Imethibitika sasa Corona iko mitaani Dar. Napata shaka kwanini Serikali sasa wako Dodoma ghafla hivi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Makonda kasema mtoto wa Mbowe anaumwa Corona. Katika hili katoa siri ya Serikali ambao wahusika wa kutangaza ni Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya.

Mbowe kakiri na kusema mwanaye kaipata Dar na sio nje ya nchi.

Wakati huo huo serikali na Rais wamehama Dar na wako Dodoma.

Mara namsikia Makonda anatangaza kupuliza dawa mitaani.

Kwa sasa watanzania tuwe macho Corona iko mitaani Dar na itaenda mikoani soon
FB_IMG_1585108093252.jpg
 
Makonda karopoka bila kujua ametoa siri, Corona ipo mitaani Dsm, ndio maana Rais akaenda kujificha kwenye mawe Dodoma, matokeo yake uropokaji wa Makonda unaleta tension kwa wakazi wa Dsm, wakati lengo la serikali lilikuwa watu wasijue kama Corona ipo mitaani Dsm.

Kutafuta sifa za kijinga kumemuaibisha na kuwaaibisha wote waliohusika kutoa taarifa za mtoto wa Mbowe, na Mbowe nae kamalizia kwa msumari mtoto wake hajatoka nje ya nchi mwaka mzima, kwahiyo kaipatia humu humu ndani, sasa kazi ipo kwa wakazi wa Dsm kujihakikishia usalama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatarioz....iko Dar na takwimu zao za maambukizi zinatia shaka. Halafu mtoto wa baba, anapiga kampeni danganyifu..

badala ya kuhimiza kujikinga na nini cha kufanya endapo utahisi una maambukizi. Eti atapuliza dawa, anafikiri hii ni malaria, dengue au kipindupindu?

Everyday is Saturday :cool:
 
Back
Top Bottom