IMF, Benki ya Dunia na nchi wafadhili haziwezi kukwepa lawama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IMF, Benki ya Dunia na nchi wafadhili haziwezi kukwepa lawama.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Mar 12, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa miongo miwili na nusu sasa, nchi yetu imekuwa ikitekeleza kile kinachoelezewa kuwa ni mabadiriko makubwa ya uchumi (structural adjustment), chini ya usimamizi wa mashirika ya fedha duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi yetu imekuwa ikipewa sifa nyingi na mashirika hayo kwa kutekeleza kikamilifu mabadiriko hayo kama ilivyo agizwa. Kwa bahati mbaya pongezi hizo haziambatani na tathmini inayoonyesha iwapo utekelezaji huo mzuri, umefanikiwaje katka kutufikisha katika malengo yaliyo kusudiwa. Tukianza na hii sera ya ubinafsishaji; utekelezaji wa sera hii uliendeshwa kifisadi. matokeo yake mali nyingi za umma zimeporwa. Mashirika hayo hayakutaka kuingilia kati kwa kuamini kwamba uporaji huo ungelisaidia katika kujenga tabaka la kati, ambalo ndilo lingeliibuka na kuwa muhimili wa uchumi wetu. Matokeo yamekuwa tofauti, kwasababu wengi wa waliofanikiwa kupata utajiri huo wamehamishia fedha hizo nchi za nje. Na hivyo ajira ambazo zilitegemewa kupatikana iwapo fedha hizo zingeliwekezwa hapa nchini hazikupatikana. Pili tutazame ili eneo la maboresho katika utumishi wa umma. katika eneo ili, ililengwa kuwa na watumishi wachache katika utumishi wa umma, wenye ari na weledi unaotakiwa katika kutoa huduma ya kiwango cha juu.Katika hali halisi hivi sasa huduma zinazotolewa na watumishi wa umma ni za kiwango cha chini sana kuliko ilivyokuwa. Aidha serikali imepanuliwa mno kiasi kwamba mapato yote ya serikali hayakidhi gharama za uendeshaji. Hii inatufanya wengi tujiulize, kama fedha zote za serikali zinaliwa na serikali yenyewe maendeleo ya nchi yatapatikanaje? Kwa haya machache inatosha kuonyesha jinsi hao wanaoitwa washirika wetu wa maendeleo wanavyo tuhadaha
   
Loading...