Utawala wa kidhalimu unaendelea kuvuruga uchumi, hii miaka 5 itakuwa worse sana kwa Wadanganyika wote.
Baada ya miaka mitano mkiona kiwanda kinapiga kazi mnatafuta jingine la kuchomekea..mtajipa matumaini sana.
 
Pamoja na kuwa Mimi si muumini wa siasa za CCM.....Lakini siwezi kufurahia habari ambayo itapelekea angamizo la watu waliokuwa maisha Yao yanategemea hapo.......

Ni mambo ambayo kwa namna moja au nyingine hayawezi kuleta athari kwa watawala wala vibaraka wao zaidi ya wananchi wanyonge......
 
Baada ya miaka mitano mkiona kiwanda kinapiga kazi mnatafuta jingine la kuchomekea..mtajipa matumaini sana.
We mfia chama wa Lumumba, hivi hujui kama uchumi wa Tanzania unazidi kupalaganyika siku hadi siku? Hujasikia habari za biashara lukuki kufungwa? Hujasikia Hotel Ngurdoto kugeuka Hostel ya wanachuo? Kitimoto we!
 
Hii nchi inazidi kutumbukia shimoni, jana Ngurdoto Hotel imekuwa hostel, leo Dangote anafungasha, sijui kesho itakuwa zamu ya nani..

Hakika watanzania tufunge mikanda, nchi imepatwa.
Kesho zamu ya ManiFongo
 
Dahhh, sasa tutegemee bei ya Cement kupanda maradufu. maana huyu ndie alitegemewa kuongeza uzalishaji hatimaye bei kushuka sana
 
Huwa unakurupuka sana, hiyo habari hata hujaisoma na kuelewa, nakuelewesha

Nsk oil, walipewa tenda ya ku supply mafuta kwenda dangote, wakachukua mkopo kutoka standard chartered kufanya hiyo kazi (overdraft) baadae Nsk na dangote hawakuelewana hivyo hakukuwa na malipo, nsk kashindwa kulipa mkopo standard chartered akawapeleka mahakamani wote.

Kesi ikiwa inaendelea NSK kapeleka maombi mahakamani kwa ajili ya kuwind up dangote mali zake ziuzwe alipwe hela yake, maombi yamekataliwa kwa kuwa kuna kesi inaendelea
 
Kumbe??? ngoja nirudi nikasome tena lugha ya sheria ni ngumu kutafuna
1607015814052.png
 
Mahakama Kuu imezuia kufungwa kwa Kiwanda cha Dangote Cement Limited ambacho mdeni wake aliomba kifungwe

Kampuni ya NSK Oil and Gas Limited ilitaka Kiwanda cha Dangote kifungwe kwa kushindwa kumlipa Tsh bilioni 5.8

Mei 2018, Dangote na NSK Oil walikubaliana kuwa kampuni ya NSK impelekee mafuta Dangote. NSK alichukua mkopo wa Tsh 11.1 bilioni Standard Chartered Bank kama mtaji wa kufanya kazi hiyo

Dangote alidaiwa kushindwa kulipa kama walivyokubaliana, hali iliyofanya Standard Chartered kuwashtaki ili walipe deni la Tsh 5.8 bilioni. Ambapo NSK aliiomba mahakama ifunge Kiwanda cha Dangote

Dangote akaomba kisifungwe kwa kutumia Ibara ya 283 ya Sheria ya Kampuni ya 2002 ambayo inaruhusu kampuni kuomba kuzuia kufungwa muda wowote kabla amri ya kufungwa haijatoka
===
Dar es Salaam. The High Court has blocked proceedings for winding up of Dangote Cement Limited instituted by NSK Oil and Gas Limited pending determination of a Sh5.8 billion suit Standard Chartered Bank has filed against the two companies.

NSK, suppliers of oil products, lubricants, and liquefied petroleum gas (LPG) has filed at the commercial division of the High Court a petition for the winding up of the cement producer over inability to settle a Sh5.8 billion debt.

The petition prompted Dangote to file an application at the same court in which it sought orders to halt the move pending determination of the case Standard Chartered has filed against them over an unsettled Sh5.8 billion overdraft facility.

Dangote then asked the court to halt the winding up proceedings including publication of the petition for winding up, arguing that the petition was premature and was filed in bad faith.

The company further argued that publication of the petition for its winding up would cause them irreparable reputational damage.

The dispute arose from an agreement Dangote entered with NSK Oil in May 2018 for the later to supply the former with fuel.


To facilitate smooth supply of the fuel, NSK Oil secure and obtained an overdraft to a limit of Sh11.1 billion from Standard Chartered Bank as a working capital.

As a security for the loan, NSK Oil assigned its debt in the performance of the agreement to the bank by a notice of assignment signed by both parties in the deal.

However, things did not go well between the bank, on one side, and Dangote and NSK Oil, on the other. Dangote allegedly failed to pay some money as agreed, forcing Standard Chartered bank to sue them to recover Sh5.8 billion debt.

While the Standard Chartered suit was pending in the commercial court, NSK Oil filed a winding up petition against Dangote over inability to pay Sh5.8 billion.

Dangote reacted immediately by filing an application at the same court, pleading with the court to stop the winding up petition because it has a direct bearing to a case Standard Chartered had sued them.

