Imefika wakati viongozi wa dini waitishe wito wa kuombea haki

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Viongozi wa dini mara zote wamekuwa wakihimiza au wao wakiombea taifa kuwa na amani.Hata hivyo tumeambiwa amani ni tunda la haki,na sisi tunahitaji tuendelee kuvuna tunda hilo.

Nadhani imefika wakati viongozi hawa wafikirie kuombea haki na waache unafiki wanaouonesha sasa.

Kuna uzoefu wa watu wenye mamlaka kujisahau na kupoka haki za watu wao.Hata viongozi wa dini wapo wanaonyanyasa wafanyakazi wao katika taasisi zilizo chini ya dini zao mfano hospitali na mashule.

Viongozi hawa wa dini wanaongoza kunyanyasa watumishi kijinsia,kikabila,na hata kunyima haki kibabe tu kwa vile wanajua huna mahali pa kuwashitaki.

Ukiachilia mbali matendo ya dhuluma yansyofanywa na waliopewa dhamana ya kutawala,kwa kujua ama kutojua,viongozi wa dini wamekuwa wakichangia sana kuamsha hasira za watu kupigania hicho kinachoonekana kunyimwa maksudi bila kufuata misingi ya sheria ama kwa kufuata sheria kandamizi.

Natoa wito kwa viongozi hawa,waitishe kongamano la kuombea haki. Haki huinua taifa
 
Mithali 34:14
Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote. OVA
 
Back
Top Bottom