Imetosha sasa...ajali za barabarani TZ zinaua kuliko magonjwa yote ...hili serikali inalichukuliaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imetosha sasa...ajali za barabarani TZ zinaua kuliko magonjwa yote ...hili serikali inalichukuliaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nderingosha, Jan 15, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 2,998
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  • Wajameni....enough is enough sasa....mpaka pale wanapoondoka duniani ghafla wapendwa wa wengi kwa kupitia hizi ajali za barabarani ndipo watu tz hujiuliza kwanini inakuwa hivi!! watanzania na watawala siku zote sijui inakuwaje hazipatikani njia muafaka za kuzuia hizi ajali za barabarani??.
  • Kwa taarifa tu za kusikitisha ni kwamba ajali za barabarani tz(yaani road traffic accidents-RTA)zinaongoza kwa kusababisha vifo na ulemavu tz (number one cause of morbidity and mortality in tz).......ikimaanisha ajali za barabarani zinazidi hata maradhi yote yakiwekwa pamoja kwa kuongoza kusababisha vifo na ulemavu kwa raia....hili linafaamika kwa serikali.Ninachojiuliza siku zoote...je inakuwaje hatuoni serikali inapambana na hizi ajali za barabarani kwa kasi kama inayotumika kupambana na maradhi ya kuambukiza? (e.g HIV/AIDS,TB au malaria)na pia maradhi yasiyoambukiza?(e.g kisukari na magonjwa ya moyo).Nasema hivi kwasababu ni ukweli usiopingika kuwa hizi ajali hapa tz sasa zimekuwa nongwa na wanapotea raia na hata viongozi na wanasiasa........ajali haziangalii maskini wala tajiri......wala hazisubiri eti mtu atapatiwa huduma nje ya nchi.....ajali zinakata maisha fasta(kwa tajiri na maskini)na tumeona hata viongozi na wanasiasa wa chama tawala wakiathirika kwa hili(hata wenye ukimwi wana maisha marefu siku hizi)...na ningetegemea serikali wapambane na ajali za barabarani kama vile wanavyojitapa kupambana na adui maradhi hapa tz.Ukitaka kujua balaa la ajali za barabarani tz basi tembelea kwenye idara za upasuaji(surgery)kwenye mahospitali yetu.........nenda pale MOI au Tumbi hospital alafu ujionee mortality na morbidity cases.....utalia.....kwa kifupi tembelea hospitali za rufaa tz upite idara za upasuaji na mifupa uone balaa lililopo........kule kcmc moshi wagonjwa wa wodi za mifupa(orthopaedics)kuna wakati wanakosa hata vitanda wanalala chini kwa corridor...ulizeni...
  • Ifike mahali sasa haya mambo yawe historia tz kwani inawezekana.....iweje wenzetu nchi nyingine wameweza kupunguza ajali???huwa viongozi wanajifunza nini wanapotembelea nchi za wenzetu???,hivi kweli tz tumeshindwa kuweka camera barabarani za ku monitor speed??hawa traffic kazi yao nini tz?.
  • Tanzania nchi ya jabu sana sana,...ni tz pekee utaona watu wanaenda bar kulewa na magari yao....mh!tena woote...raia wa kawaida na hata viongozi....wanakwenda bar na magari yao wanalewa alafu baadae wanarudi na magari yao manyumbani...only in tz yaani....kwa wale tuliokaa nje ya nchi mnajua zero tolerance iliyopo kwa kuendesha ukiwa hata umeonja kileo(alcohol)...lakini tz hili linawezekana kwani ni sehemu ya maisha ya watu....nobody cares...kupata leseni ya udereva tz si deal..unaweza kuhonga tu hela ukapata leseni...huitaji hata kukaa darasani kujifunza gari kwa muda mrefu...tena unaweza hata kuendesha gari bila leseni tz..tumeona hata viongozi wakiua raia wakiwa hawana leseni au wamelewa.....haya yanaonekana ya kawaida tu kwani hata adhabu zenyewe mahakamani zina mashaka......kwa kifupi niseme tu tz watu wanaishi kwa kudra za mungu saaana......Nchi inapokosa umadhubuti kwenye sheria na utendaji.... things like these(RTAs)are a common occurance......tafakari....
   
 2. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,657
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mkuu huweziamini nipo kwenye basi ndio nato mizani ya dikese nimekutana na ajali ya gari sasa hivi,ukweli bora ya maradhi kuliko hizi ajali zinazotukuta sisi watanzania.gari iliyopata ajali ni toyota colora.mungu tusaidie hata trafi hakuna wamekaa barabarani wanachanga hela ya mboga tu.innakera.
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,209
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hapa JF tumepiga kelele weee kuhusu hizi ajali.......naona wahusika wameziba masikio..........ngoja nikaongeze hii kero ya ajali kwenye mada aliyoianzisha Mh Regia (RIP).........dahh
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ni kuchukua hatua wangekua wameshalimaliza tatizo kwani hili ni tatizo la siku nyingi sana
   
Loading...