Elections 2015 Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Kwai
Pasco, inaonekana ama hujui nini kimesababisha uchaguzi urudiwe ama unafanya makusudi. CUF wanajua kuwa uchaguzi ukirudiwa hawawezi kushinda. Bao la mkono walilofunga limekataliwa na mwamuzi na hivyo kuamuru mpira wa adhabu kuelekezwa kwenye lango la timu iliyopoga bao hilo la mkono.

CUF wanajua kuwa CCM itaelekeza nguvu zake zote kwenye uchaguzi huo na hivyo hakutakuwa na fursa tena ya bao jingine la mkono. Kinachogomba hapa si kwamba maalim seif alishinda ama la. Bali ni zile rafu walizocheza CUF mpaka wakajipatia ushindi rafu ambazo zilielezwa bayana na mwamuzi wa mchezo huo, Mzee Jecha

KWAIYO WALISHINDA,ILA USHINDI WAO ULIPATIKANA KWA kucheza rafu Una maanisha
 
Pasco, inaonekana ama hujui nini kimesababisha uchaguzi urudiwe ama unafanya makusudi. CUF wanajua kuwa uchaguzi ukirudiwa hawawezi kushinda. Bao la mkono walilofunga limekataliwa na mwamuzi na hivyo kuamuru mpira wa adhabu kuelekezwa kwenye lango la timu iliyopoga bao hilo la mkono.

CUF wanajua kuwa CCM itaelekeza nguvu zake zote kwenye uchaguzi huo na hivyo hakutakuwa na fursa tena ya bao jingine la mkono. Kinachogomba hapa si kwamba maalim seif alishinda ama la. Bali ni zile rafu walizocheza CUF mpaka wakajipatia ushindi rafu ambazo zilielezwa bayana na mwamuzi wa mchezo huo, Mzee Jecha
Tuonyeshe ki,bo gani lililamika rafu?

Pili, kwanini matokeo yalisitishwa kutangazwa wakati wa kuhesabu na si kukusanya

Kumbuka, majimboni matokeo yalibandikwa. Nini kilipelekea tume isisitishe kabla ya kuanza kuhesabu?

Tatu, Kwanini Jecha alitangaza matokeo mwenyewe wenzake wakiendelea kuhesabu?
 
Wenyewe hawataki kabisa kusikia ikosozi juu ya Zanzinar,

Kuwa makini Pasco

Pole Mzee ni ukweli mwingine mchungu huo.

Unanikumbusha 1972 Chief Buthelezi ikihutubia ukumbi wa Lumumba UDSM alimwambia Gora Ibrahim kuwa ili kufanikisha mapambano ni lazima wawe na watu wao ndani ya Afrika Kusini. Kupigania nje kunamnyima mtu kujua udhaifu wa adui. Sijui kama kuna watu ndani ya mgogoro huu wa Zanzibar wakutupa ukwe4li maana tungejua ukweli mikakati sahihi ingetumika
 
Kadawi Limbu ndio mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi? Msomi wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndio unakuja na story hiyo na authority yako ni Kadawi Limbu?

Kweli sheria imevamiwa!
 
Pasco lazima tuwe wakweli tu. CCM walishindwa ZNZ kwasababu nguvu kubwa iliekelezwa bara

Uchaguzi wa marudio CUF watashindwa tu, Nape aliposema kwa bao la mkono hakukosea

Vyombo vya dola vitatumika. Ikiwa Jecha peke yake alibebwa na kufuta matokeo akiwa hana mamlaka na serikali zote mbili zinajua hana mamlaka nini kitashindikana kwa Jecha kwenda kutangaza matokeo hata kama hakuna kura iliyopigwa?

Kinachotafutwa hapa ni kuhalalisha ushindi wa CCM lakini si uchaguzi

Maswali hayana majibu isipokuwa kauli moja tu 'tume imefuta'

Tuulize, kwa mamlaka gani tume imepewa kufuta matokeo ya Jumla

Matokeo yanayofutwa ni yapi ya Rais au Wabunge na Wawakilishi?

Je wapiga kura wa Rais wa JMT nao itakuwaje

Jamani tukubaliane ni uhuni tu wa kudhalilisha Taifa

Leo tutasimama wapi kuzungumzia demokrasia? Huko Burundi tusiende wala kwingineko

Tuondoe boriti kwenye macho yetu, ndipo tutafute vibanzi kwa wenzetu

CUF hawawezi kushinda, Nape Nnauye alisem a 'CCM itashinda hata kwa bao la mkono'
 
unashawishi cuf iingie kwenye uchaguzi wa marudio kwani ule wa kwanza walioshinda ulikuwa na matatizo gani ? , umeanza vizuri bali umemaliza vibaya sana , kama unaogopa kuandika ya limbu ulikuja kufanya nini hapa ?
 
