The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Pasco lazima tuwe wakweli tu. CCM walishindwa ZNZ kwasababu nguvu kubwa iliekelezwa bara
Uchaguzi wa marudio CUF watashindwa tu, Nape aliposema kwa bao la mkono hakukosea
Vyombo vya dola vitatumika. Ikiwa Jecha peke yake alibebwa na kufuta matokeo akiwa hana mamlaka na serikali zote mbili zinajua hana mamlaka nini kitashindikana kwa Jecha kwenda kutangaza matokeo hata kama hakuna kura iliyopigwa?
Kinachotafutwa hapa ni kuhalalisha ushindi wa CCM lakini si uchaguzi
Maswali hayana majibu isipokuwa kauli moja tu 'tume imefuta'
Tuulize, kwa mamlaka gani tume imepewa kufuta matokeo ya Jumla
Matokeo yanayofutwa ni yapi ya Rais au Wabunge na Wawakilishi?
Je wapiga kura wa Rais wa JMT nao itakuwaje
Jamani tukubaliane ni uhuni tu wa kudhalilisha Taifa
Leo tutasimama wapi kuzungumzia demokrasia? Huko Burundi tusiende wala kwingineko
Tuondoe boriti kwenye macho yetu, ndipo tutafute vibanzi kwa wenzetu
CUF hawawezi kushinda, Nape Nnauye alisem a 'CCM itashinda hata kwa bao la mkono'
Safari hii matokeo yatatengenezwa kwanza na hayo ndio atakayopewa ayasome na baada ya hapo, thamani yake kwao ndio itakua imeisha. Busara kwake ilikua ajiuzulu tu.