Imekaaje hii? Rais kukabidhiwa mkoba wa pesa ikulu

MamaParoko

JF-Expert Member
Jan 14, 2008
463
60
Mwakilishi wa Televisheni ya Emmanuel ya The Synagogue Church Of All Nations, Martha Harvey akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete mkoba wenye Sh milioni 25 kwa ajili ya waathirika wa ajali ya meli ya mv Spice Islanders iliyozama na kusababisha vifo vya mamia ya watu hivi karibuni. Mchango huo uliokabidhiwa Ikulu, Dar es Salaam, ulitolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo, Nabii Themitope Balogun Joshua, ambaye anaishi makao makuu ya kanisa hilo Lagos, Nigeria. (Picha na habarileo).

kikwete.jpg

My Take:

Kuna kitu hakipo sawa, rais kukabidhiwa mkoba wa mahela ikulu!
Hii imakaaje wadau?
 
Zile suti 5 mbona hakupiga picha akikabidhiwa? Au kwa kuwa zenyewe zilikuwa ni rushwa!
 
swali: kwanini rahisi akabidhiwe fedha in cash ikulu?

MODE PLEASE DO THE NEEDFUL NILIKUWA SIJAONA POST INGINE KUHUSIANA NA SUALA HILI!
 
Serikali ya JK iko too curative than preventive....... Kitu ambacho ni kibaya sana.

Anyway, EL alishaenda kusali kwa TB Joshua na yule mama alieibua sakata la Katibu Mkuu wa Nishati nae alienda kusali aliporudi akasema amehakikishiwa na TB Joshua kwamba Rais ajaye ni EL. Huwezi jua labda EL anamtumia Joshua kutimiza hiyo ndoto. Huenda pia ni yeye EL alietoa hizo fedha.... Kila kitu kinawezekana. Kwa majanga yote Africa na huko Nigeria sijawahi sikia atoe msaada km huo.... Kuelekea 2015 tutaona na kushuhudia mengi tu.
 
Binafsi sioni tatizo. Kapelekewa sasa angekataa msaada? Swali ni kama zitawafikia walengwa. Kama hazitawafikia ndio tulaumu.
 
Mwenye kanisa hili si ndiye aliyemtakasa Mh. Edward Ngoyai Lowasa au?
 
Kwa hakika Bongo haitakuja kuisha kufanya mambo kibongobongo; milioni 25 CASH???!!! Kwani Kanisa halina account benki? Je Ikulu, yaani yule mzee (jina limenitoka) Katibu Mkuu Kiongozi, haikutaarifiwa hizo pesa zitaletwa kwa njia gani ambapo wangeweza kumshauri mama wa watu kukabidhi cheki badala ya mkoba!!! bongobongo tu!! Je hizi ni PESA SAFI??????????????????????????????????????:disapointed:
 
hizi ni pesa chafu kama zingekua safi kwa nini mil 25 akabidhiwe mtu cash? kama sio njia ya kuzisafisha sijui
 
Mkwerè lazima Atakula pesa hizo., kama alivyokula pesa za epa na desi.
 
Kwani huo msaada mpaka upige piche na rais?
Wangepeleka kitengo cha maafa ofisi ya PM kunakohusika na majanga
 
Haaa jamani sasa picha zikuwa za nini wangepeana tu kimya kimya manake mpango wenyewe kama danganya toto vilee,anywayz time will tell tuone bro atakuja na mikakat gani kwa hao wahanga, ataibuka kama clouds na maboya au atanunua maharagwe na sembe!na akiendahuko pia asisahau kupiga picha
 
Haaa jamani sasa picha zikuwa za nini wangepeana tu kimya kimya manake mpango wenyewe kama danganya toto vilee,anywayz time will tell tuone bro atakuja na mikakat gani kwa hao wahanga, ataibuka kama clouds na maboya au atanunua maharagwe na sembe!na akiendahuko pia asisahau kupiga picha,,,'karibu ningesahau na huko pande ya pili watakubali misaada toka kanisani!! Teheheee kazi ipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom