Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi, leo kuna msomi mmoja Bw. Kidawi Limbu, amethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar wa 2015, kama usinge futwa, Maalim Seif Shariff Hamad, wa Chama cha Wananchi CUF ndie angelikuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Zanzibar.
Amewashangaa wasomi wana kigugumizi gani kuikemea ZEC kutaka kulazimisha uchaguzi wa maudio ili waweze kupata ushindi wa bao la mkono!.
Msomi Kidawi Limbu amesema uthibitisho kuwa CUF ndio iliyoshinda, ni matokeo ya uchaguzi wa urais wa JMT, uliosimamiwa na NEC kule Zanzibar ambao uchaguzi haukuwa na dosari, katika uchaguzi huo, mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, alimgaagaza vibaya mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.
Kwa vile wapiga kura ni wale wale, na chama cha wananchi CUF, kilikuwa ni msharika katika UKAWA, haiwezekani wapiga kura wale wale, wamchague mgombea wa UKAWA kwenye urais wa Muungano na kumpiga chini mgombea wa CCM, halafu wapiga kura hao hao, wakaja kumpigia kura mgombea wa CCM, kwenye uchaguzi wa Zanzibar, hivyo amethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar, CUF ilishinda, Maalim Seif Shariff Hamad, ndie angepaswa kuwa rais halali wa Zanzibar kwa mujibu wa uchaguzi wa October 25, 2015, ila hakutangazwa baada ya matokeo halali kubatilishwa kinyume cha sheria!.
Matokeo Rasmi ya uchaguzi ya Urais wa Zanzibar ambayo yanaonyesha wazi kuwa CCM imeshindwa kwa kura nyingi kwa kiwango na uzoefu wa Zanzibar, hata kura za Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa upande wa Zanzibar zinaonyesha hivyo hivyo na kwa hiyo kuthibitisha kuwa CCM ilipoteza uchaguzi huo. Kwa muhtasari matokeo ya Urais wa Muungano kwa upande wa Zanzibar ni kama yafuatavyo:
MGOMBEA KURA HALALI ASILIMIA
DR. JOHN POMBE MAGUFULI 194,317 46.5%
EDWARD NGOYAYE LOWASSA 211,033 50.50%
IDADI YA KURA HALALI 417,882
Matokeo ya kura za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani yote yanaonyesha CCM imeshindwa kwa idadi ya kura za walio wengi (popular votes). CCM imeweza kupata viti sawa na CUF katika uwakilishi na ubunge kwa sababu ya mbinu zilizotumika katika ukataji wa majimbo.
Maadam tarehe ya uchaguzi wa marudio imeishatangazwa , na kama ni kweli Maalim Seif Shariff Hamad, alishinda kihalali, kuna ubaya gani kama CUF watashiriki tena uchaguzi huu wa marudio ili washinde tena. ila wanapaswa kuwa makini sana na bao la mkono, hivyo kama Maalim Seif Shariff Hamad, alishinda kihalali bila mbinu zozote, hata uchaguzi ukirudiwa mara 100, bado atashinda!, sasa ni nini kinachowatia CUF kigugumizi kuhusu kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio?.
Source: Nimemsikia mwenyewe kwa masikio yangu!.
My Take
Kama mtu kama huyu ni kweli alishinda uchaguzi wa 2015, then there is a possibility alikuwa anashinda chaguzi zote za nyuma, but matokeo yanapinduliwa, hivyo kilichotokea 2015 was a mistake, ikabidi uchaguzi ufutwe!, then this means the game of 2020 must be planned very careful never to repeat the same mistakes again!.
Kwangu kitu muhimu sio, mtu kushinda na matokeo kupinduliwa, this is an action, kitu muhimu zaidi ni the motives behind, the reasons za kwanini ashinde asipewe hadi uchaguzi ufutwe!. This means Zanzibar ni lazima CCM ishinde.
Kama watu wa Maalim Seif wana akili timamu, they have to find out the reasons na kuhakikisha zimeondolewa, kabla ya kuingia tena kwenye uchaguzi wa 2020!.
Vinginevyo, kama Maalim Seif ataingia tena uchaguzi wa 2020 kichwa kichwa, bila kuzijua sababu, akitegemea this time atapewa, huku kutakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu!.
Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2020, tutakumbushana.
Paskali