IMF: Nchi za kipato cha chini hupoteza 50% kwa miradi ya miundombinu isiyo na tija

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limetoa ripoti kitabu cha kuonesha namna bora ya kufanya miradi ambayo itakuwa na uchumi jumuishi ambao utapunguza tofautii kati ya walionacho na wasionacho.

Kitabu hicho kimeonesha miradi ya serikali huwa ya gharama sana na huwa haina ubora. Pia huwa haina manufaa kwa watu na uchumi kwa ujumla.

Kwa kuwa serikali huwekeza kwenye miradi mikubwa ya muda mrefu isiyo na tija hutengeneza mianya ya rushwa na ubadhirifu ambao hupoteza hadi 50% ya fedha za uwekezaji wa miundombinu husika.

Ili kupunguza ubadhirifu na wizi katika miradi ya serikali IMF imeshauri kuwa na taasisi imara na uongozi bora wakitolea mfano Chile na Korea ambao walianikiwa kuweka uwazi katika shughuli za ugavi wa serikali.

IMF imesema miradi ya serikali inapaswa kuwa jumuishi, kupunguza tofauti ya kipato kwa walionacho na wasionacho na kutengeneza fursa za kiuchumi kwa wote.

Wamesema nchi nyingi zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la #COVID19, miradi ya serikali inaweza kuurudisha uchumi katika hali nzuri. Ambapo fedha za walipa kodi inapaswa kutumika kwenye miradi stahiki.

Katika hilo wameshauri kuwekeza katika Afya, Mazingira na Digitali itaboresha maisha ya watu kwa kuunganisha masoko na kuongeza ustahimilvu wa nchi kwa mabadiliko ya hali ya hewa na majanga yanayokuja.

Ujumbe wao ni kuwa ‘Kukomesha upotevu wa fedha kwenye miradi ya serikali na kutengeneza miundombinu bora yenye lengo na mipango ya kuboresha usimamizi bora wa miradi’
 
'Kwa kuwa serikali huwekeza kwenye miradi mikubwa ya muda mrefu isiyo na tija hutengeneza mianya ya rushwa na ubadhirifu ambao hupoteza hadi 50% ya fedha za uwekezaji wa miundombinu husika.'

Si ndio maana wamekomalia ujenzi ujenzi ujenzi maana wana 10% hapo.
 

IMF: NCHI ZA KIPATO CHA CHINI HUPOTEZA 50% YA FEDHA KWA MIRADI YA MIUNDOMBINU ISIYO NA TIJA

Imesema Miradi ya Serikali huwa ya gharama na haina manufaa kiuchumi

Miradi ya muda mrefu huleta mianya ya rushwa inayopoteza hadi 50% ya fedha

 
Back
Top Bottom