Imekaaje Rais kubadilishiwa msaidizi tena ugenini?

Hii nchi ina vichaa wengi sana wanaojifanya wajuaji.
Juzi mmoja kaja hapa eeehh inakuwaje Rais wetu apokelewe na Waziri wa mambo ya nje!!!!
Hata kukujibu naona kazi ila shortly fahamu kuwa watu wanajua kuliko wewe unayejifanya unajua kisa kijiweni kwako wanakuona kichwa.
Baadhi ya watu sijui mnaumwa utindio wa ubongo! Inamaana kuhoji ni ujuaji..?
Mkuu huo utaratibu sidhani Kama unafanyika kwa viongozi wote mfano rais wa marekani ama Russia!
Ifike hatua watu muwe mnafikiri vyakutosha sio unaandika tu.
 
Swali ulilouliza ni la ajabu mkuu .. sorry lakini kwa kusema hivi maana inaonekana una hasira
 
Baadhi ya watu sijui mnaumwa utindio wa ubongo! Inamaana kuhoji ni ujuaji..?
Mkuu huo utaratibu sidhani Kama unafanyika kwa viongozi wote mfano rais wa marekani ama Russia!
Ifike hatua watu muwe mnafikiri vyakutosha sio unaandika tu.

..Raisi wa Marekani haambatani ni askari anayevaa kijeshi na anayefanya kazi kama mpambe. Kwa hiyo akija hapa Tz hutaona amepewa mpambe toka Jwtz.

..Suala la ulinzi wa kiongozi wa nje anayetembelea Tz hufanyika kwa ushirikiano kati walinzi wa kiongozi husika na walinzi toka Tz.

NB

..miaka ya zamani mpambe wa Rais wa Tz alikuwa akitokea ktk jeshi la Polisi. Sijui kwanini utaratibu ulikuwa hivyo na sijui kwanini ulibadilishwa.
 
Ungeuliza utaratibu wa usaidizi wa raisi awapo ugenini upoje. Ni vizuri kuonyesha hujui jambo usilo na uhakika nalo kabla hujalijadili.
 
Hii nchi ina vichaa wengi sana wanaojifanya wajuaji.
Juzi mmoja kaja hapa eeehh inakuwaje Rais wetu apokelewe na Waziri wa mambo ya nje!!!!
Hata kukujibu naona kazi ila shortly fahamu kuwa watu wanajua kuliko wewe unayejifanya unajua kisa kijiweni kwako wanakuona kichwa.
Tuvumiliane tu ndugu. Kuna issue unaweza kuiona ndogo sana lakini mwingine kwake ni tofauti ndio maana ANASHANGAA.

Mfano hata Mimi kuna jambo niliona tofauti na nilivyozoea huku.

NI HIVI

Mama akiwa Kenya alipokuwa anakagua gwaride aliloandaliwa nilishangaa kuona anapita kukagua bila wale walinzi wanaovaa suti. Yaani aliambatana na wale wajeshi wa Kenya tu. Tofauti na tulivyozoea huku Rais akikagua lazima suti nyeusi ziambatane naye.

Pia aliyehusika kufungua mlango wa gari na kufunga ni yule mjeshi wa kike wa Kenya tofauti na huku kwetu kazi hiyo hufanywa na mtu wa suti nyeusi
 
Na ajabu huko Kenya walinzi wa mama wame wavutia sana wa kalenjing na luos na kikuyuz nilikuwa napitia online news yaan wakenya wanataman sasa na wao wapate rais mwana mama eti waone ulinzi
 
Watapata tu..
 
Rais anapotembelea nchi nyingine ni jukumu la nchi mwenyeji kuhakikisha usalama wa mgeni. Lolote baya likimtokea ugenini nchi mwenyeji itawajibika kwa kushindwa kuhakikisha usalama:
 
Mkuu KENZY

Pole sana. Umeuliza swali lakini badala ya kujibiwa umeishilia kuambiwa swali la kijinga.

Nitakueleza kwa kadri ninavyojua:
Ulinzi wa viongozi wakuu wa nchi wanaotembelea katika nchi za kigeni unakuwa chini ya idara mahususi kwa ulinzi wa viongozi wa Umma katika nchi mwenyeji. Mfano, akitembelea Tanzania basi ulinzi unakuwa chini ya TISS.

Vivyo hivyo utambue kuwa Mpambe wa Rais (ADC), ni muwakilishi wa jeshi husika mahala popote alipo Rais.

Sasa kwa Protokali, Rais anapokuwa ugenini basi jeshi la nchi husika ndiyo linawakilishwa. Na ndiyo maana, akiwa katika shughuli maalum katika nchi husika basi huambatana na ADC kutoka katika jeshi la nchi husika.

Walinzi wake alioambatana nao pia huwepo katika ulinzi lakini kwa muongozo wa ulinzi aliopewa katika nchi husika.

Hii ni kwa sababu, ulinzi hauanzii kwenye ule mzunguko tu unaouona.. Ulinzi huanzia kwa ukusanyaji wa intelijensia, uchakataji wa taarifa na ulinzi wenyewe. Ile circle ni hatua ya mwisho kabisa.

Sasa, wenye jukumu la kufanya hivyo ni idara husika katika nchi husika.. Kufanya ujasusi ndani ya nchi nyingine ni kosa kubwa sana kidiplomasia..

Pia, walinzi wa maafisa wa Serikali wa nchi mwenyeji wanaufahamu zaidi wa mazingira wa nchi yao kuliko wageni.

Na pia kwa kuzingatia kuwa, Rais akipatwa na matatizo katika nchi ya kigeni basi wanaowajibika ni nchi mwenyeji. Kwa hiyo wana haki kuhakikisha usalama wa Rais na wasaidizi wake kwa kila namna..
 
Mkuu ahsante kwa ufafanuzi..
 
Back
Top Bottom