Imekuwaje Meya wa Kinondoni awasikilize CHADEMA na kufuata Madiwani wake...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imekuwaje Meya wa Kinondoni awasikilize CHADEMA na kufuata Madiwani wake...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chibhitoke, Mar 31, 2011.

 1. c

  chibhitoke Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama hakika nguvu za CHADEMA zinanatisha, sasa imedhihirika kuwa CHADEMA ndicho chama kinachoongoza kanseli ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni badala ya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho kilichopewa ridhaa ya kuiongoza na wananchi wa Wilaya ya Kinondoni.

  Licha ya CHADEMA kuwa na jumla ya viti 17 ndani ya Kanseli (Council) dhidi ya viti zaidi ya 25 vya CCM, lakini CHADEMA ndicho kimekuwa kikiendesha Kanseli kwa maana ya kutawala hoja, kutoa maamuzi mbalimbali na hata kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa watumishi wa Halmashauri ya Kinondoni. Na mara nyingi maelekezo ya CHADEMA yamekuwa tofauti na maelekezo ya mwajiri wao ambaye ni TAMISEMI.

  Ingawa CCM ndio yenye viti vingi zaidi kwenye Kanseli, na pia ndio waliotoa Meya na Naibu Meya wa lakini CHADEMA kimewazidi kabisa nguvu madiwani wa CCM kiasi kwamba mustakabali wa manispaa hiyo umo mikononi mwa CHADEMA. CHADEMA wamekuwa wakitawala vikao vya Kanseli, wao ndio wamekuwa wakizungumza zaidi tena kwa mamlakamakubwa na maamuzi yao ndio ambayo yamekuwa yakiheshimiwa na kufanyiwa kazi licha ya kuwa wao ni wachache na sio wanaongoza kanseli.

  Mwanya wa kufanya hivyo wameupata kutokana na Meya Mstahiki Yusuph Mwenda Kutumikia maslahi ya CHADEMA kuliko maslahi ya Chama chake. Madiwani wa CHADEMA wamekuwa kila mara wakishutumu maamuzi, utendaji , na mipango iliyokuwa imepitishwa na Kanseli ambayo kimsingi ilikuwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Pia Madiwani hao wamekuwa wakiponda uanzishwaji na utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kanseli. Wamekuwa pia wakiwatukana na kuwaponda watumishi wa Manispaa na kuwaita kuwa ni wezi tu.

  Watumishi wanapomueleza Mkurugenzi wa Manispaa kuwa CHADEMA na Meya wamekuwa wanawaita wao wezi na ‘’incompetent’, Mkurugenzi huyo amekuwa akijibu wamuache yeye apumzike maana ana mwezi mmoja tu kabla ya kustaafu.
  Jambo la kushangaza ni kuwa , Meya badala ya kuungana na watumishi wa manispaa na madiwani wa CCM kutetea miradi hiyo kwa kuwa ilikuwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, yeye hugeuka na kusema watumishi wote wa Manispaa hawafai kabisa.

  Katika hali ya kustajaabisha kabisa katika kikao wiki iliyopita, alisema inabidi watumishi wote wahamamishiwe huko Makete kauli ambayo iliungwa mkono na madiwani wa ChADEMA. Sasa Meya ambaye anatoka kwenye Chama dola ambacho ndicho kinaoongoza serikali iliyowaajiri wafanyakazi hao anapoungana na CHADEMA kuwanyanyasa waende kwa nani?. Madiwani wa CCM wamekuwa waoga ‘’kumvaa’’ Meya kwa vile inasadikiwa aliwekwa hapo na kigogo mmoja’’ mzito’’ sana ndani ya Chama na serikali, hivyo wanadai ukicheza vibaya na huyo Meya unaweza kuingia matatizo. Hivyo njia rahisi ni kuacha mambo yaendelee kama ilivyo ili CHADEMA waendelee kuongoza halmashauri hadi chama chenyew kitaposhtuka.

