IMF na World Bank tambueni hii nchi ni huru

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Miaka ya nyuma niliwai soma kitabu cha Mwaharakati wa Guyana ambaye hata miaka ya 70 aliwai fundisha chuo Kikuu cha Dsm. Kwenye kitabu hicho cha How Europe under developed Africa kwa tafsiri yangu ni:Jinsi Ulaya inavyoifukarisha Africa..

Ukisoma kitabu hicho utagundua mambo mengi sana kuhusu hawa jamaa Imf na world bank jinsi wanavyokuja na sera mbovu za kuendesha uchumi kwenye za Africa.

Na wakikuta Nchi ina msimamo kama tunavyoona hapa sasa Tanzania lazima wanakuja na mizengwe mingi ilmradi tu wao ndo wawe wanashauri wa sera zote za kuendesha uchumi wako.

Ifike mahala Watanzania tuache kushadadia vitu vya hovyo na kuacha mshikamamo na Utaifa wetu hasa kwenye mambo ya msingi kama haya.

Mh Rais Magufuli tunaomba endelea na msimamo wako katika kuendesha uchumi wa Taifa letu sio kupelekeshwa na hawa mabeberu ambao kimsingi huwa hawatutakii mema.

Alex Fredrick
Dar es salaam
 
Mshikamano wa kitaifa unaouzungumzia ni upi? Mnatesa watu,mnawafunga wapinzani bila sababu yakiwa fika shingoni ndio mnataka tushirikiane?

Kama mmelikoroga kunyweni wenyewe,kwanza hao IMF na WB mmeanza nao urafiki leo?

Je tangu lini ndio mmejua kwamba ni wabaya?
Mbona uchumi ukiwa unakua kwa 7% mlitingisha sana makalio ila saiz umeenda 4% ndio mnataka tuomboleze wote.

Kwanza msituchoshe sana na nyuzi zenu za WB na IMF zmekuwa nyingi sana na chama maana mnachojadili hakuna
 
Akili yako ina uelewa mdogo sana..tunachokataa kupangiwa masharti ya hovyo..wewe unajua wanachokifanya hawa wajinga?mbona wao wanavyopora rasimali barani Africa hilo huwa hawazungumzi?Tumepata Rais bora Magufuli ujinga wao wapeleke huko sasa wanatafuta vijisababu tu
 
kama utaki kupangiwa na wewe ukome kutembeza bakuli kwao na bila hata aibu wanakupa msaada mpaka wa net na condom bila kusahau arv
 
Akili yako ina uelewa mdogo sana..tunachokataa kupangiwa masharti ya hovyo..wewe unajua wanachokifanya hawa wajinga?mbona wao wanavyopora rasimali barani Africa hilo huwa hawazungumzi?Tumepata Rais bora Magufuli ujinga wao wapeleke huko sasa wanatafuta vijisababu tu

Anapika data za uchumi hilo halina ubishi. Kama mlitarajia kupata sifa ili kuhadaa umma kwamba mambo ni mazuri, basi mjue hao IMF sio taasisi ya ccm. Hata ripoti ya CAG haionyeshi huu upuuzi unaotetea hapa.
 
Upuuzi mtupu.

Hakuna Taifa lililo huru kufanya uovu ndiyo maana kuna vyombo vya kimataifa ambavyo vipo kwaajili ya kutoa mwongozo, kushauri, kuonya na kudhibiti.

Kuna mambo ambayo kila Taifa lipo huru kuyafanya na yapo ambayo nchi haiwezi kuyafanya iwe dhidi ya wananchi wake au Taifa jingine.

Lakini serikali yetu ni mfano mbaya wa kuigwa. Inataka iwe huru lakini yenyewe haitaki watu wake wawe huru kwa mujibu wa katiba.
 
Nafikiri mwenye hicho kitabu ni Walter Rodney, kwa kukosea tu hapo nimeona haupo makini na huenda hata ulichokiandika hukijui.
Huyo huenda amesoma title tuu, hajui content na context.

Anaonekana ni kijana mdogo hajui effects za anachokiongea, mwalimu aliwahi kutuingiza kwenye ugomvi na mabwana wakubwa hawa, mashikamoo tunakumbuka folen za sukari, unga wa ngano, soda, bia na Hata chumvi n.k. hajui anachokisema na anafuata mkumbo wa ujinga!

Labda angemtafuta mkubwa wake amsimulie kilichojili wakati wa kufunga mkanda, na wakati wa kusonga mbele na kutokugeuka nyuma kuepuka kuwa jiwe la chumvi!!!
 
Hahaha sacarsm. Wataalam wetu toka report ya CAG itoke wamekaa kimya.
Naunga mkono hoja. IMF na World Bank wasitubabaishe. Wataalam wetu wetu wamethibitisha uchumi wetu unakua kwa 7% eti wao wanasema 4%. Hizo ni njama. JPM kaza Uzi hapo hapo. Waambie wakitaka kuchapisha basi waonyeshe uchumi unakua si chini ya 7%. Chini ya hapo usikubali.
 
Huyo huenda amesoma title tuu, hajui content na context.

Anaonekana ni kijana mdogo hajui effects za anachokiongea, mwalimu aliwahi kutuingiza kwenye ugomvi na mabwana wakubwa hawa, mashikamoo tunakumbuka folen za sukari, unga wa ngano, soda, bia na Hata chumvi n.k. hajui anachokisema na anafuata mkumbo wa ujinga!

Labda angemtafuta mkubwa wake amsimulie kilichijili wakati wa kufunga mkanda, na wakati wa kusonga mbele na kutokugeuka nyuma kuepuka kuwa jiwe la chumvi!!!
Na hajui kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya nchi inategemea mikopo na misaada. Huyu huyu anayempigia makofi alipoingia tu madarakani deni la taifa lilipanda toka trillion 30 - 49 ndani ya miaka 3 tu. Ndipo ajue kuna mambo hayaendi bila mikopo.
 
Back
Top Bottom