IMF kudhamini chanjo ya Corona kwa nchi masikini

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
IMF kudhamini fedha za chanjo ya corona kwa nchi maskini

Apr 06, 2021 12:54 UTC

[https://media]

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umesema kuwa una uwezo wa kudhamini asilimia 70 ya chanjo za COVID-19 zinazohitajiwa na nchi maskini na zenye kipato cha chini ifikapo mwaka 2022 iwapo hatua za dharura zitachukuliwa za kuongeza dola bilioni 44 katika mfuko huo wa kimataifa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, inatarajiwa kwamba, wakuu wa fedha wa nchi 20 zenye uchumi bora duniani maarufu kwa jina la G20 wiki hii wataunga mkono kuingizwa dola bilioni 650 katika hesabu ya "Haki Maalumu ya Kutoa Fedha" (SDR) ya IMF.

Hesabu ya SDR ya Mfuko wa Fedha za Kimataifa IMF ni ya fedha za kigeni inayotumiwa na IMF kutoa mikopo ya dharura.

Maafisa wa IMF na wataalamu mbalimbali wa fedha wanasema kuwa, gharama za chanjo na ustawi wa kiuchumi unatofautiana sana baina ya nchi za dunia.

[https://media]Mfuko wa Fedha Duniani IMF



Leo Jumanne taasisi binafsi ya fedha ya Rockefeller ya nchini Marekani imesambaza ripoti inayoonesha kuwa, nchi tajiri duniani zinaweza kutenga akiba zao mpya za fedha kwa ajili ya kupunguza pengo kubwa lililopo katika uchumi wa nchi za dunia na hivyo kuwezesha watu wengi zaidi kupigwa chanjo ya corona duniani. Iwapo hilo litatendeka, uchumi wa dunia utaweza kufufuka baada ya janga la corona na ugonjwa huo utaweza kudhibitiwa.

Ripoti ya taasisi hiyo imeashiria kuwa, ni kujidanganya kudhani kwamba kwa kuudhibiti ugonjwa wa corona katika baadhi ya nchi na kuzipuuza nchi nyingine kutaliondoa janga hili ambalo ni la dunia nzima na kusema kuwa, nchi zenye wastani wa asilimia 86 ya ustawi wa kiuchumi zilishajidhaminia chanjo ya COVID-19 mwishoni mwa mwezi Machi. Kinachotakiwa sasa ni nchi zilizoendelea kutenga kwa uchache dola bilioni 100 kwa ajili ya kuzidhaminia chanjo hizo nchi maskini duniani.

4by080bcae4d731uhjg_800C450.jpeg
 
Back
Top Bottom