. Since Kikwete was the architect of the now infamous appointment of Dr. Rashid at Tanesco, I am urging the House to move quickly and decisively to interdict and impeach him immediately.

  This nation can not inexorably be held hostage by a president whose ambition to lead this nation is percolating from his self-aggrandizement schemes and he has neither a sense of ethics nor honour. It is now up to the House to rise to the occasion and rebuke this brazen president through a carefully scripted impeachment process and stop him from damaging further the institution of presidency. The nation is watching…


  Mahali pa kuanzia katika kumtimua Kikwete kazi ni Richmond/Dowans scandal...........haiwezekani nchi ikalipa ufisadi huu wa wazi na Kikwete aendelee hapo alipo.............Anatucheka..............It is time to call a spade a spade but not a big spoon.................Are you ready to be part of this piece of History makers.............
   
 2. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma

  You are very correct.

  According to our Tanzania National Constitution it allows an impeachment to the President of the United Republic of Tanzania. I suggest for the opposition parties under leadership of CHADEMA to organize an impeachment immediatelly after Bunge session begins in early February,2011.

  Hapa chini nimenukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoeleza bayana namna ya kumshtaki Rais ndani ya Bunge baada ya kufanya madudu kama haya ya RICHMOND/DOWANS. Kinachotakiwa ni Asilimia 20% ya Wabunge kuiunga mkono na kutia sahihi Taarifa ya Maandishi yenye kueleza bayana MAKOSA ALIYOYATENDA RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA MADARAKANI.

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  _________________________________________________________________
  32
  Kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
  Sheria ya 1992
  Na.20 ib.5
  Sheria ya 1994
  Na.34 ib.
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

  (a) Baada ya Bunge kuvunjwa;
  (b) Baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge kwanza:
  (c) Baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasi madaraka ya kuchaguliwa;
  (d) Baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba hii, na kuondolewa katika madaraka;
  (e) Baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi
  kumudu kazi na shughuli zake;
  (f) baada ya Rais kufariki.
  (3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.


  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  _________________________________________________________________
  37
  Bunge laweza kumshtaki Rais
  Sheria ya 1992 Na.20 ib.8
  Sheria ya 1995 Na.12 ib.4  46A
  .-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakaniendapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
  inadaiwa kwamba Rais-

  Sheria ya ….


  (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

  (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au (c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
  (3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-
  (a) Taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
  Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
  (b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
  kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
  wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
  (4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
  (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
  (b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  _________________________________________________________________
  38
  (c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
  uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.
  (5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa dhidi yake.
  (6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
  (7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
  (8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
  utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge. (9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
  kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika
  (10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
  (11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Raia inabidi tuwahamasishe kwa maandamano mpaka Bunge lililofurika CCM liogope na kusikiliza kilio cha raia..kuwa Enough is Enough.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Chadema badala ya kupoteza muda kwenye majukwaa ya vyombo vya habari pekee ni vizuri wakakutana na kujadili mkakati wa kumfukuza kazi Kikwete vinginevyo huu ufisadi utaendelea kushamiri na kutuumiza raia wanyonge............
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Sijui kama bado mnaukumbuka huu unafiki wa JK.........katika gazeti la Habari Leo.....

  Habari za Kitaifa

  JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd April 2009 @ 07:30 Imesomwa na watu: 13275; Jumla ya maoni: 10

  Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

  "Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

  Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

  Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.

  Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

  Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

  Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

  "Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana. Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

  Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla. "Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema. Kuhusu msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unaanza leo London, Uingereza, alisema umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

  "Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini, itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na masikini. Matajiri watakuwa masikini na masikini watakuwa fukara zaidi," alisema. Alisema kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora.

  "Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinahitaji sana, bado hazijasaidiwa," aliongeza. Pia alielezea masikitiko yake kwa ajali tatu zilizotokea hivi majuzi, ya magari Mbeya; ya treni mbili zilizogongana Dodoma na ya mgodi kufukia wachimbaji, Geita.

  "Kwa ajali zote hizo tatu, moyo wangu uko pamoja na familia za wafiwa na waliojeruhiwa. Majonzi yao ndiyo majonzi yangu. Na machungu yao ndiyo machungu yangu. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wetu hao mahali pema peponi. Amin!" Alisema na kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa taifa.
   
Loading...