Imekuwa mazoea kwa serikali ya CCM kuwafungulia kesi za jinai viongozi wapinzani ambao ni tishio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imekuwa mazoea kwa serikali ya CCM kuwafungulia kesi za jinai viongozi wapinzani ambao ni tishio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 25, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0  Leo hii viongozi wa Chadema wamefikishwa tena mahakamani Arusha katika kesi yao ile iliyotokana na maandamano. Kuna baadhi wamebadilishiwa charges.

  Lakini swali langu hapa ni kwa nini huu utawala wa CCM huku Bara (na hata kule Zenj) una mtindo wa kuhakikisha kwamba viongozi wakuu wa upinzani – na hasa kutoka chama/vyama ambavyo vinakuwa tishio – wanakabiliwa na kesi za jinai.

  Kesi zenyewe basi si kesi wala chochote, ni namna tu ya kuwavuruga kisaikolojia kwani tangu vyama vingi vianze sijaona kesi za wakuu hawa wa upinzani wakiishia jela – labda Mtikila pekee, naye hahesabiwi sasa kama mpinzani wa kweli na tishio kwa CCM.

  Tujikumbushe - niko radhi kusahihishwa au kuongeza orodha):

  * Maalim Seif na wenzake waliwahi kuwekwa ndani kutokana na kesi ya kukutwa na nyaraka za serikali. Hii ilikuwa mwanzoni tu mwa kuanzishwa kwa vyama vingi.

  * Lipumba amewahi kukabiliwa na kesi ya jinai kuhusu maandamano ingawa ilifutwa mapema.

  * Mrema alikuwa na kesi ya madai ya hongo ya milioni 900 na hatimaye kushinda. Nadhani ana kesi nyingine bado iko mahakamani kama sikosei, iwapo haitakuwa imefutwa.

  * Maalim Seif alikuwa na kesi huko Zenj kuhusu kupatikana kwa silaha – nayo ilifutwa.

  * Viongozi 18 wa CUF walikuwa na kesi ya ‘uhaini' wakati wa utawala wa Dr Salmini – nayo ilikuja futwa.

  * Sasa hivi akina Slaa na wenzake wana kesi hiyo ya Ars – nayo haitafika popote.

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Siyo hapa Tanzania peke yake -- hata nchi nyingine zenye tawala za kidikteta kama vile Zimbabwe. Yule Tzvangirai amekuwa kila mara akikabiliwa na kesi za jinai.

  Sababu kubwa ni namna jinsi vyama tawala vinapokosa hoja za kuwajibu wapinzani -- hukimbilia kutumia nguvu za doila kuwadhibiti.
   
Loading...