“…this petition is intended to threaten the applicant (Dangote) and was filed with mala fide intended to embarrass, ridicule, and inflict irreparable reputational damage to the applicant. “Entertaining the winding up petition will be tantamount to turning this court into debt collection agent,” argued lawyer for Dangote,” argued Dangote through its lawyer.

NSK Oil strongly opposed the application, saying the case Standard Chartered had filed against them had no bearing with the winding up petition

In his recent decision, High Court Judge Stephen Magoiga said Dangote was justified to defend her interests by opposing the winding up process.

“I am of the strong considered opinion the this winding up petition has a strong bearing to the Commercial Case No. 7 of 2020 ( the case Standard Chartered Bank is suing Dangote and NSK Oil, hence, the call to restrain is justifiable,” said the judge.

Section 283 of the Companies Act, 2002 allows a company or creditor to apply for orders to stop winding up petition at any time before winding up order has been made.

“The winding up of a company amounts to legally killing and burying of the company and our parliament in its wisdom by incorporating the provision of section 283 of the Companies Act was meant to protect the process where the circumstances are so demanding. In this application, I find this is one of the fit cases for this court to exercise its discretion,” said the judge.
 
Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuwekeza biashara katika utawala wa kijinga namna hii. Cement kwasasa hainunuliki.
 
Pamoja na uwepo wa mada inayohusu kufungwa kwa kampuni ya Dangote hapa nchini iliyoletwa na Mkuu Return Of Undertaker, naomba Moderators muuache Uzi huu kwa maslahi ya mjadala na uelewa.

Kichwa pamoja na maudhui ya uzi wa mtajwa hapo juu ni kuleta habari na kutaka kuaminisha umma kuwa Dangote anataka kufunga kampuni yake kule Mtwara na kuondoa uwekezaji wake hapa Tanzania. Katika kuonesha ukweli huo kumeambatishwa habari ya gazeti la the Citizen la leo.

Kwa msomaji makini ataona na kujua kuwa Dangote ndiye anayepinga kufungwa kwa kampuni yake hapa nchini. Hivyobasi, hana nia ya kuifunga na kuondoka. Yeye ndiye aliyepinga na kufanikiwa kuzuia shauri la kufungwa kwa kampuni yake.

Iko hivi kwenye habari hiyo: Kampuni ya Dangote, kama kampuni nyinginezo, iliingia mkataba wa kuletewa fuel na kampuni ya NSK. Katika kufanikisha hilo, kampuni ya NSK ikachukua mkopo kama mtaji kutoka benki ya Standard Chartered wa bilioni 11.1.

Baada ya kushindikana kulipwa kwa mkopo huo, Standard Chartered ikawashtaki NSK na Dangote. Kufuatia shauri hilo, na katika hali ya kujitetea, NSK akapeleka shauri la kufungwa (winding up) kwa kampuni ya Dangote kwa kushindwa kulipa deni lake kwa kampuni hiyo.

Naye Dangote akawasilisha Mahakamani hapohapo Ombi dogo la kusitisha kwa muda shauri la kufungwa kwa kampuni yake. Ombi lake dogo Dangote ndilo lililotolewa uamuzi kwa kusitisha shauri la kufungwa kwa kampuni yake. Ndiyo kusema, Dangote amefanikiwa kwenye maombi yake.

Kwa kifupi, Dangote ndiye anayepinga kufungwa kwa kampuni yake pamoja na deni linalodaiwa kuwepo dhidi ya kampuni ya NSK. Kwenye mashauri hayo yaliyoripotiwa na the Citizen hakuna mahali Dangote na kampuni yake wameonyesha nia ya kufungwa kwa kampuni hiyo na kuondoka nchini.

Ni vyema kusoma habari kwa makini kabla ya kuandika uelewa ambao wakati mwingine waweza kubeba picha ya kupotosha umma. Dangote ndiye aliyepinga kwa nguvu zake zote kufungwa kwa kampuni yake kwenye mashauri matatu yaliyopo Mahakama Kuu yakihusika kampuni yake, kampuni ya NSK na benki ya Standard Chartered.
Hao ndo huwa wanajinasibu wanajua lugha ya malkia, kumbr ni mbwembwe tu.
Mtu ukiishi kwa unafiki hata kuchukua umakini huwezi.
Wao walivyoon kufunga tayari mtu anakimbia kuandika danagoye nafunga kiwanda hata bila kusoma kwa umakini,
Wachawi utawajua tu kwa tabia zao, lakini nchi itaenda tu.
 
Kwa kiasi kikubwa siasa imepunguza uwezo wa akili za vijana wengi kuchambua na kuchanganua mambo mbali ya kimsingi hata yanayohitaji fikra ndogo.........

Hali hiyo imepelekea jukwaa la siasa kuwa kijiwe cha matusi ya nguoni na kuvunjiana heshima badala ya kujadiliana kwa hoja nzito zenye kujenga!!.....

Imekuwa jambo la kawaida mtu anapoona habari inayoenda kinyume na matakwa ya hisia zake kumwaga matusi ya nguoni na kila aina ya lugha chafu........

Nadhani Tanzania tutakuwa na aina yetu ya siasa......Maana sijapatapo kuona wanaharakati nguli wakitumia lugha za matusi kwenye kudai haki zaidi ya hoja zenye nguvu........
 
Back
Top Bottom