Mzee Warioba naye kaliongelea hili si kwenye hilo kongamano la leo ?? Warioba kasema watu waache kulichukulia swala la Zanzibar kama ni swala la ccm au ukawa hili ni jambo la kitaifa na sio la kupuuzwa
Pia kasema hata kukiwa na tume huru ya namna gani kama hatuna maadili ya kitaifa ,hapa kazungumzia udini,ukanda,ukabila ,miiko ya uongozi ,tume huru haitosaidia chochote
 
Wanabodi, leo kuna msomi mmoja Bw. Kidawi Limbu, amethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, wa Chama cha Wananchi CUF ndie aliyeshinda uchaguzi wa rais wa Zanzibar, amewashangaa wasomi wana kigugumizi gani kuikemea CCM kutaka kulazimisha uchaguzi wa maudio ili waweze kupata ushindi wa bao la mkono!.

Msomi Kidawi Limbu amesema uthibitisho kuwa CUF ndio iliyoshinda, ni matokeo ya uchaguzi uliosimamiwa na NEC kule Zanzibar ambao uchaguzi haukuwa na dosari, katika uchaguzi huo, mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, alimgaagaza vibaya mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.

...
Pasco
Pasco Siku Seif Sharif alifanya mkutano hivi karibuni na waandishi wa habari alitoa idadi ya kura alizopata Lowassa na Magufuli. Pia laitoa idadi ya kura alizopata Shein na alizopata yeye. Fungua na usome document attached, WARAKA1.

Pitia uzi huu. Link Hali ya Kisiasa Zanzibar: Maalim Seif aongea na Vyombo vya Habari - Jan 11, 2016

Nimeipenda hoja yako. Upo sahihi. Niliuliza majuzi hapa jukwaani kama Pasco bado anajitambua! NI hatari sana kuwa na waandishi wa aina ya Pasco!
Kmuita Jecha mzee ni uhayawani, lile lafaa kuitwa jitu , kuwa na baba kama jecha ni fedheha kubwa duniani
Kama amethibitisha ameshinda basisiku hiyo ya uchaguzi ndio siku Maalim ataapishwa mnazi mmoja znz. Soku hio cuf na wazanzibari wote wataenda kumuapisha rais wa znz alie chaguliwa....ccm watakwenda kwenye uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wao siku hio..tena bila kuguswa lakini wazanzibari wao watAkua wamemwapisha rais halali
..

Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Kama Hiyo Ni Kauli Ya Msomi, Basi Napata SHAKA Na Wasomi Wetu, Hasa Ktk Kujenga Uhalali Wa UCHAGUZI Wa Marudio Na Kujaribu Kuwashawishi WATANZANIA, Wanachama, Wafuasi, Wapenzi Na Viongozi Wa CUF Wakubali Kuingia Ktk UCHAGUZI Huo!! HUKU Wakishindwa Kutoa Sababu Za UCHAGUZI Wa 25Oct 15 Na MATOKEO KUFUTWA!!!!!
 
Pasco, inaonekana ama hujui nini kimesababisha uchaguzi urudiwe ama unafanya makusudi. CUF wanajua kuwa uchaguzi ukirudiwa hawawezi kushinda. Bao la mkono walilofunga limekataliwa na mwamuzi na hivyo kuamuru mpira wa adhabu kuelekezwa kwenye lango la timu iliyopoga bao hilo la mkono.

CUF wanajua kuwa CCM itaelekeza nguvu zake zote kwenye uchaguzi huo na hivyo hakutakuwa na fursa tena ya bao jingine la mkono. Kinachogomba hapa si kwamba maalim seif alishinda ama la. Bali ni zile rafu walizocheza CUF mpaka wakajipatia ushindi rafu ambazo zilielezwa bayana na mwamuzi wa mchezo huo, Mzee Jecha
Eidha hujui au unafanya kusudi kujitoa chaji...
1. Sababu za kurudia uchaguzi azione Jecha peke yake..?
2. Chama gani kilijaza fomu ya malalamiko juu ya uchaguzi huo..??
3. Waangalizi wa kimataifa ilikuwaje waliona uchaguzi ulikiwa huru na wa haki..??
 
Wenyewe hawataki kabisa kusikia ikosozi juu ya Zanzinar,

Kuwa makini Pasco
Mkuu
Yericko Nyerere
, pole kwa yaliyokukuta, na asante kwa angalizo!. Nadhani wale jamaa zetu wanaangalia fb tuu, humu hawaangalii vingine wengi wetu yangetukuta siku nyingi!, ila pia nimenote uchangiaji wako wa mtindo wa aliyeumwa na nyoka!, na amini usiamini hicho ndicho walichokitaka!.

Po;e.

Pasco
 
Back
Top Bottom