Imekaaje hii? Ex boyfriend anaposhindwa kumove on

Meridah Tough

Member
Nov 27, 2017
98
250
Habarini ndugu zangu?
Mimi binafsi kuna jambo linalonisumbua kichwa.
Kuna ex boyfriend wangu ambaye toka tulipoanza kudate, nikiri tu kuwa ilikuwa na mahusiano yenye furaha na amani. Tulishirikiana kwa kila jambo hadi kuna kipindi tulifikia kuwaza ndoa.
Sababu za kuachana kwetu ni watu. Ambapo hakuna kosa nililomfanyia mwenzangu na pia kuniacha pasipo kosa ni jambo ambalo liliniumiza sana lakini baada ya muda kupita nikaona ni sawa. Kila mtu akachukua hamsini zake.
Tatizo linakuja hapa. Huyu ex haonyeshi dalili zozote za kuondoka katika maisha yangu.
Attention yake yote uwa ananipa mimi na hata akidate na wadada wengine, uwa ananitafuta kuniambia madhaifu yao.
Sina maajabu yoyote na wala sina uzuri wa kutisha, ni mdada wa kawaida sana.
Nimejiuliza sana maswali pasipo kuwa na majibu. Hata yeye nikimuuliza hana jibu lolote la maana.
Ndugu zangu ambao mnaweza kunifafanulia situation ya namna hii na jinsi ya kuepukana nayo.
Kubadili namba za simu siwezi kwa sababu ni za kazi pia lakini pia ni mtu ambaye sina uwezo wa kupotea maishani mwake sababu anajua nyumbani na ndugu zangu pia wanajuana na sometimes wanatafutana.
Ahsanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom