IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki

Afyayaakili

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
923
1,255
Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.

Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.

Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .
Image caption
Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.

Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.

Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.

IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.

Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.

Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Image copyright
Getty
Image caption
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.

Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.

Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.

Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
Ivory Coast 8.5%
Tanzania 6.9%
Senegal 6.6%
Kenya 6%
Zambia 3.4%
Nigeria 2.3%
Afrika Kusini 0.6%
 
Hizi takwimu zioane na hali halisi ya maisha ya watu wake,sio uchumi unakuwa alafu kunakuwa na mfumuko mkubwa wa bidhaa mtaani,huko vijijini ndio hakuelezeki psssss
 
Bado kuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi na kuwa kwenye double-digit growth. Ivory Coast cannot do better than Tanzania given the resources we have as a country. Nina hakika wanafanya vizuri kuliko Tanzania kwa sababu wameanza kuweka structures za uchumi wao vizuri kuliko huko nyuma. Hata hivyo, 6.8% tuliyofikia isiwe kigezo cha kuamini ukuwaji wa uchumi ukizingatia kwamba tulikuwa tumefika pabaya huko nyuma.
 
tukaze buti tuwe wa kwanza............
najua inawezekana
kwa kuweka sera nzuri katika madini na rasilimali nyingine..............
mirija ya wapigaji wa ten percnt ikatwe......
vasco
 
Hizi takwimu zioane na hali halisi ya maisha ya watu wake,sio uchumi unakuwa alafu kunakuwa na mfumuko mkubwa wa bidhaa mtaani,huko vijijini ndio hakuelezeki psssss
Utapeli wa wazungu huu, hamnaga kitu hapo
 
Maswali ya ku - digest - Je:

Ni sekta zipi zinachangia kasi hii ya uchumi kukua kwa karibia 7%?

Sekta hizi zinashirikisha wananchi kwa kiasi gani - kwa maana ya (ajira) employment na fursa mbalimbali kwa wananchi kama vile the supply and/or goods and services (upstream and down stream linkages)?

Sekta yenye kuajiri nguvu kazi kuliko zote (Kilimo) imekuwa kwa kiasi gani? Sana sana asilimia tatu, tena ni wastani wa miaka 15 (tokea 2000). Maana yake nini? Maana yake ni kwamba kasi hii haishirikishi na haina manufaa kwa wananchi walio wengi.

Mwaka 1999/2000, tuliambiwa kwamba nchi maskini kama Tanzania ikifanikiwa kukuza uchumi wake kwa 7% au zaidi kwa miaka 15 mfululizo, umaskini utapungua kwa asilimia hamsini (50%) au zaidi. Tumefanikiwa kuwa na wastani karibia na huo kwa miaka 15 mfululizo. Je umaskini miongoni mwa watanzania umepungua kwa kiasi gani? Hatujafanikiwa hata kwa 10%. Je mafanikio ya kukua kwa kasi hii ya uchumi yameshuka huko chini kwa wananchi kwa kiasi gani? Ukweli ni kwamba yamebakia huo huko huko juu.

Mafanikio ya uchumi wa "NCHI" yanatakiwa kugeuzwa kuwa mafanikio ya uchumi wa "WANANCHI". Vinginevyo ni maigizo tu ya kuona wawekezaji wakija kuchimba chimba mashimo kuchukua madini yetu, kisha katika takwimu, uzalishaji wao kuchangia kasi ya kukua kwa uchumi kwa 10% au zaidi, huku wananchi wakiendelea kuishi maisha ya tabu.

Kuna kila dalili kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya chama kile kile CCM, haitaweza kuondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.

To put it in a nutshell - Umaskini ndio mtaji wa CCM. Umaskini unakisaidia chama hiki kikongwe to pracatice her cheap populist strategies to win the hearts of the poor, especially the rural poor. Thats how the party has survived in power for over 50 years.

Lakini yapo matumaini. The future is 'Urban' ambapo by 2025, watanzania wengi zaidi watakuwa wanaishi mijini kuliko vijijini.

Even magicians run out of tricks. Mazingaombwe ya CCM yatakomea hapo.
 
Hii habari habari ni ya kupikwa nakumbuka Na zile tuzo alikuwa anapewa kikwete kwa mfululizo wakati ukiangalia zilikua haziendani Na uhalisia wowote.
wameanza tena kwa Magufuli ili kumsahaulisha shida za Tanzania.

Kusema ukweli Tanzania Hali bado ni mbaya sana tukiachana hizo propaganda hao IMF wanatudai pesa nyingi sana.
 
Maswali ya ku - digest - Je:

Ni sekta zipi zinachangia kasi hii ya uchumi kukua kwa karibia 7%?

Sekta hizi zinashirikisha wananchi kwa kiasi gani - kwa maana ya (ajira) employment na fursa mbalimbali kwa wananchi kama vile the supply and/or goods and services (upstream and down stream linkages)?

Sekta yenye kuajiri nguvu kazi kuliko zote (Kilimo) imekuwa kwa kiasi gani? Sana sana asilimia tatu, tena ni wastani wa miaka 15 (tokea 2000). Maana yake nini? Maana yake ni kwamba kasi hii haishirikishi na haina manufaa kwa wananchi walio wengi.

Mwaka 1999/2000, tuliambiwa kwamba nchi maskini kama Tanzania ikifanikiwa kukuza uchumi wake kwa 7% au zaidi kwa miaka 15 mfululizo, umaskini utapungua kwa asilimia hamsini (50%) au zaidi. Tumefanikiwa kuwa na wastani karibia na huo kwa miaka 15 mfululizo. Je umaskini miongoni mwa watanzania umepungua kwa kiasi gani? Hatujafanikiwa hata kwa 10%. Je mafanikio ya kukua kwa kasi hii ya uchumi yameshuka huko chini kwa wananchi kwa kiasi gani? Ukweli ni kwamba yamebakia huo huko huko juu.

Mafanikio ya uchumi wa "NCHI" yanatakiwa kugeuzwa kuwa mafanikio ya uchumi wa "WANANCHI". Vinginevyo ni maigizo tu ya kuona wawekezaji wakija kuchimba chimba mashimo kuchukua madini yetu, kisha katika takwimu, uzalishaji wao kuchangia kasi ya kukua kwa uchumi kwa 10% au zaidi, huku wananchi wakiendelea kuishi maisha ya tabu.

Kuna kila dalili kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya chama kile kile CCM, haitaweza kuondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.

To put it in a nutshell - Umaskini ndio mtaji wa CCM. Umaskini unakisaidia chama hiki kikongwe to pracatice her cheap populist strategies to win the hearts of the poor, especially the rural poor. Thats how the party has survived in power for over 50 years.

Lakini yapo matumaini. The is 'Urban' ambapo by 2025, watanzania wengi zaidi watakuwa wanaishi mijini kuliko vijijini.

Even magicians run out of tricks. Mazingaombwe ya CCM yatakomea hapo
.

Nimeipenda hii.Hapa umeongea facts tupu. Bado nchi hii hakuna uzalendo wa kweli.Kuongezeka kwa pato la Taifa isiwe kwenye kukusanya kodi tu pesa wakaziweka hazina na zisitusaidie kitu chochote kama awamu zilizopita uchumi kukua kwa 7% huku sarafu yetu ikiporomoka vibaya.

Haya ni madhara ya kuendekeza wawekezaji kupita kiasi na sisi kishindwa kuboresha uwezo wa ndani kwa watanzania kupewa fursa kwanza za uwekezaji.

Kwamfano mimi siamini dunia ya leo hakuna mtanzania asiye na uwezo wa kuendesha kiwanda kusindika bidhaa zitokanazo na kilimo,mifugo na uvuvi watanzania wenye nia ya dhati wapo ila mifumo yetu hasa siasa ya chama tawala mibovu ya kupendelea wachina,wahindi na mataifa mengine kuwa wao ndio wanao weza matokeo yake wamekuwa wakivuna huku kwetu sana fedha zetu wanakwenda wekeza kwenye nchi zao sisi tukiambulia kodi tena inayokusanywa chini ya kiwango ukilinganisha na wanachozalisha.

Tukiboresha uwezo wa ndani kwa maana ya kuwawezesha watanzania kwanza mgeni baadae kwa kutumia sera madhubuti tutaongeza uelewa wetu na thamani ya rasilimali tulizo nazo kwa sasa na vizazi vijavyo na sio kiwaachia hawa wezi tunaowaita wawekezaji wakatufanyia kila kitu.
 
Mkuu,
hoja zako zinaamsha na kufikirisha, kwa mfano, uchumi (GDP) unakua kwa karibia asilimia saba ya pato la taifa kwa miaka 15 mfululizo, lakini makusanyo ya kodi as percentage of GDP bado ipo pale pale kwa miaka yote 15, yani 12% to 13% of GDP. Tunashangilia ongezeko la kodi kwa sababu 12% ya trilioni 30 sio sawa na 12% ya trilioni 80. Lakini kwanini hatudadisi kukwama kwa 12% kwa kipindi chote?
 
tunaongoza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi na si ukubwa wa uchuhumi

Uko sahihi. Twende kwa mfano rahisi; nitalinganisha Mkulima mmoja masikini kule kijijini (Tanzania) na Tajiri mmoja wa Dar es Salaam (SA/Nigeria). Kutokana na hali nzuri ya hewa kwa miaka mitano mfululizo, Mkulima huyu kipato chake kiliongezeka kutoka T.Shs. 35,000; 60,000; 110,000; 180,000; na 450,000 kwa miaka hiyo mitano.

Kwa upande mwingine, kutokana na mdororo wa uchumi wa dunia mapato jumla ya Tajiri yule kwa miaka mitano mfululizo yamekuwa yakiporomoka kutoka USD 110m; 105m; 85m; 60m; na 35m.

Huwezi kusema eti Mkulima yule ana hali nzuri ya kimaisha kuliko Tajiri simply kipato chake kimekuwa kikikua kwa kasi ilhali cha Tajiri kimekuwa kikishuka. Ni sawa na Kusini ilivyo mbali na Kaskazini!
 
Mkuu,
hoja zako zinaamsha na kufikirisha, kwa mfano, uchumi (GDP) unakua kwa karibia asilimia saba ya pato la taifa kwa miaka 15 mfululizo, lakini makusanyo ya kodi as percentage of GDP bado ipo pale pale kwa miaka yote 15, yani 12% to 13% of GDP. Tunashangilia ongezeko la kodi kwa sababu 12% ya trilioni 30 sio sawa na 12% ya trilioni 80. Lakini kwanini hatudadisi kukwama kwa 12% kwa kipindi chote?

Nikweli kabisa.Lakini tunarudi kwenye misingi ile tuliyojiwekea kwamba viongozi wetu wamekuwa wakipenda shortcut katika kujenga uchumi ikiwemo wasomi ambao wametumia dhana ya uwekeza kama sera ya kukuza uchumi.
Lakini huwezi kukuza uchumi bila wewe mwenyewe kushiriki. Namaanisha sio ku shiriki katika mikataba ya kusaini na kukusanya kodi bali sisi wenyewe tushiriki mojakwamoja katika sekta mbalimbali kwa vitendo sio kwenye makaratasi tu.
Kushindwa kufanya hivyo inatunyima fursa ya kucontrol uchumi ndio maana hiyo 12% iko hapo hapo na hizi figure wanatoa vyombo vya uchumi kutoka nje na sio figure hali inayoakisi uchumi wa ndani.

Hii inaleta taswira kwamba uchumi wetu wa ndani asilimia 99% unamilikiwa na wageni ambao wao ndio wenye maamuzi yote na ndio maana wawekezaji wengi wamekuwa wakitunyanyasa na kuleta jeuri na kufanya wanachotaka kwasababu wanajua hawa watanzania wote na viongozi wao hawajielewi.
 
Takwimu za kwenye makaratasi hazioani na maisha halisi, ya kibongo
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Naandaa uzi maalum juu ya Magufuli na Uchumi 2015-2020: Matarajio na Changamoto. Nitahitaji sana mchango wako.
 
Back
Top Bottom