  Suala ambalo Meya hajatambua ni kuwa CHADEMA wapo pale kuwakilisha maslahi ya chama chao kwa hiyo wanatafuta kila aina ya kasoro kwenye utendaji ili wanapoenda kwenye maandamano yao wapate uongo wa kukiponda Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo Meya anapoungana na CHADEMA kuponda mipango, utekelezaji wa miradi na watumishi wa Manispaa anakuwa anawasaidia zaidi CHADEMA katika ajenda yao ya kutaka kuipaka matope serikali ya Chama cha Mapinduzi.

  Madiwani wa CCM wamekuwa kimya kabisa(wamenywea) wanasema ndo ambayo chama chao walitaka kwa kumpitisha Meya ambaye amejaa majivuno na majigambo ya kisomi lakini anashindwa kabisa kusimamia na kuendesha vikao vya kanseli kiasi cha kufikia vikao hivyo kuwa kama vikao vya harusi pale Katumba Bar. Uliwahi kuona wapi kikao cha Kanseli madiwani wanne wanasimama na kuongea kwa wakati mmoja, au diwani mmoja hajamaliza kuzungumza mwingine kisha simama na kuanza kuzungumza.

  Na wanaofanya hivyo ni madiwani wa CHADEMA, Meya badala ya kutunza nidhamu ya kikao yeye huonekana kutikisa kichwa na kufurahia hizo vurugu za CHADEMA. Hajui kuwa madiwani wa CHADEMA pia wanakabiliwa na ‘’ulena’’ wa kushiriki vikao kama vya kanseli. Wao wamezoea vikao vyao ambavyo wakishavaa yale magwanda yao basi ni vurugu tupu. Unaweza hata kumtia mwenzio kidole kwenye macho kwao hiyo haina shida, sasa ndo wanataka kuleta mtindo huu hata kwenye vikao vya Kanseli. Meya lazima awe thabiti na kusema hapana, vikao vina utaratibu wake na oda zake ambazo ni lazima zifuatwe.

  Bahati mbaya Meya mwenyewe naye inaonyesha hajui utaratibu wa vikao, yeye naye labda amezoea vikao vya timu za Veterani pale Rose Garden. Hivi Hakuna semina elekezi za Madwani na Mameya kama zile za Wabunge?
  Kutokana na rabsha hizo za Chadema na ulegevu wa Meya hivi sasa Wakuu wa Idara wamekuwa waoga kufanya maamuzi. Utekelezwaji wa miradi umesimama, watu wanasema tusubiri Meya na CHADEMA wake waje wafanye kazi. Sababu ni kuwa Meya amekuwa akiwadharau wafanyakazi na kuwaaambia kuwa’’ watu tuna shule zetu bwana kama kazi hamuwezi tutakuja tufanye wenyewe”.

  Kila akikutana na mfanyakazi swali la kwanza kuuliza ‘’ una elimu kiwango gani”. Kutokana na manyanyaso hayo ya Meya na usongo wa CHADEMA wa kupinga kila jambo ili kukiharibia CCM, sasa hivi sasa kazi zote zimesimama.
  Hii ni Hatari kwa CCM kwasababu kama Chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza hakifanyi hivyo na kimegawa ‘’uzaliwa wake wa kwanza’’ kwa CHADEMA maaana yake ni kuwa wamewasaliti wananchi waliowachagua . Pia kutotekelezwa kwa miradi maana yake ni CCM kujichimbia kaburi maana kinashindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi .

  Swali kubwa ni kuwa je kitendo cha Meya kuungana na CHADEMA kuvunja moyo watumishi wa Manispaa na hata madiwani wenzie; je anajua athari zake kwa Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya kupoteza imani kwa wananchi?
  Mimi nashauri Chama cha Mapinduzi kifanye utafiti mdogo tu, na kitabaini mambo hayo. Chama kichukue hatua ya kuchukua uongozi wa Kanseli toka mikononi mwa CHADEMA na watumishi warudishiwe kujiamini ili utendaji urejee kwenye kiwango chake na wananchi waweze kutimiziwa yale ambayo Rais wao aliwaahidi wakati wa kampeni katika vipindi vyote viwili.

