Imeniuma sana, mpenzi wangu hanipi hata senti wakati mimi namsaidia sana

Feb 7, 2017
11
26
Habari zenu,

Mwenzenu nina mpenzi ambaye asilimia kubwa mimi ndo msaada kwake, cha ajabu kapokea mshahara hata kunipa elfu kumi hajanipa nilienda kulala kwake hata kusema nauli hii hapa hakuna na ukizingatia ni mume mtarajiwa halafu huku ananisumbua nimzalie mtoto.

Yani kila kitu ni kumuelekeza kama mtoto mdogo jana ikabidi nimwambie ukweli maana aliniletea itikadi za kusema oooh kuna mtu ananitaka ana hela ikabidi nimwambie ukweli kuwa nenda kwa haohao watakaokupa hela leo ndo anajifanya kukiri kakosea alichokifanya si sahihi.

Jamani kaka zangu watunzeni wake zenu msije mkachapiwa bure.

Nawasilisha
 
Habari zenu,

mwenzenu nina mpenzi ambaye asilimia kubwa mimi ndo msaada kwake, cha ajabu kapokea mshahara hata kunipa elfu kumi ajanipa nilienda kulala kwake ata kusema nauli hii hapa hakuna na ukizingatia ni mume mtarajiwa halafu huku ananisumbua nimzalie mtoto... yani kila kitu ni kumuelekeza kama mtoto mdogo jana ikabidi nimwambie ukweli mana aliniletea itikadi za kusema oooh kuna mtu aninitaka ana ela ikabidi nimwambie ukweli kuwa nenda kwa haohao watakao kupa ela....leo ndo anajifanya kukiri kakosea alichokifanya si sahihi

jamani kaka zangu watunzeni wake zenu msije mkachapiwa bure.....

nawasilisha

kuna tatizo hapa........kubwa kidogo......
 
Umemuonjesha tamu ya Bure sijui ulikua na kiu ya bwana,manake sio kwa kumdekeza hivyo,naelewa unaweza kumpa mpenzi wako lakini kupeyana ni kikoa toa na wewe upewe,lakini yeye amekua kama majini ya sikuizi,mara pete,mara mbuzi,mara kidani, kwanza unajisikiaje kutoa tuuuuuuuuuuu kumhonga baba zima unanunua service yake? na haitoshi na kukwambia pumba juu eti kuna mtu ananitaka atakiwe kwa lipi? au anatakiwa akahudumiwe na mwengine kwako pesa haitoshi? Wallah hata sijui Tafran hizi mnaziokotea wapi mwambie aende asije akachelewa akuwache upate mwenye kheir na wewe..
 
Habari zenu,

mwenzenu nina mpenzi ambaye asilimia kubwa mimi ndo msaada kwake, cha ajabu kapokea mshahara hata kunipa elfu kumi ajanipa nilienda kulala kwake ata kusema nauli hii hapa hakuna na ukizingatia ni mume mtarajiwa halafu huku ananisumbua nimzalie mtoto... yani kila kitu ni kumuelekeza kama mtoto mdogo jana ikabidi nimwambie ukweli mana aliniletea itikadi za kusema oooh kuna mtu aninitaka ana ela ikabidi nimwambie ukweli kuwa nenda kwa haohao watakao kupa ela....leo ndo anajifanya kukiri kakosea alichokifanya si sahihi

jamani kaka zangu watunzeni wake zenu msije mkachapiwa bure.....

nawasilisha
una miaka mingapi ya kuzaliwa maana ulivyoandika hapa!!!!!!!!!!!!
 
Mapenzi haya endi hivo mkuu! Hususani kwa mtu mwenye malengo na ww sizani kama anaweza kukufanyia hivo, hivo ni viishara tu kuwa wewe atakutumia tu na sio akuchukulie kama wife CHAMSINGI ACHANA NAE kama kweli alikua anania ya kukufanya mke, utaona juhudi zake kuludisha penzi lako.
 
Mvumilie tu,ila usikae kimya bila kumwambia ukweli kuwa unahitaji nini akufanyie kwani si wanaume wote wanaojiongeza juu ya kuwahudumia wapenzi wao.Mwambie unahitaji nn na hupendi jambo gani.
 
Back
Top Bottom