Imekaaje CDF kumpigia salute Mkuu wa Wilaya?

ni utaratibu tu, haumshushi CDF kwa namna yeyote ile. Hata akifa askari wa chini yake, hata koplo, maiti yake CDF ataipigia saluti. Ni utaratibu tu
Naongezea nyama hata angekufa raia tu wa kawaida.Na CDF ameshiriki kuaga mwili akiwa amevaa sare ni lazima apige salute.
 
Mi naona CDF atulie kwenye combania zake za kijeshi kama ma CDF wa zamani.
Kitendo cha kumwona mara kwa mara CDF akiwapigia saluti watu mbali mbali na mnavyosema hata maiti ni kuipunguza imani yake kwa wananchi.
CDF anahudhuriaje vikao vidogo vidogo vinanvyo ondoa imani yetu kwake.?
CDF anatakiwa asionekane kabisa mitaani na akionekana labda anapita kweye msafara ndani ya gari za kijeshi.

Washauri wake please zingatieni hizi nasaha.
 
Hii imekaaje CDF anampigia salute DC?

View attachment 1493174
Dah,hapa nimeikumbuka kauli ya kiongozi mmoja aliyesema
''Baba yangu aliniamkia shikamoo,nilipomuuliza,kuliko akasema sikuamkii wewe,ila hii shikamoo ni ya madaraka''
sasa hapa napo huenda saluti hii ni ya kitu kingine ambacho sisi hatuwezi kujua,angalia vizuri sura za wanaozunguka eneo la tukio.
 
DC Ni muwakilishi wa President
its very true, japo imekaa vibaya sana kwa baadhi ya matukio. Kuna wakuu wa wilaya na mikoa nchini ambao ni wanajeshi. Kicheo cha kijeshi, wako chini ya CDF, ila inambidi CDF ampigie saluti kwa vile huyu ni mwakilishi wa Amri jeshi mkuu.
 
Back
Top Bottom