  SOURCE: Waraka wa Siri ulionaswa ukijiandaa kwenda CCM (Kinondoni)
   
 2. markach

  markach Senior Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Acha kulalamikia cdm, kwa hiyo unataka watu wafanye kazi kwa mazoea eti? Hakuna kula kula ovyo, kila kona cdm wanakodoa macho, kama umeshindwa kazi nafuu uende makete huko. Hiyo ndio peoples power. Cdm fanyeni kazi mliotumwa na wananchi
   
 3. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nchi hii ni yetu sote, sasa hapa unataka kusema kuwa CHADEMA wao siyo watulivu na hawajui jinsi vikao vya council vinavyooendeshwa? Acha utahira, wewe nadhani ni mtumidhi pale Kinondoni sasa tunajua kila kichokuwa kikiendelea pale, nilisoma ile socio econominc profile ya 2009/2010 ya hapo kinondoni, tulijua kilichokuwa kikiendelea,sasa utendaji ulikuwa si wa kuridhisha wewe unataka mambo yaende kama huko nyuma. Ndg ngoja mambo yabadilike ili wananchi wapate maendeleo. Acha Ushabiki usiyokuwa wa lazima Mkuu.
   
 4. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa ulilonalo wewe uliyeleta hii mada either ni mfanyakazi wa manispaa au diwani wa CCM ni ufisadi uliokujaa na hivyo unaona Meya wa sasa ambaye yuko independent maana si mla rushwa wala fisadi hivyo he don't buy into your fisadi deals mnaona anawawekea kiwingu.Na kwa taarifa yako nimepata kuongea naye ana kwa ana na akaniaeleza jinsi inavyomuwia vigumu ku-push mambo ya maendeleo katika baraza kwasababu madiwani wengi hasa nyinyi wa CCM mlitumia pesa nyingi katika kampeni na mna matarajio makubwa ya kufaidika kwa kuwa madiwani badala ya kuweka maslahi ya nchi na ya wakazi wa dar mbele. Najua lazima inawauma kwani Meya Mwenda si kama Londa aliyekuwa anashinda ofisi za Manispaa na kukimbiza files kama mtendaji wa kawaida.Jamani mirija yenu ya ufisadi ikizibwa mnaanza fitina? kama kuna mtu anaweza kufuatilia ukweli wa hoja za huyu aliyeleta hii taarifa atagundua namna nchi hii inavyowapiga vita wazalendo na kwa kuwa Chadema wanawakilisha maslahi ya umma basi Meya anaonekana yuko upande mmoja nao kwasababu naye anaimba wimbo unaofanana nao.Issue si semina elekezi bali ni CCM na wabunge na madiwani wao kufundishwa somo la Uzalendo hilo ndiyo muhimu ili wazaliwe akina Yusuph Mwenda wengi ndani ya chama.
   
 5. M

  Mzalendoo Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa mwalalamika nin? Acheni hizo,ktk dunia ya sasa hatupashwi kufanya maamuz kw kuangalia idadi,hvyo naona huyo meya ana akil timamu sabab anasikilza hoja na sio wingi wa watu, safi sana.zibeni mirija yote ya rushwa.
   
 6. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  waraka huu ni wakada wa ccm.analalamika mabadiliko ambay hajatambua na kuamin kwamb yametokea.bado yuko na normal path.pole yake
   
 7. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  waraka huu ni wakada wa ccm.analalamika mabadiliko ambay hajatambua na kuyaamin kwamb yametokea.bado yuko na normal path.pole yake
   
 8. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kama madiwani wa ccm hawana hoja wataongea nini? Yawezeka wanamuogopa kwa cv ilivyo maana na sikia an cpa, mba,na ni mwana sheria
   
 9. g

  gepema Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sasa tunataka tuone kazi hata kwenye ofc za serikali maana si mambo mliyoyazoea. Unamsikia mtu anataka akafanye kazi serikalini ili apate muda wa kufanya mambo yake binafsi!
   
 10. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  unalalmika sana, yawezekana na wewe ni diwani mmoja wapo au ni mtumishi wa halimashauri ambaye unahofia kwenda Makete.

  Ungetumia neno baraza, badala ya kanseli....ushauri tu.
   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  aaahaaaaaa...oohoo!,ama kweli,maskini CCM walizoea kudekezwa,wakazoe siasa laini ...ole wao!
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  kazi mbona haijaanza bado?
   
 13. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Wewe ni diwani au Mkuu wa Idara hapo kino sasa unaona maslahi yenu yamebanwa unakuja kulia lia hapa JF....utakiona cha moto hamtauza tena viwanja vya wazi....
   
 14. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii nchi kila kitu siasa tu,kwani kuna ubaya gani meya wa ccm kukubaliana kihoja na madiwani wa cdm??

  Tuongelee hoja, na kama hoja ipo kwa maslahi ya wananchi basi hicho ndio raia walichowatuma viongozi wake wakayafanye.

  Muacheni meya afanye kazi yake,waacheni madiwani wafanye kazi zao! Tuwahukumu kwa makosa ya msingi. Tupende amani ya kweli
   
 15. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukisoma kwa makini utaona huu ni uzushi mtupu,umbea,unafiki,wivu,majungu na uchochezi tu. Hamna nyaraka za pumba wala siri hapa,tusidanganyane. Haya ni mashairi kama ya taarab.

  Unaweka hoja zako binafsi kabisa kwa chuki yako na meya sie tujadili kweli? Ok,angalia umesema Meya
  -amewekwa na kigogo
  -vikao vyake vya maveteran rose garden
  -vikao vya harusi katumba
  -anajigamba amesoma

  Unatuonyesha hivi ndio vitu ccm mnajadili kwenye vikao vyenu ama? Mnajadili majungu?? Kweli?

  Tafadhali,najua utakuwa umeguswa kimaslahi zaidi ndio maana una huu uchungu wa uongo kupitia mgongo wa ccm. Kama ni kiwanja cha wazi umekikosa basi pole. Ila usilete hoja zisizo na tija..labda ungeweka kwenye forum ya macelebrity or something else
   
 16. S

  Songasonga Senior Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I love this boy hurraaah Mayor endelea kuchApa kazi tunataka kuona tofauti Kati yako na Londa
   
 17. c

  chibhitoke Member

  #17
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA mbona mna ''double standards'' sana? Shibuda alipojiunga na CCM kuwaponda wabunge wenu mlisema kanunuliwa. Leo Mayor wa CCM anaungana na wabunge wenu kuponda ilani na maelekezo ya Chama chake mnaona kuwa ni sawa.

  Naomba muongozo: Hivi unaweza kuwa diwani/Meya na ukaendelea na ajira yako serikalini?. Maana huyu Meya bado anaendelea na kazi TRA, asubuhi anaripoti kinondoni, then gari ya manispaa Kinondoni inampeleke TRA. Je hapo ni halali pia?.

  KItilya alivyoulizwa kuhusu hilo la mtu kuwa MEya na kuwa mtumishi wa umma, alijibu kwa kifupi kuwa suala la huyu bwana linashughulikiwa na ngazi za juu... je ni sawa hapo pia?

  Jamaa ameamua kuside na CDM kwa vile anajua watamlinda ktk soo hiyo.

  CCM angalieni jamani ilani haitekelezwi tena, watu hawafanyi kazi tena..... angalieni CDM ni wajanja sana, wana tawala Baraza kwa mlango wa nyuma
   
Loading...